Watakaoingia Peponi Pasina Hesabu Watafufuliwa Uchi Na Kupita Kwenye Swiraat?

Muulizaji: Yule ambaye ataingia Peponi pasina hesabu hali kadhalika atafufuliwa akiwa migu peku na uchi? Jibu: Hadiyth iko wazi ya kwamba kila mtu atafufuliwa akiwa peku na uchi kwamba watatoka ndani ya makaburi yao wakiwa katika sifa hii. Wa mwanzo wao atayetoka ni Ibraahiym kama ilivyokuja katika Hadiyth. Muulizaji: Hali kadhalika watapita kwenye Swiraat? Jibu: Ndio. Kila mtu atapita kwenye Swiraat. Lakini upitaji wa juu ya Swiraat unatofautiana. Kuna ambao watapita kama umeme, kwa kiasi ambacho hawatohisi kitu na kusibiwa na kitu.

Muulizaji: Yule ambaye ataingia Peponi pasina hesabu hali kadhalika atafufuliwa akiwa migu peku na uchi?

Jibu: Hadiyth iko wazi ya kwamba kila mtu atafufuliwa akiwa peku na uchi kwamba watatoka ndani ya makaburi yao wakiwa katika sifa hii. Wa mwanzo wao atayetoka ni Ibraahiym kama ilivyokuja katika Hadiyth.

Muulizaji: Hali kadhalika watapita kwenye Swiraat?

Jibu: Ndio. Kila mtu atapita kwenye Swiraat. Lakini upitaji wa juu ya Swiraat unatofautiana. Kuna ambao watapita kama umeme, kwa kiasi ambacho hawatohisi kitu na kusibiwa na kitu.