Wazazi Kuwachunga Bara Bara Watoto Wa Kike

´Allaamah al-Fawzaan: Wasichungwe watoto wa kiume peke yap, bali khasa wanawake; kwa kuwa mabanati wamekuwa kama watoto wa kiume siku hizi. Wanatoka kwenda kwenye Madrasah, sokoni n,k bali ndio wanaotoka zaidi kuliko wanaume. Unakuta watoto wa kiume mara nyingi wamelala zao nyumbani kutokana na tabu nk, lakini mabanati hawalali. Wako juu kwa kutoka. Na Shaytwaan kawapambia hilo na anawatetea katika kutoka. Wao ndio aula zaidi kuhifadhiwa, kunasihiwa na kudhibitiwa. Kwa kuwa wao ni fitnah. Fitnah yao ni kubwa kuliko fitnah ya watoto wa kiume. Inatakiwa kuwa makini juu ya mabanati. Na ni wajibu kwa walii [muangalizi] wa mabanati kuwaangalia, kuwachunga na kuwafuatilia. Hatari kwao ni kubwa - khasa kwenye zama hizi ambazo imekithiri mchanganyiko wa wanawake na wanaume n,k - fitnah na makemeo ni kubwa. Ni juu ya mawalii wa mabanati kuwaangalia, kuwafuatilia na kuwadhibiti kweli kweli kwa kuwa wao ni amaanah. Kuharibika kwa binti kunaharibu familia yote. Familia na nyumba inaharibika yote. Binti huyu anakuwa hana tena thamani kwenye jamii; anakuwa maiti. Mauti yake ni jambo kubwa kuliko mauti ya kuondokwa na haya; anakuwa maiti wa haya, dini na tabia. Ni juu ya walii wa binti aombe kinga kwa Allaah, asubiri na amfuatilie hadi hapo atakapomsalimisha kwa mume wake (kumuozesha). Atakapokujieni yule ambaye mmemridhia dini yake na tabia yake, mumsalimishe kwake kwa ndoa. Kama hakufanya hivyo basi yeye atakuwa mwenye kuulizwa juu yake [huyo binti].

´Allaamah al-Fawzaan:

Wasichungwe watoto wa kiume peke yap, bali khasa wanawake; kwa kuwa mabanati wamekuwa kama watoto wa kiume siku hizi. Wanatoka kwenda kwenye Madrasah, sokoni n,k bali ndio wanaotoka zaidi kuliko wanaume.
Unakuta watoto wa kiume mara nyingi wamelala zao nyumbani kutokana na tabu nk, lakini mabanati hawalali. Wako juu kwa kutoka. Na Shaytwaan kawapambia hilo na anawatetea katika kutoka. Wao ndio aula zaidi kuhifadhiwa, kunasihiwa na kudhibitiwa. Kwa kuwa wao ni fitnah. Fitnah yao ni kubwa kuliko fitnah ya watoto wa kiume. Inatakiwa kuwa makini juu ya mabanati.

Na ni wajibu kwa walii [muangalizi] wa mabanati kuwaangalia, kuwachunga na kuwafuatilia. Hatari kwao ni kubwa – khasa kwenye zama hizi ambazo imekithiri mchanganyiko wa wanawake na wanaume n,k – fitnah na makemeo ni kubwa.

Ni juu ya mawalii wa mabanati kuwaangalia, kuwafuatilia na kuwadhibiti kweli kweli kwa kuwa wao ni amaanah. Kuharibika kwa binti kunaharibu familia yote. Familia na nyumba inaharibika yote. Binti huyu anakuwa hana tena thamani kwenye jamii; anakuwa maiti. Mauti yake ni jambo kubwa kuliko mauti ya kuondokwa na haya; anakuwa maiti wa haya, dini na tabia.

Ni juu ya walii wa binti aombe kinga kwa Allaah, asubiri na amfuatilie hadi hapo atakapomsalimisha kwa mume wake (kumuozesha). Atakapokujieni yule ambaye mmemridhia dini yake na tabia yake, mumsalimishe kwake kwa ndoa. Kama hakufanya hivyo basi yeye atakuwa mwenye kuulizwa juu yake [huyo binti].