Wasomaji Ruqyah Wanaotumia Jini

Kuko watu wanaotumia majini na Mashaytwaan na wanaongea nao. Majini hayo yanawaambia “umefikwa na kadhaa na fulani ndiye ambaye kakufanyia hivi.” Wanasema kuwa jini hili ni miongoni mwa Waislamu. Wewe umejuaje kuwa jini hili ni katika Waislamu? Isitoshe ni kwamba haijuzu kutaka msaada kutoka kwa majini. Kwa kuwa ni viumbe ambavyo havionekani. Hatuvioni sisi. Haijuzu kutaka msaada kutoka kwa mtu ambaye haonekani wala kutoka kwa maiti. Kutaka msaada kunakuwa kwa mtu ambaye yuko hai na yuko mbele yako (unamtaka msaada) kwa yale anayoyaweza. Ama yule anayeelezea mambo ya ghaibu, huyu ni katika makuhani. Haijuzu kumuuliza, haijuzu kumsadikisha, haijuzu kumwendea na wala haijuzu kutaamiliana nae kwa njia yoyote.

Kuko watu wanaotumia majini na Mashaytwaan na wanaongea nao. Majini hayo yanawaambia “umefikwa na kadhaa na fulani ndiye ambaye kakufanyia hivi.” Wanasema kuwa jini hili ni miongoni mwa Waislamu. Wewe umejuaje kuwa jini hili ni katika Waislamu?

Isitoshe ni kwamba haijuzu kutaka msaada kutoka kwa majini. Kwa kuwa ni viumbe ambavyo havionekani. Hatuvioni sisi. Haijuzu kutaka msaada kutoka kwa mtu ambaye haonekani wala kutoka kwa maiti. Kutaka msaada kunakuwa kwa mtu ambaye yuko hai na yuko mbele yako (unamtaka msaada) kwa yale anayoyaweza. Ama yule anayeelezea mambo ya ghaibu, huyu ni katika makuhani. Haijuzu kumuuliza, haijuzu kumsadikisha, haijuzu kumwendea na wala haijuzu kutaamiliana nae kwa njia yoyote.