Wasifu Wa Shaykh ‘Ubayd al-Jaabiriy

JINA LAKE NA KUZALIWA: Jina lake ni ' Ubayd bin ´Abdillaah bin Sulaymaan al-Hamdaaniy al-Jaabiriy kutoka katika kabila la Banuu Jaabir linatoka katika kabila la Harbiy Hijaaz. Amezaliwa katika kijiji cha al-Faqiyr katika maeneo ya Waadiy' Far´ karibu na Madiynah katika wa 1357 B.H. MASOMO YAKE: Alihama pamoja na baba yake Mahd-udh-Dhahab katika mwaka wa 1365 B.H. na akaanza kusoma katika shule ya msingi, baadaye akahamia Madiynah katika wa 1374 B.H. ambako alilazimika kusitisha masomo kwa muda fulani. Shaykh baadaye alianza kusoma katika shule Daar-ul-Hadiyth Madiynah, na baadaye al-Ma'had al-'Ilmiy na baadaye akaendelea katika kitovu cha Shari´ah na akakhitimu katika mwaka wa 1392 B.H. kwa shahada ya juu na alikuwa mwanafunzi bora katika miaka yote ya shule. Akachukua shahada ya udaktari (Ph.D) katika Tafsiyr. WAALIMU WAKE: 1) Shaykh 'Abdul-´Aziyz bin Baaz, Muftiy wa Saudi Arabia wa kabla. Shaykh Falaah amesema kuwa alikuwa katika watu wa karibu na Shaykh Ibn Baaz . 2) Shaykh Hammaad al-Answaariy, mwanachuoni mkubwa katika elimu ya Hadiyth. 3) Shaykh 'Abdul-Kariym Muraad, mmoja katika wanachuoni wakubwa wa Hadiyth Pakistan. WANAFUNZI WAKE: Shaykh ana wanafunzi wengi ambao walisoma kwake wakati alipokuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah, na wanafunzi wengine wengi ambao wamesoma kwake kwenye Msikiti wake. Miongoni mwao ni: 1) Shaykh Falaah Ismaa´iyl, mwanachuoni mkubwa kutoka Kuwait alisoma kwa Shaykh 'Ubayd wakati alikuwa mwanafunzi Madiynah. 2) Shaykh 'Abdullaah al-Bukhaariy, mmoja katika waalimu maarufu katika elimu ya Hadiyth katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah. KAZI ZAKE: 1) Alianza kama Daa'iy wa Wazaarat-ul-Awqaaf, Muftiy na alikuwa makamu wa mkurugenzi wa Da'wah Markaz kati ya mwaka wa 1396 B.H. mpaka mwaka wa 1404 B.H. 2) Alikuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah kati ya mwaka wa 1404 B.H. mpaka mwaka wa 1417 B.H. SIFA ZA WANACHUONI KWAKE: Shaykh Rabiy' al-Madkhaliy alisema juu yake: "Shaykh 'Ubayd ni katika wanachuoni wa kwanza wa kisalafi na anajulikana kwa kujiepusha kwake na mambo ya kutatanisha na kwa kuipa kwake nyongo dunia." Shaykh Swaalih as-Suhaymiy alisema juu yake: "Shaykh 'Ubayd ni katika Mashaykh bora, kati ya wale wanaotafuta elimu na wanachuoni wakubwa."

JINA LAKE NA KUZALIWA:

Jina lake ni ‘ Ubayd bin ´Abdillaah bin Sulaymaan al-Hamdaaniy al-Jaabiriy kutoka katika kabila la Banuu Jaabir linatoka katika kabila la Harbiy Hijaaz.

Amezaliwa katika kijiji cha al-Faqiyr katika maeneo ya Waadiy’ Far´ karibu na Madiynah katika wa 1357 B.H.

MASOMO YAKE:

Alihama pamoja na baba yake Mahd-udh-Dhahab katika mwaka wa 1365 B.H. na akaanza kusoma katika shule ya msingi, baadaye akahamia Madiynah katika wa 1374 B.H. ambako alilazimika kusitisha masomo kwa muda fulani. Shaykh baadaye alianza kusoma katika shule Daar-ul-Hadiyth Madiynah, na baadaye al-Ma’had al-‘Ilmiy na baadaye akaendelea katika kitovu cha Shari´ah na akakhitimu katika mwaka wa 1392 B.H. kwa shahada ya juu na alikuwa mwanafunzi bora katika miaka yote ya shule. Akachukua shahada ya udaktari (Ph.D) katika Tafsiyr.

WAALIMU WAKE:

1) Shaykh ‘Abdul-´Aziyz bin Baaz, Muftiy wa Saudi Arabia wa kabla. Shaykh Falaah amesema kuwa alikuwa katika watu wa karibu na Shaykh Ibn Baaz .

2) Shaykh Hammaad al-Answaariy, mwanachuoni mkubwa katika elimu ya Hadiyth.

3) Shaykh ‘Abdul-Kariym Muraad, mmoja katika wanachuoni wakubwa wa Hadiyth Pakistan.

WANAFUNZI WAKE:

Shaykh ana wanafunzi wengi ambao walisoma kwake wakati alipokuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah, na wanafunzi wengine wengi ambao wamesoma kwake kwenye Msikiti wake. Miongoni mwao ni:

1) Shaykh Falaah Ismaa´iyl, mwanachuoni mkubwa kutoka Kuwait alisoma kwa Shaykh ‘Ubayd wakati alikuwa mwanafunzi Madiynah.

2) Shaykh ‘Abdullaah al-Bukhaariy, mmoja katika waalimu maarufu katika elimu ya Hadiyth katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah.

KAZI ZAKE:

1) Alianza kama Daa’iy wa Wazaarat-ul-Awqaaf, Muftiy na alikuwa makamu wa mkurugenzi wa Da’wah Markaz kati ya mwaka wa 1396 B.H. mpaka mwaka wa 1404 B.H.

2) Alikuwa mwalimu katika chuo kikuu cha Kiislamu Madiynah kati ya mwaka wa 1404 B.H. mpaka mwaka wa 1417 B.H.

SIFA ZA WANACHUONI KWAKE:

Shaykh Rabiy’ al-Madkhaliy alisema juu yake: “Shaykh ‘Ubayd ni katika wanachuoni wa kwanza wa kisalafi na anajulikana kwa kujiepusha kwake na mambo ya kutatanisha na kwa kuipa kwake nyongo dunia.”

Shaykh Swaalih as-Suhaymiy alisema juu yake: “Shaykh ‘Ubayd ni katika Mashaykh bora, kati ya wale wanaotafuta elimu na wanachuoni wakubwa.”


  • Author: Mukhtasari pamoja na baadhi ya nyongeza kutoka http://www.ajurry.com/TarjamaObid.htm na mapendekezo yake yamechukuliwa kutoka mafaili ya sauti.
  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 23rd, February 2014