Yule Ambaye Anataja Mazuri Ya Watu Wa Bid´ah Anasambaza Bid´ah

Manhaj ya Ahl-us-Sunnah ni mtu kuwasusia Ahl-ul-Bid'ah ili waache Bid’ah zao. Ikiwa mtu hatowagomea, basi itakuwa unawasaidia na kukubaliana na wanayoyafanya na kuwadanganya wengine. Ikiwa wanachuoni na wale viigizo bora watawagomea, watu pia watakuja kuwatenga. Itakuja pia kusababisha wahisi aibu kwa watu. Ndio maana watu wa Bid’ah walikuwa wanajificha wakati wa Maswahabah na zile karne bora. Watu wa Bid’ah walianza kujitokeza katika karne ya nne baada ya zile karne bora kutoweka. Haifai kusema kama jinsi wajinga wa leo wanavyosema, haki ni kuwa ni lazima mtu ataje kwanza mazuri ya watu wa Bid’ah kisha Bid’ah zao. Wao huita Muwaazanaat, haki sawa. Kwa njia hii huenea Bid’ah. Sisi hatujaamrishwa kutaja yale mema mazuri. Hilo tumuachie nalo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Isitoshe, vipi tutakuwa tunajua mazuri yao na kwamba kweli yanachukuliwa vizuri na Allaah? Sisi hatujaamrishwa hilo. Sisi tulichoamrishwa tu ni kuonyesha makosa ili watu waepukane nayo na ili mtu huyoaje kutubia kwa Allaah ('Azza Wa Jalla) ikiwa Allaah Anamtakia mazuri. Kutaja sifa zake nzuri kunawafanya watu kuchukulia Bid’ah ni kitu chepesi.

Manhaj ya Ahl-us-Sunnah ni mtu kuwasusia Ahl-ul-Bid’ah ili waache Bid’ah zao. Ikiwa mtu hatowagomea, basi itakuwa unawasaidia na kukubaliana na wanayoyafanya na kuwadanganya wengine.

Ikiwa wanachuoni na wale viigizo bora watawagomea, watu pia watakuja kuwatenga. Itakuja pia kusababisha wahisi aibu kwa watu. Ndio maana watu wa Bid’ah walikuwa wanajificha wakati wa Maswahabah na zile karne bora. Watu wa Bid’ah walianza kujitokeza katika karne ya nne baada ya zile karne bora kutoweka.

Haifai kusema kama jinsi wajinga wa leo wanavyosema, haki ni kuwa ni lazima mtu ataje kwanza mazuri ya watu wa Bid’ah kisha Bid’ah zao. Wao huita Muwaazanaat, haki sawa.

Kwa njia hii huenea Bid’ah. Sisi hatujaamrishwa kutaja yale mema mazuri. Hilo tumuachie nalo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Isitoshe, vipi tutakuwa tunajua mazuri yao na kwamba kweli yanachukuliwa vizuri na Allaah? Sisi hatujaamrishwa hilo.

Sisi tulichoamrishwa tu ni kuonyesha makosa ili watu waepukane nayo na ili mtu huyoaje kutubia kwa Allaah (‘Azza Wa Jalla) ikiwa Allaah Anamtakia mazuri. Kutaja sifa zake nzuri kunawafanya watu kuchukulia Bid’ah ni kitu chepesi.


  • Author: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan. Sharh Lum’at-il-I’tiqaad, Uk. 269
  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj-ul-Muwaazanah (Mfumo wa haki sawa)
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013