Waungu Wa Watu Wa Zamani Na Wa Watu Wa Leo

“Laa ilaaha illa Allaah” maana yake ni hapana mungu mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Kutanguliza “kwa haki” ni jambo la kidharurah. Mwenye kusema kuwa maana yake ni hapana mwenye kuabudiwa isipokuwa Allaah pasina kuweka neno “kwa haki” amekosea na hafahamu maana ya “laa ilaaha illa Allaah”. Kwa kuwa maana yake ni kwamba amekanusha (kutokuwepo kwa) vinavyoabudiwa vyote kabisa. Ukweli wa mambo sivyo. Vinavyoabudiwa vipo katika kila wakati. Lakini mwenye kuabudiwa kwa haki ni Allaah Mmoja. Hii ndio maana Shahaadah ndani yake mna kufuru na imani. Kukufuru vinavyoabudiwa na anayeabudiwa badala ya Allaah na badala yake kumwamini Allaah Mmoja. Hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah Mmoja, ama vinavyoabudiwa na wanaoabudiwa, tangu watu walipoanza kuabudu masanamu mpaka hivi leo, uabudiwa wao ni wa batili. Kilugha wote hao wanaitwa “miungu”. Waarabu walikuwa wanawaita “miungu” (Aalihah). Watu leo wakati walipokosa kuijua lugha hawawaiti miungu, badala yake wanawaita “Mashaykh, watu wema, mawalii na makaburi”. Majina yamebadilishwa. Ni waungu. Kila kinachoabudiwa badala ya Allaah hata kama itakuwa ni mti, jiwe, Shaytwaan au mtu mwema, hakuna tofauti. Hakuna tofauti kati ya mtu kuabudu mtu mwema au akaabudu Shaytwaan na mtu muovu. Wote hawa ni waungu wa batili ambao hawastahiki ´ibaadah hata kama watakuwa ni katika watu wema. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 37 Toleo la: 25-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

“Laa ilaaha illa Allaah” maana yake ni hapana mungu mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Kutanguliza “kwa haki” ni jambo la kidharurah. Mwenye kusema kuwa maana yake ni hapana mwenye kuabudiwa isipokuwa Allaah pasina kuweka neno “kwa haki” amekosea na hafahamu maana ya “laa ilaaha illa Allaah”. Kwa kuwa maana yake ni kwamba amekanusha (kutokuwepo kwa) vinavyoabudiwa vyote kabisa. Ukweli wa mambo sivyo. Vinavyoabudiwa vipo katika kila wakati. Lakini mwenye kuabudiwa kwa haki ni Allaah Mmoja. Hii ndio maana Shahaadah ndani yake mna kufuru na imani. Kukufuru vinavyoabudiwa na anayeabudiwa badala ya Allaah na badala yake kumwamini Allaah Mmoja. Hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah Mmoja, ama vinavyoabudiwa na wanaoabudiwa, tangu watu walipoanza kuabudu masanamu mpaka hivi leo, uabudiwa wao ni wa batili. Kilugha wote hao wanaitwa “miungu”.

Waarabu walikuwa wanawaita “miungu” (Aalihah). Watu leo wakati walipokosa kuijua lugha hawawaiti miungu, badala yake wanawaita “Mashaykh, watu wema, mawalii na makaburi”. Majina yamebadilishwa. Ni waungu. Kila kinachoabudiwa badala ya Allaah hata kama itakuwa ni mti, jiwe, Shaytwaan au mtu mwema, hakuna tofauti. Hakuna tofauti kati ya mtu kuabudu mtu mwema au akaabudu Shaytwaan na mtu muovu. Wote hawa ni waungu wa batili ambao hawastahiki ´ibaadah hata kama watakuwa ni katika watu wema.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 37
Toleo la: 25-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Imani, Kufuru na Shirki
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 25th, May 2014