Wasifu Wa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy

JINA LAKE Ni Shaykh al-´Allaamah al-Muhaddith Rabiy´ bin Haadiy bin Muhammad ´Umayr al-Madkhaliy, kutoka kabila la al-Madaakhilah ambayo ni maarufu katika eneo la kusini mwa Jaazaan Saudi Arabia, ambayo chimbuko lake ni kutoka katika kabila la al-Qahtwaan. KUZALIWA KWAKE NA MWANZO WA MASOMO YAKE Alizaliwa katika kijiji cha al-Jaraadiyyah ambacho ni kijiji kidogo kilichopo kilomita tatu mwa magharibi ya mji katika Swaamitwah mwaka 1351 H [1]. Baba yake alifariki alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu, hivyo akalelewa na mama yake ambaye alitumia juhudi kubwa katika malezi yake. Alipokuwa na umri wa miaka minane alianza kujifunza kusoma, kuandika na akaanza kuhifadhi Qur-aan kwa wanachuoni waliokuwa wakieshi katika wilaya yake. Ndipo akaanza kusoma kwenye madrasah ambayoyalikuwepo karibu na Swaamitwah ambapo wanachuoni wakubwa walikuwa wakifundisha hapo, kama Shaykh Naaswir Mubaarakiy, Shaykh al-Haafidhw al-Hakamiy, Shaykh Ahmad an-Najmiy na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy. Kisha alihamia Riyadh na kusoma pale kwa muda mfupi katika kitivo cha Shari'ah ili baadaye asafiri kwenda kusoma katika Chuo kikuu kipya cha Kiislamu kilichokufunguliwa Madiynah. WAALIMU WAKE KATIKA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU MADIYNAH 1) Shaykh 'Abdul-´Aziyz bin Baaz, Muftiy wa zamani wa Saudi Arabia na mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa zama hizi. Alisoma al-'Aqiydah atw-Twahaawiyyah pamoja naye. 2) Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Mwanachuoni mkubwa wa Hadiyth katika zama hizi. Alisoma elimu ya Hadiyth na isnadi pamoja naye. 3) Shaykh Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy, mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa Tafsiri. Alisoma Tafsiri pamoja naye kwa miaka minne. 4) Shaykh 'Abdul-Ghaffaar al-Hindiy, mmoja wa wanachuoni wakubwa India katika Hadiyth. Alisoma elimu ya Hadiyth na Mustwalah pamoja naye. Shaykh alifanya kazi baadaye kama mwalimu kwa muda, na kisha aliendelea masomo yake ya juu na alichukua shahada ya pili, na shahada ya udaktari katika Chuo Kikuu cha ´Abdul-´Aziyz cha kitengo cha Makkah katika somo la Hadiyth. Shaykh baadaye akawa Profesa katika Hadiyth na mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Madiynah katika kitengo cha Sunnah. WANAFUNZI WAKE Shaykh ana wanafunzi wengi na baadhi yao sasa huchukuliwa ni katika Wanachuoni. Baadhi yao ni: 1) Shaykh Swaalih as-Suhaymiy, ni mwalimu katika Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Madiynah. 2) Shaykh Falaah Ismaaiyl, Mwanachuoni wa Kuwait. 3) Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy, mmoja katika Wanachuoni maarufu Madiynah [2]. VITABU VYAKE Shaykh ameandika vitabu vingi juu ya elimu ya Hadiyth na kupiga Radd vipote potevu, vikundi na watu binafsi. Idadi ya vitabu alivyoandika ni zaidi ya thelathini. Ingawa Shaykh ana zaidi ya miaka themanini, hata hivyo bado anaendelea mpaka hivi leo kuandika vitabu ili alinde Sunnah. SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE Kutokana na Shaykh kupiga Radd vipote vingi, vikundi na watu binafsi, hivyo alipata maadui wengi. Kwa ajili hiyo Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunnah wamemtetea na kumsifu yeye na vitabu vyake. Miongoni mwa Wanachuoni wakubwa ambao walimsifu wa miaka ya karibuni ni: 1) Shaykh Ibn Baaz amesema: “Shaykh Rabiy´ ni katika vigogo kabisa wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa'ah. Ni maarufu ya kuwa ni katika Ahlus-Sunnah. Vitabu vyake na maandiko yake ni maarufu.” 2) Shaykh al-Albaaniy kasema: "Sisi, bila shaka tunamhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Kujaalia katika Da´wah hii njema, iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa Manhaj ya Salafus-Swaalih Ma-Du´aat katika miji mbali mbali ya Kiislamu ambao wanasimama kwa Fardh al-Kifaayah, faradhi ambayo wamekuwa wachache wenye kusimama kwayo katika ulimwengu wa Kiislamu wa leo. Kwa hivyo, hawa Mashaykh wawili watukufu, Madu´aat wawili wanaolingania katika Qur-aan na Sunnah na juu ya yale waliyosimamia Salafus-Swaalih, na kupigana vita na wale ambao wanakwenda kinyume na Manhaj hii sahihi, ni kama mnavyojua nyote (kuhusiana na watu hawa wanaowaponda) ni mmoja ya watu wawili, ima ni: 1) Jaahil (Mjinga), au 2) Swaahibu Hawaa (mtu wa matamanio) Mjinga kama nilivyotangulia kusema, anaweza kuongozwa kwa urahisi, kwa kuwa mtu aina hii hudhani ana elimu fulani – na wakati itambainikia elimu sahihi ataongoka... Ama kwa mtu wa matamanio, hatuna juu yetu njia nyingine isipokuwa ikiwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atamuongoza. Hawa watu wanaowasema vibaya (wanaoponda) hawa Mashaykh wawili, ni kama tulivyosema, ima ni mjinga afunzwe; na ima ni mtu wa matamanio, Aombwe Allaah Atukinge na shari yake na tunamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ima Amuongoze au amvunje mgongo wake.” 3) Shaykh Ibn 'Uthaymiyn amesema: “Shaykh Rabiy´ ni katika Wanachuoni wa Sunnah, ni katika watu wema. ´Aqiydah yake ni salama na Manhaj yake ni yenye nguvu. Lakini wakati alipoanza kuzungumzia baadhi ya mambo ya watu waliokuja baadaye, hivyo ndo wakamshutumu na mambo (utata) haya.” Chanzo: Tovuti ya Shaykh www.rabee.net na baadhi ya nyongeza. Na Sifa za Wanachuoni wengine zinapatikana katika kitabu "Sifa kuu za Wanachuoni kwa Shaykh Rabiy´ cha Shaykh Khaalid adh-Dhufayriy ambapo kataja Maulmaa na Mashaykh 16 walivyosema kuhusu Shaykh.

JINA LAKE
Ni Shaykh al-´Allaamah al-Muhaddith Rabiy´ bin Haadiy bin Muhammad ´Umayr al-Madkhaliy, kutoka kabila la al-Madaakhilah ambayo ni maarufu katika eneo la kusini mwa Jaazaan Saudi Arabia, ambayo chimbuko lake ni kutoka katika kabila la al-Qahtwaan.

KUZALIWA KWAKE NA MWANZO WA MASOMO YAKE
Alizaliwa katika kijiji cha al-Jaraadiyyah ambacho ni kijiji kidogo kilichopo kilomita tatu mwa magharibi ya mji katika Swaamitwah mwaka 1351 H [1]. Baba yake alifariki alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu, hivyo akalelewa na mama yake ambaye alitumia juhudi kubwa katika malezi yake. Alipokuwa na umri wa miaka minane alianza kujifunza kusoma, kuandika na akaanza kuhifadhi Qur-aan kwa wanachuoni waliokuwa wakieshi katika wilaya yake. Ndipo akaanza kusoma kwenye madrasah ambayoyalikuwepo karibu na Swaamitwah ambapo wanachuoni wakubwa walikuwa wakifundisha hapo, kama Shaykh Naaswir Mubaarakiy, Shaykh al-Haafidhw al-Hakamiy, Shaykh Ahmad an-Najmiy na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy.
Kisha alihamia Riyadh na kusoma pale kwa muda mfupi katika kitivo cha Shari’ah ili baadaye asafiri kwenda kusoma katika Chuo kikuu kipya cha Kiislamu kilichokufunguliwa Madiynah.

WAALIMU WAKE KATIKA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU MADIYNAH
1) Shaykh ‘Abdul-´Aziyz bin Baaz, Muftiy wa zamani wa Saudi Arabia na mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa zama hizi. Alisoma al-‘Aqiydah atw-Twahaawiyyah pamoja naye.
2) Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Mwanachuoni mkubwa wa Hadiyth katika zama hizi. Alisoma elimu ya Hadiyth na isnadi pamoja naye.
3) Shaykh Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy, mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa Tafsiri. Alisoma Tafsiri pamoja naye kwa miaka minne.
4) Shaykh ‘Abdul-Ghaffaar al-Hindiy, mmoja wa wanachuoni wakubwa India katika Hadiyth. Alisoma elimu ya Hadiyth na Mustwalah pamoja naye.

Shaykh alifanya kazi baadaye kama mwalimu kwa muda, na kisha aliendelea masomo yake ya juu na alichukua shahada ya pili, na shahada ya udaktari katika Chuo Kikuu cha ´Abdul-´Aziyz cha kitengo cha Makkah katika somo la Hadiyth. Shaykh baadaye akawa Profesa katika Hadiyth na mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Madiynah katika kitengo cha Sunnah.

WANAFUNZI WAKE
Shaykh ana wanafunzi wengi na baadhi yao sasa huchukuliwa ni katika Wanachuoni. Baadhi yao ni:
1) Shaykh Swaalih as-Suhaymiy, ni mwalimu katika Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Madiynah.
2) Shaykh Falaah Ismaaiyl, Mwanachuoni wa Kuwait.
3) Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy, mmoja katika Wanachuoni maarufu Madiynah [2].

VITABU VYAKE
Shaykh ameandika vitabu vingi juu ya elimu ya Hadiyth na kupiga Radd vipote potevu, vikundi na watu binafsi. Idadi ya vitabu alivyoandika ni zaidi ya thelathini. Ingawa Shaykh ana zaidi ya miaka themanini, hata hivyo bado anaendelea mpaka hivi leo kuandika vitabu ili alinde Sunnah.

SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE
Kutokana na Shaykh kupiga Radd vipote vingi, vikundi na watu binafsi, hivyo alipata maadui wengi. Kwa ajili hiyo Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunnah wamemtetea na kumsifu yeye na vitabu vyake. Miongoni mwa Wanachuoni wakubwa ambao walimsifu wa miaka ya karibuni ni:
1) Shaykh Ibn Baaz amesema:
“Shaykh Rabiy´ ni katika vigogo kabisa wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Ni maarufu ya kuwa ni katika Ahlus-Sunnah. Vitabu vyake na maandiko yake ni maarufu.”

2) Shaykh al-Albaaniy kasema:
“Sisi, bila shaka tunamhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Kujaalia katika Da´wah hii njema, iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa Manhaj ya Salafus-Swaalih Ma-Du´aat katika miji mbali mbali ya Kiislamu ambao wanasimama kwa Fardh al-Kifaayah, faradhi ambayo wamekuwa wachache wenye kusimama kwayo katika ulimwengu wa Kiislamu wa leo.
Kwa hivyo, hawa Mashaykh wawili watukufu, Madu´aat wawili wanaolingania katika Qur-aan na Sunnah na juu ya yale waliyosimamia Salafus-Swaalih, na kupigana vita na wale ambao wanakwenda kinyume na Manhaj hii sahihi, ni kama mnavyojua nyote (kuhusiana na watu hawa wanaowaponda) ni mmoja ya watu wawili, ima ni:
1) Jaahil (Mjinga), au
2) Swaahibu Hawaa (mtu wa matamanio)
Mjinga kama nilivyotangulia kusema, anaweza kuongozwa kwa urahisi, kwa kuwa mtu aina hii hudhani ana elimu fulani – na wakati itambainikia elimu sahihi ataongoka…
Ama kwa mtu wa matamanio, hatuna juu yetu njia nyingine isipokuwa ikiwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atamuongoza.
Hawa watu wanaowasema vibaya (wanaoponda) hawa Mashaykh wawili, ni kama tulivyosema, ima ni mjinga afunzwe; na ima ni mtu wa matamanio, Aombwe Allaah Atukinge na shari yake na tunamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ima Amuongoze au amvunje mgongo wake.”

3) Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn amesema:
“Shaykh Rabiy´ ni katika Wanachuoni wa Sunnah, ni katika watu wema. ´Aqiydah yake ni salama na Manhaj yake ni yenye nguvu. Lakini wakati alipoanza kuzungumzia baadhi ya mambo ya watu waliokuja baadaye, hivyo ndo wakamshutumu na mambo (utata) haya.”

Chanzo: Tovuti ya Shaykh www.rabee.net na baadhi ya nyongeza. Na Sifa za Wanachuoni wengine zinapatikana katika kitabu “Sifa kuu za Wanachuoni kwa Shaykh Rabiy´ cha Shaykh Khaalid adh-Dhufayriy ambapo kataja Maulmaa na Mashaykh 16 walivyosema kuhusu Shaykh.


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 18th, October 2013