Wasifu Wa Shaykh Muqbil bin Haadiy al-Waadi’iy

Mimi natoka Waadi´iyah, ambapo ni sehemu ya mashariki ya mji wa Sa´adah kutoka bonde la Dammaaj. Jina langu ni Muqbil bin Haadiy bin Muqbil bin Qaa´idah al-Hamdaaniy al-Waadi´iy al-Khallaaliy, kutoka kabila la ´Aaliy Raashiyd.[1] Sifa zote zinamstahiki Allaah, wengi wa watu wa Waadi´iyah, ambao ni majirani wa Sa´adah walinitetea mimi na Da´wah. Baadhi yao walikuwa wanataka kutetea Dini wakati wengine walikuwa wakitetea kabila lao. Lau ingelikuwa si Allaah kwanza, kisha wao, maadui wa Da'wah (Salafi), khaswa Mashia wa Sa´adah, wasingeliacha nyuma yetu ishara yoyote au athari ya sisi. Nitataja baadhi ya mifano yao ambayo namuomba Allaah Awalipe kwayo, moja wapo ilikuwa wakati mimi nilikuwa nakabiliwa na upinzani mkali katika Msikiti wa Haadiy kwa sababu nilikuwa nawatoa watu katika Da´wah huko (ya Kishia). Kwa hiyo baadhi ya watu wa Waadi´iyah na wengine walisimama na mimi kwa uhakika kwa kiasi ambacho Allaah Alininisuru kupitia mikono yao. Mashia walitaka kunisimamishia hukumu dhidi yangu. Hapa ilikuwa ni wakati wa Ibraahiym al-Hamdiy. Na watu waovu miongoni mwa wakomunisti na Mashia wakasimamisha vichwa vyao na nikafungwa kwa muda wa siku kumi na moja katika mwezi wa Ramadhaan. Takriban vijana khamsini kutoka Waadi´iyah walikuwa wakija kunitembelea gerezani wakati wa baadhi ya usiku, wakati watu wengine mia na khamsini walikuwa wakija gerezani kuwaghasi walinzi wa jela katika usiku hizi, waliendelea hivyo kiasi kwamba walinzi walichoshwa nawakanitoa jela, himidi zote ni za Allaah. Mfano mwingine ni kwamba maadui wa Da´wah wakati mwingine walikuwa wakija Dammaaj pamoja na silaha zao, hivyo watu wa Dammaaj walikuwa wakiwafukuza na kulazimishwa kuondoka kwa fedheha. Mfano mwingine ni wakati wa safari zetu. Wakati nilikuwa nasema: Tunataka kusafiri.Walikuwa wakishindana -Allaah Awahifadhi– ili kuona ni nani atakayeongozana na mimi na kunilinda. Hivyo wakati mwingine tulikuwa tukitoka nje na baadhi ya safari zetu zilikuwa na magari takriban 15! Kipindi cha muda huu, Da´wah ilikuwa inaendelea kwa namna nzuri kwa sababu - himidi zote ni za Allaah – nilikuwa na umri mkubwa. Pengine katika hatua hii nilikuwa nimefikisha umri wa miaka 62. Hivyo kulikuwa na ukimya na mashauri kutoka kwa watu ambao wanapenda Da´wah jambo ambalo lilinipelekea katika wema na kunihifadhi dhidi ya maadui, ambao hawakuwa na lolote zaidi ya matusi na uvukaji mipaka. Wakati wa duruus zangu pia, kuandika na kutoa Da´wah, sikuwa na uwezo wa kupata muda wa kushughulika na hawa maadui. Hivyo niliwaacha waseme watakalo kwani madhambi yangu ni mengi, pengine kwa sababu ya kashfa (matusi) yao, dhambi zangu zitakuwa zikifutwa na badala yake zikianguka juu ya mabega yao. DURUUS ZANGU NA WAALIMU WANGU: Nilisoma katika shule mpaka nilipokamilisha mtaala wa shule. Kisha muda mrefu ukapita bila ya mimi kutafuta elimu tangu wakati ambapo kulikuwa hakuna mtu ambaye angeweza kunihamasisha au kunisaidia katika kutafuta elimu. Hivyo nikatafuta elimu katika Msikiti wa al-Haadiy lakini sikusaidiwa kwa hilo. Baada ya muda fulani, niliiacha nchi yangu (ya Yemen) na nikaenda katika ardhi tukufu (Makkah/Madiynah) na Najd. Nilikuwa nikisikiliza wahubiri na nikipenda Khutbah zao. Hivyo nikatafuta ushauri kwa baadhi ya wahubiri juu ya vitabu gani naweza kununua? Wakanishauri niweze kupata Swahiyh al-Bukhaariy, Buluwgh al-Maraam, Riyaadh asw-Swaalihiyn, na Fath-ul-Majiyd, Sharh ya Kitaab at-Tawhiyd. Na wakanipa nakala ya vitabu vya kozi ya Tawhiyd. Wakati huo, nilikuwa nikifanya kazi kama mlinzi wa jengo moja huko Makkah, na hivyo nilikuwa nikishikamana barabara na vitabu hivyo, na hivyo nilikuwa nikichanganyikiwa kwa sababu mambo waliyokuwa wakifanya watu katika nchi yetu yalikuwa yakienda kinyume na mambo yaliyokuwa katika vitabu hivi; khaswa Fath-ul-Majiyd. Baada ya muda kupita, nikarudi katika nchi yangu na nikaanza kukemea kila kitu nilichokuwa naona kinaenda kinyume na yaliyokuwemo katika vitabu hivyo; kama vile kuchinja kwao badala ya kumchinjia Allaah, kuyajengea makaburi, na kuwaomba marehemu. Hivyo habari hizi zikawafikia Mashia na wakaanza kushambulia vikali yale niliyosimamia. Mmoja wao alikuwa anaweza kusema (Hadiyth): “Yeyote ambaye atabadilisha Dini yake, basi muueni.” Mwengine akatuma barua kwa watu wa familia yangu kusema: “Ikiwa hamtomzuia, basi tutamfunga jela.” Lakini baada ya hilo, wakakubaliana mimi kuingia Msikiti wa Haadiy ili kusoma pamoja nao, ili pengine waweze kuondoa fikira potofu zilizonipata kwenye moyo wangu! Hivyo, baada ya hilo, nilikubali kusoma pamoja nao katika Msikiti wa Haadiy. Kiongozi wa elimu alikuwa ni Jaji Mutahhir Hanash. Nilisoma kitabu cha al-´Aqd-uth-Thamiyn na ath-Thalaathiyn Mas-alah, pamoja na maelezo ya Haabis. Miongoni mwa waalimu walionifundisha alikuwa ni Muhammad bin Hasan al-Mutamayyiz. Siku moja tulikuwa tukijadili mada ya kuhusu kuonekana kwa Allaah Aakhirah, hivyo akaanza maskhara na kumkejeli Ibn Khuzaymah na ma-Imaam wengine wa Ahl-us-Sunnah, lakini nilikuwa nikificha Iymaan yangu. Pamoja na kwamba, nilikuwa dhaifu mno kwa kuweka mkono wangu wa kulia juu ya mkono wangu wa kushoto wakati wa Swalah, na nilikuwa nikiswali kwa kuiachilia mikono yangu. Tulisoma nakala za al-Azhaar hadi katika sehemu ya ndoa. Nilisoma maelezo ya Shari´ah kuhusu Mirathi kutoka katika kitabu kikubwa kilichokuwa katika kiwango cha ngazi ya juu, lakini sikustafidi kwacho. Hivyo nikaona ya kwamba vitabu vilivyotolewa havikuwa na manufaa, isipokuwa Sarufi, tangu niliposoma vitabu al-Aajruumiyyah na Qatr an-Nadaa na wao. Kisha nikamuomba Jaji, Qaasim bin Yahyaa ash-Shuwayl, kunifundisha Buluwgh al-Maraam. Hivyo tukakianza, lakini baadae harukukubaliwa, hivyo tukakiacha. Hivyo, nilipoona vitabu vinavyotolewa kwa ajili ya masomo vilikuwa ni vitabu vyenye asili ya Kishia na Mu´tazilah, nikakubali tu kuchukua vitabu vya Sarufi. Hivyo nikasoma Qatr an-Nadaa mara kadhaa chini ya Ismaa´iyl al-Hatbah (Rahimahu Allaah), katika Msikiti ambapo nilikuwa nikiishi na nikiswali humo. Alikuwa akitupa muda mwingi na umakini. Wakati mmoja, Muhammad bin Huuriyyah alikuja Msikitini na nikamshauri kuachana na utabiri wa nyota. Hivyo akawaambia watu hapo wanitupe nje ya barnamiji za masomo, lakini wakaniombea kwa niaba yangu na akanyamaza kimya. Baadhi ya Mashia walikuwa wakinipita wakati mimi nilipokuwa nasoma Qatr an-Nadaa na kutoa maneno ya kwamba elimu haitokuwa na athari yoyote kwangu. Lakini sikuwajali, nilikuwa nikibaki zangu kimya na kunufaika na vitabu vya Sarufi. Niliendelea hivyo hadi mapinduzi yalipoanza Yemen, wakati tuliacha nchi na makazi yetu Najraan. Huko nilisoma na Abul-Husayn Majd-ud-Diyn al-Mu´iyd na nikastafidi kutoka kwake khaswa katika lugha ya Kiarabu. Nikabaki Najraan kwa muda wa miaka miwili. Baada ya mimi kuwa na uhakika kwamba vita kati vyama vya kisiasa (Yemen) ilikuwa ni kwa ajili ya sababu za kidunia, nikaamua kwenda katika ardhi tukufu (Makkah/Madiynah) na Najd. Niliishi Najd kwa mwezi mmoja na nusu katika shule ya kuhifadhi Qur-aan, iliyokuwa ikiendeshwa na Shaykh Muhammad bin Sinaan al-Hadaa´iy. Alikuwa mkarimu sana kwangu kwa sababu aliona kuwa nastafidi kwa elimu. Akanishauri nibaki kwa muda mpaka aliponituma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu (cha Madiynah). Lakini mazingira ya Riyaadh yalinibadilikia na nikaamua kufasiri kwenda Makkah. Nilikuwa nafanya kazi wakati nilipokuwa nikiipata, na nilikuwa natafuta elimu wakati wa usiku, nikihudhuria duruus za Shaykh Yahyaa bin ´Uthmaan al-Paakistaaniy za Tafsiyr ya Ibn Kathiyr, Swahiyh al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim. Nilikuwa nikipitia vitabu kadhaa na huko nilikutana na Mashaykh watukufu wawili katika Wanachuoni wa kutoka Yemen: Wa kwanza: Jaji, Yahyaa al-Ashwal. Nilisoma Subul-us-Salaam cha Swan´aaniy pamoja naye na akinifunza somo lolote nililokuwa nikimuomba. Wa pili: Shaykh ´Abd-ur-Razzaaq ash-Shaahidhiy al-Muhwaytiy. Alikuwa akinifunza pia kitu chochote nilichokuwa ninamuomba kwacho. Kisha taasisi ya elimu Makkah ikafunguliwa na nikafanya mtihani wa kujiunga pamoja na kundi la wanafunzi, na mimi nikapasi, himidi zote ni za Allaah. Aliyekuwa akijulikana sana katika waalimu wetu alikuwa ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz as-Subayyal. Mimi, pamoja na kundi la wanafunzi kutoka Chuo hicho, tulikuwa tunasoma pia na Shaykh ´Abdullaah bin Muhammad bin Humayd (Rahimahu Allaah), kitabu at-Tuhfah as-Saniyyah baada ya ´Ishaa katika Haram. Alikuwa (Rahimahu Allaah) akileta nukta nyingi zenye faida kutoka kwa Ibn ´Aqiyl na maelezo mengine ya Wanachuoni. Masomo yalikuwa katika kiwango cha juu kwa wenzangu, wakaanza kukimbia mpaka hapo aliposimamisha darasa. Nilisoma pia pamoja na kundi la wanafunzi na Shaykh Muhammad as-Subayyal (Rahimahu Allaah), somo la Shari´ah kuhusu Mirathi. Baada ya kukaa katika Chuo kwa muda fulani, nilitoka kwenda katika familia yangu Najraan. Kisha nikawaleta kuishi pamoja nami Makkah. Tukaishi huko pamoja kwa muda mrefu wa masomo yangu katika Chuo na katika Haram yenyewe, ambayo ilidumu kwa miaka sita. Baraka ya kusoma katika Misikiti inajulikana. Usiulize kuhusu mazingira ya kirafiki na utulivu tuliyokuwa tukihisi katika Misikiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kweli wakati aliposema: “Kundi la watu halikusanyiki katika moja ya Nyumba (Msikiti wa) Allaah, wakisoma Kitabu cha Allaah na wakakizingatia baina yao, isipokuwa huteremka juu yao utulivu, Malaika huwazunguka, Rahmah huwaenea, na Allaah Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja naye.” Hivyo nilikuwa natumia siku kusoma katika Chuo hicho, na masomo yote yalinisaidia Iymaan yangu na Dini. Kisha kutoka baada ya ´Aswr mpaka baada ya Swalah ya ´Ishaa, nilikuwa nikienda Haram na kunywa maji ya Zamzam, ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuhusu maji hayo: “Kwa hakika, ni kinywaji kinachoshibisha na ni tiba ya maradhi.” Na tulikuwa tunasikiliza wahubiri wanaokuja Makkah kutoka katika nchi mbalimbali kufanya Hajj au ´Umrah. Miongoni mwa waalimu tuliojifunza kutoka Haram kati ya Maghrib na ´Ishaa ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Raashid an-Najdiy, mwandishi wa kitabu Taysiyr-ul-Wahyayn fil-Iqtiswaar ´alal-Qur-aani wasw-Swahiyhayn, ambacho kina makosa na hatukubaliani na yeye kwacho. Alikuwa akisema (Rahimahu Allaah): “Ahaadiyth ambazo ni Swahiyh ambazo hazipatikani katika mkusanyiko wa Swahiyhayn (al-Bukhaariy na Muslim) zinaweza kuhesabika na vidole vya mtu mmoja.” Hii kauli yake haikutoka akilini mwangu tangu nilipokitilia umuhimu. Hii ilikuwa njia yote mpaka nilipoamua kuandika as-Swahiyh-ul-Musnad mimmaa laysa fiys-Swahiyhayn baada ya kuwa na uhakika kuhusu ubatili wa kauli yake (Rahimahu Allaah). Miongoni mwa waalimu wangu wa Msikiti Mkuu (Haram) wa Makkah ambaye nilistafidi kutoka kwake ni Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah as-Sumaaliy, kwa maana nilihudhuria masomo yake kwa miezi saba au zaidi. Na alikuwa ni ishara katika istilaha ya elimu ya wapokezi wanaotumiwa na Mashaykh wawili (al-Bukhaariy na Muslim). Nilistafidi kiasi kikubwa kutoka kwake katika Sayansi ya Hadiyth. Himidi zote ni za Mola Wangu, tangu nilipoanza kutafuta elimu, sipendi kitu chochote isipokuwa elimu ya Kitabu na Sunnah. Baada ya kumaliza ngazi za kati na sekondari ya taasisi ya elimu Makkah, na baada ya kumaliza masomo yangu yote ya Dini, nikaenda Madiynah katika Chuo Kikuu cha Kiislamu huko. Wengi wetu walihamishwa katika Kitivo cha Da´wah na Usuul-ud-Diyn.Katika wale wanaojulikana sana waliotufunza ni: Shaykh as-Sa´iyd Muhammad al-Hakiym na Shaykh Mahmuud ´Abdul-Wahhaab Faa´iyd, wote ni kutoka Misri. Wakati wa likizo unapokuja, nakhofia wakati usipotee bure hivyo najiunga na Kitivo cha Shari´ah, kutokana na sababu mbili, ya kwanza ambayo ilikuwa ni kupata elimu: Hii ilikuwa wakati tangu baadhi ya madarasa huko yalikuwa ni yakupasi wakati mengine yalikuwa yakikutana (na nilivyosema hapo kabla). Hivyo ilikuwa ni kama marudio ya yale tuliyosoma katika Kitivo cha Da´wah. Nilikamilisha Kitivo cha kazi zote mbili, himidi zote ni za Allaah, na nilipewa digrii mbili. Hata hivyo, sifa zote ni za Allaah, sivipi umuhimu vyeti; kile nilichokuwa najali mimi ni elimu. Katika mwaka huo huo nilipomaliza kozi katika vyuo viwili, nilisonga mbele, na masomo ya juu ya shahada ya pili ambayo ilikuwa imefunguliwa katika Chuo Kikuu cha Kiislamu. Basi, nikawa nimeenda kwa ajili ya mtihani wa mahojiano na nikapita, himidi zote ni za Allaah. Masomo ya kiwango cha juu ilikuwa ni Sayansi ya Hadiyth. Himidi zote ni za Allaah, nikasoma somo ambalo nilikuwa nalipenda zaidi. Watu maarufu zaidi katika wale waliokuwa wakitufundisha ilikuwa ni Shaykh Muhammad al-Amiyn al-Misriy (Rahimahu Allaah), Shaykh as-Sa´iyd Muhammad al-Hakiym al-Misriy, na wakati wa sehemu ya mwisho ya masomo yangu, Shaykh Hammaad bin Muhammad al-Answaariy. Katika baadhi ya usiku, nilikuwa napenda kuhudhuria duruus za Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz kwenye Msikiti wa Mtume (Madiynah) juu ya somo la Swahiyh Muslim. Nilikuwa napenda pia kuhudhuria mkusanyiko wa vikao vya Shaykh Al-Albaaniy, ambavyo vilikuwa ni maalum kwa watafutaji wa elimu tu, ili kujifunza kutoka kwake. Pindi nilipokuwa Makkah, nilikuwa nafundisha baadhi ya watafutaji wa elimu kutoka katika vitabu Qatr-un-Nadaa na at-Tuhfah as-Saniyyah. Na wakati nilipokuwa Madiynah, nilikuwa nafundisha baadhi ya ndugu zangu kitabu at-Tuhfah as-Saniyyah kwenye Msikiti wa Mtume. Kisha nikawaahidi ndugu zangu Waislamu kwamba nitashikilia duruus katika Jaamiy´ (Sunan) ya at-Tirmidhiy, Qatr-un-Nadaa na al-Baa´ith-ul-Hathiyth kwa ajili yao katika nyumba yangu baada ya ´Aswr. Hivyo, wimbi kubwa la Da´wah likaenea Madiynah, ambalo lilijaza dunia kwa muda wa miaka sita. Ilikuwa ni baadhi ya watu wa haki ndio walichukua jukumu la kugharamia, wakati Muqbil bin Haadiy na ndugu zake Waislamu ndio walichukua jukumu la kuwafundisha ndugu zao wengine. Ama kusafiri kwa madhumuni ya kulingania kwa Allaah katika mikoa yote ya Mamlaka (Saudi), hili lilikuwa wakisaidizana ndugu wote watafutaji wa elimu ili mtu aweze kupata elimu na kunufaisha wengine, na mtu wa kawaida ili naye aweze kujifunza. Hii ilikuwa kama kwamba wengi wa watu wa kawaida wananufaika kwalo na kuzidi kuipenda Da´wah (ya Salafi). Mmoja katika ndugu zetu Waislamu miongoni mwa watafutaji wa elimu alikuwa ni Imaam wa Msikiti wa Riyaadh. Siku moja baadhi ya watu watafutaji wa elimu walimkemea kwa kutumia kwake Sutrah. Basi akasema: “Hatuna uwezo mbele yenu, lakini naapa, si mwengine zaidi isipokuwa mtu wa kawaida ndiye ambaye anaweza kukufundisha Ahaadiyth kuhusiana na Sutrah.” Basi, akaita ndugu katika watu wa ujumla aliyekuwa akipenda Da´wah na alikuwa amehifadhi Ahaadiyth kuhusiana na Sutrah kutoka katika al-Lu´lu´ wal-Marjaan fiymataffaqa ´alayhi ash-Shaykhaan. Basi akajitokeza na akasimulia Ahaadiyth hizi, baada ya hapo wapinzani wakaona aibu na kukaa kimya. Baada ya hili, wafuasi wanaofuata kipofu na Wanachuoni wa uovu wakaanza kujipanga, na sababu hii wakachochea wafuasi vipofu, ambaye alikuwa anachukuliwa kuwa ni Mwanachuoni katika macho ya watu, kwa sababu ilikuwa wakati wowote wanapopata mwanafunzi kijana mtafutaji wa elimu miongoni mwa wanafunzi wetu na anaweza kutumia Hadiyth kama dalili, mwanafunzi huyu anawaambia: Mpokezi wa Hadiyth? Na hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa la kawaida. Kisha alikuwa akiwaambia: Daraja ya Hadiyth? Hili lilikuwa pia ni jambo lisilokuwa la kawaida. Basi walikuwa wakiwaaibisha mbele ya watu. Wakati mwingine mwanafunzi anawaambia: Hii ni Hadiyth dhaifu. Hali ni hivi na hivi na mlolongo wake wa upokezi na vivyo hivyo kuihukumu kuwa ni dhaifu. Hivyo juu ya kusikia hivi, ni kama kwamba dunia isingekuwa na wapinzani wengi wafuataji kipofu. Na wakawa wanaenda kueneza uongo kwamba wanafunzi hawa ni Khawaarij, wakati kwa kweli ndugu hawakuwa katika Khawaarij ambao wanahalalisha kumwaga damu ya Waislamu na ambao wanawachukulia Waislamu kuwa ni makafiri kwa sababu ya hesabu ya madhambi. Hata hivyo, huko kulikuwa kunaweza kutokea baadhi ya makosa kwa upande wa baadhi ya ndugu wapya, na hii ilikuwa ni kwa sababu wanaoanza huzidiwa kila mara na bidii nyingi. Katika wakati huo, nilikuwa naandaa mtihani wangu wa shahada ya pili, ghafla usiku mmoja, kabla ya mimi kujua kitachotokea, wakanitia mbaroni mimi na wengine waliokamatwa karibu watu mia moja na khamsini. Baadhi ya watu walikuwa wako tayari kutoroka, lakini dunia ikatetemeka kati ya wale ambao wanapinga na wale wanaokubaliana na kukamatwa kwetu. Tukabaki gerezani kwa muda wa mwezi mzima au mwezi mmoja na nusu. Baada ya hapo tukaachwa huru, himidi zote ni za Allaah. Muda mfupi baada ya tukio hili, maandiko ya kundi la Juhaymaan yakatolewa na kundi katika sisi likakamatwa tena.[2] Wakati wa kuhojiwa, wakaniuliza: Je, ni wewe ndiye uliandika hivi? Nini, Juhaymaan hawezi kuandika? Hivyo nikakanusha hili, na Allaah Anajua kwamba sikuandika hivi na wala mimi sikushiriki sehemu yoyote katika hili. Lakini baada ya kukaa jela kwa miezi mitatu, amri ilitolewa ya kuwarejesha wageni makwao. Nilipofika Yemen, nikarudi kijijini kwetu na nikakaa huko kwa muda nikifundisha watoto Qur-aan. Kabla ya kujua hilo, ilionekana kama dunia nzima ilikuwa nje kwa vita dhidi yangu. Ilikuwa ni kama vile nimetoka nje kwa ajili ya kuharibu nchi, Dini na utawala. Wakati huo, sikuwa najua kiongozi yeyote au mkuu wa kikabila. Hivyo nilikuwa nikisema: “Allaah Ananitosheleza na ni Mlinzi wangu bora.” Wakati mambo yalipokuwa magumu, nilikuwa naenda San´aa au Haashid au Dhimmaar, na pia Tayiz, Ibb na Hudaydah kutoa Da´wah na kutembelea ndugu Waislamu. Baada ya siku kadhaa, baadhi ya watu wema walinitumia Maktabah yangu kutoka Madiynah. Wakatuma vitabu Sa´adah ambapo Sunnah ilikuwa imepamba moto. Baadhi ya wenzetu wakaenda kuomba vitabu vyangu, wakaambiwa: Njoo baada ya Dhuhr, In Shaa Allaah. Lakini aliyetoa ahadi ya kutoa vitabu hakurudi baada ya Dhuhr. Badala yake, baadhi ya waliohamasishwa na Mashia na walinzi wa usalama wakazuia hivyo vitabu kwa sababu vilikuwa ni vitabu walivyoita vya ‘Wahaabiy’! Usiulize kuhusu ada ya fedha, shida na dhuluma niliyokuwa nafanyiwa kama matokeo ya kujaribu kupata vitabu vyangu! Ndugu wengi wakaazi wa nchi yangu walifanya juhudi kubwa kufuatilia hilo, akiweno Shaykh ´Abdullaah bin Husayn al-Ahmar, Shaykh Hazaa´iy Dab´iyaan, msimamizi wa Kituo cha mwaongozo na ushauri, kama vile Jaji Yahyaa al-Fasayyal (Rahimahu Allaah), na ndugu ´Aa´iyd bin ´Aliy Mismaar. Baada ya shida ya muda mrefu, watu wa Sa´adah walituma telegrafu kwa Rais ´Aliy bin ´Abdillaah bin Swaalih, hivyo akampa kesi hakimu, ´Aliyas-Samaan. Jaji akanitumia barua na kuniahidi kwamba atanirudishia Maktabah yangu. Na akasema: Watu wa Sa´adah ni wakali sana. Wanawaita Wanachuoni wa Sa´adah kuwa ni makafiri. Hivyo nikaenda San´aa kuchukua vitabu vyangu. Allaah Aliamuru vitabu vyangu kufika huko wakati hakimu ´Aliy Samaan alikuwa nje ya nchi juu ya kazi fulani. Hivyo wakati baadhi ya ndugu walienda kuviomba, mkuu wa Wizara ya Waqf akawaambia: Vitabu hivi vinahitajia kuchunguzwa. Hivyo, baadhi ya ndugu zetu Waislamu katika Kituo cha Ushauri na uongofu wakahamasishwa na kwenda kuomba vitabu. Wakasema: Vitabu hivi viko chini ya mamlaka yetu. Lazima tuvichunguze. Tutavipeleka mpaka al-Waadi´iy na chochote kitachokiuka Dini, tutavichukua. Hivyo kwa kufanya hivyo, wakaja kugundua ya kwamba vitabu vilikuwa kweli ni vya kidini na wakanipa bila ya kuvikagua, Allaah Awalipe. Nikaleta vitabu kwenye mji wangu, himidi zote ni za Allaah. Na mtu wangu wa karibu, Allaah Amhifadhi, akajenga Maktabah ndogo na Msikiti mdogo. Na wakasema: Tutaswali Ijumaa hapa ili kuepuka uzito na matatizo. Wakati mwingine tulikuwa tunaswali hapo na (Jamaa´ah ya) watu wa sita waliohudhuria. Wakati mmoja gavana Haadiy al-Hashiyshi alinihitajia, hivyo nikaenda kwa Shaykh Qaa´iyd Majliy (Rahimahu Allaah), ambaye alimpigia simu na kumwambia: Unataka nini kutoka kwa al-Waadi´iy? Akasema: Hakuna, isipokuwa tu nataka kumjua. Hivyo akasema: Tutamtazama na Chuo chake. Katika hali nyingine, baadhi ya viongozi wengine waliniulizia na hivyo Husayn bin Qaa´iyd Majliy akaenda pamoja na mimi kumuona mtu huyo. Huyo (Majliy) akaanza kuzungumzia dhidi ya Mashia na akamuelewesha ya kwamba sisi tunalingania katika Qur-aan na Sunnah na kwamba Mashia wanatuchukia kwa sababu wanakhofia haki itatoka kuwahusu wao, hivyo kiongozi huyu akasema: Kwa hakika, Mashia wamechafua historia ya Yemen, hivyo maadamu Da´wah yenu ni kama mnavyosema, basi mlinganie na sisi tuko pamoja nanyi. Baada ya tukio hili, nikawa natumia muda katika Maktabah yangu. Baada tu ya siku chache kupita wakati baadhi ya ndugu wa Misri walipokuja na tukaanza duruus ya baadhi ya vitabu vya Hadiyth na lugha ya Kiarabu. Baada ya hili, wanafunzi wakaendelea kuja kutoka Misri, Kuwait, Ardhi Takatifu (Makkah na Madiynah), Najd, ´Aden, Hadhramaut, Algeria, Libya, Somalia, Ubelgiji, na nchi nyingine za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu. Idadi ya wanafunzi imefikia sasa kati ya mia sita mpaka mia saba ya wanafunzi, miongoni mwao ni familia mia na sabini.[3] Na Allaah ndiye Ambaye Alikuwa Akiwapa riziki. Na yote haya haikuwa kwa sababu ya nguvu zetu au utukufu wetu, wala kutokana na kiasi cha elimu yetu tuliyokuwa nayo au ujasiri wetu au ufasaha wa Khutbah. Badala yake, hili ni jambo ambalo Allaah Alipenda liwe. Hivyo alikuwa ni Yeye peke Yake (Sifa zote ni za Allaah) Ambaye Alitupatia baraka hii. [Mwisho wa Tafsiri ya maelezo ya wasifu wa Shaykh Muqbil kutoka kwake mwenyewe] KIFO CHAKE: Shaykh Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy alifariki tarehe 2 ya Jumaadal-Uwlaa, 1422H (07/21/2001) kutokana na ugonjwa wa ini ambalo lilimletea mateso kwa muda mrefu, na ambalo lilimfanya akasafiri kwenda Marekani, Ujerumani na Saudi Arabia wakati wa sehemu ya mwisho ya maisha yake kwa ajili ya kutafuta matibabu. Alikuwa takriban na umri wa miaka sabini alipokufa Jeddah. Swalah yake ya janaza iliswaliwa Makkah na alizikwa katika makaburi ya al-´Adl karibu na kaburi la Shaykh Ibn Baaz na Ibn al-´Uthaymiyn (Rahimahumu Allaah). SIFA ZA WANACHUONI KWAKE: Shaykh Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn kasema: “Mwambie ya kwamba mimi namchukulia yeye kuwa ni Mujaddid (Mwenye kuhuisha Diyn).” Shaykh Al-Albaaniy kasema: "Sisi, bila shaka tunamhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Kujaalia katika Da´wah hii njema, iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa Manhaj ya Salafus-Swaalih Ma-Du´aat katika miji mbali mbali ya Kiislamu ambao wanasimama kwa Fardh al-Kifaayah, faradhi ambayo wamekuwa wachache wenye kusimama kwayo katika ulimwengu wa Kiislamu wa leo. Kwa hivyo, hawa Mashaykh wawili watukufu, Madu´aat wawili wanaolingania katika Qur-aan na Sunnah na juu ya yale waliyosimamia Salafus-Swaalih, na kupigana vita na wale ambao wanakwenda kinyume na Manhaj hii sahihi, ni kama mnavyojua nyote (kuhusiana na watu hawa wanaowaponda) ni mmoja ya watu wawili, ima ni: 1) Jaahil (Mjinga), au 2) Swaahibu Hawaa (mtu wa matamanio) Mjinga kama nilivyotangulia kusema, anaweza kuongozwa kwa urahisi, kwa kuwa mtu aina hii hudhani ana elimu fulani – na wakati itambainikia elimu sahihi ataongoka... Ama kwa mtu wa matamanio, hatuna juu yetu njia nyingine isipokuwa ikiwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atamuongoza. Hawa watu wanaowasema vibaya (wanaoponda) hawa Mashaykh wawili, ni kama tulivyosema, ima ni mjinga afunzwe; na ima ni mtu wa matamanio, Aombwe Allaah Atukinge na shari yake na tunamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ima Amuongoze au amvunje mgongo wake.” [Mfululizo Silsilah al-Hudaa wan-Nuur: 1/851]. Shaykh Yahyaa al-Hajuwriy kapokea ya kwamba Shaykh Rabiy´al-Madkhaliy kasema juu yake: “Ni Mujaddid katika nchi ya Yemen na kwamba kasema: Hakuwezi kupatikana kutoka katika zama za ´Abdur-Razaaq as-Swan´aaniy katika zama zetu hizi mtu ambaye anasimamisha Da´wah imara na kuihuisha kama mfano wa al-Waadi´iy.”[4 Chanzo: Tarjamah Abiy ´Abdir-Rahmaan (uk. 16-29, pamoja na Mukhtaswar kidogo) [Toloe la pili; 1999] ----------------------------- [1] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Katika aliyoandika kuhusiana na historia ya baba yake, Umm ´Abdillaah al-Waadi´iyyah kasema, Baba yake alikufa wakati alipokuwa kijana mdogo na hakuwa anamjua. Hivyo alikua kama yatima na chini ya uangalizi wa mama yake kwa kipindi cha muda. Alikuwa (mama) akimuomba (baba) afanye kazi ili apate pesa, na akimuamrisha kuangalia hali ya jamii yake ili aweze kuwa kama wao. Lakini alikuwa akiyapuuza haya na kumwambia: Nitaenda kusoma. Hivyo (mama) akimwambia: Allaah Akuongoze. Akimuombea aongoke, kwa wanawake kadhaa ambao walikuwa wakati ule ndio walivyonambia. Pengine Du´aa yake ilikutana na wakati ambapo Du´aa hupokelewa tangu alipokuwa mmoja aliyeongozwa, na akaongoza wengine. [Nubdhah Mukhtaswarah: uk. 18]. [2] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Hili linamhusu Juhaymaan bin Muhammad al-´Utaybiy, mpotofu kutoka Saudi Arabia ambaye aliuteka nyara Msikiti Mkuu wa Makkah na mamia ya wafuasi katika mwaka wa 1979, na akaushikilia kwa siku kadhaa, baada ambapo Wanachuoni waheshimiwa wakaruhusu nguvu zitumike katika eneo tukufu la Ka´bah ili kurejesha Msikiti huo. Kundi la Walinzi wa Saudi la Taifa likawazingira takriban mnamo wiki mbili, baadaye baada ya damu nyingi kumwagika, na wengine kujeruhiwa katika mapambano ya waasi na jeshi la Saudi. Waasi waliobaki na kushikwa, walihukumiwa kuuawa. Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kamtaja huyu Juhaymaan katika kitabu chake as-Swahiyhah (5/872) akisema: Na mfano wa wafuasi wa Juhaymaan wa Saudi, ambaye alisababisha fitinakwenye Msikiti Mkuu wa Makkah mwanzoni wa mwaka 1400 (Hijriy). Alidai ya kwamba Mahdiy anayesubiriwa yuko pamoja naye na alitaka kutoka kwa wale waliopo Msikitini kumpa bay´ah (utiifu). Baadhi ya watu wenye akili fupi, wakaghafilika na watu waovu wakamfuata. Kisha Allaah Akamaliza fitinah hii baada ya kumwagika kiasi kikubwa cha damu ya Waislamu. [3] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Inatakikana ijulikane ya kwamba maneno haya hapa yamekuja tangu toleo la pili la wasifu wake, ambayo ilichapishwa mwaka wa 1.999. Tangu wakati huo idadi hii iliendelea kuongeza, kama ilivyo wakati wa sasa katika shule ya Shaykh, ambayo kwa sasa inafundisha na kusimamiwa na Shaykh Yahyaa al-Hajuuriyna ina wanafunzi karibu 1.000 na familia 500, himidi zote ni za Allaah. [4] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Maneno haya ni kutoka katika kitabu Nubdhah Mukhtaswarah cha bint wa Shaykh Muqbil, Umm ´Abdillaah (uk. 46).

Mimi natoka Waadi´iyah, ambapo ni sehemu ya mashariki ya mji wa Sa´adah kutoka bonde la Dammaaj. Jina langu ni Muqbil bin Haadiy bin Muqbil bin Qaa´idah al-Hamdaaniy al-Waadi´iy al-Khallaaliy, kutoka kabila la ´Aaliy Raashiyd.[1]

Sifa zote zinamstahiki Allaah, wengi wa watu wa Waadi´iyah, ambao ni majirani wa Sa´adah walinitetea mimi na Da´wah. Baadhi yao walikuwa wanataka kutetea Dini wakati wengine walikuwa wakitetea kabila lao. Lau ingelikuwa si Allaah kwanza, kisha wao, maadui wa Da’wah (Salafi), khaswa Mashia wa Sa´adah, wasingeliacha nyuma yetu ishara yoyote au athari ya sisi.

Nitataja baadhi ya mifano yao ambayo namuomba Allaah Awalipe kwayo, moja wapo ilikuwa wakati mimi nilikuwa nakabiliwa na upinzani mkali katika Msikiti wa Haadiy kwa sababu nilikuwa nawatoa watu katika Da´wah huko (ya Kishia). Kwa hiyo baadhi ya watu wa Waadi´iyah na wengine walisimama na mimi kwa uhakika kwa kiasi ambacho Allaah Alininisuru kupitia mikono yao. Mashia walitaka kunisimamishia hukumu dhidi yangu. Hapa ilikuwa ni wakati wa Ibraahiym al-Hamdiy. Na watu waovu miongoni mwa wakomunisti na Mashia wakasimamisha vichwa vyao na nikafungwa kwa muda wa siku kumi na moja katika mwezi wa Ramadhaan. Takriban vijana khamsini kutoka Waadi´iyah walikuwa wakija kunitembelea gerezani wakati wa baadhi ya usiku, wakati watu wengine mia na khamsini walikuwa wakija gerezani kuwaghasi walinzi wa jela katika usiku hizi, waliendelea hivyo kiasi kwamba walinzi walichoshwa nawakanitoa jela, himidi zote ni za Allaah.

Mfano mwingine ni kwamba maadui wa Da´wah wakati mwingine walikuwa wakija Dammaaj pamoja na silaha zao, hivyo watu wa Dammaaj walikuwa wakiwafukuza na kulazimishwa kuondoka kwa fedheha.

Mfano mwingine ni wakati wa safari zetu. Wakati nilikuwa nasema: Tunataka kusafiri.Walikuwa wakishindana -Allaah Awahifadhi– ili kuona ni nani atakayeongozana na mimi na kunilinda. Hivyo wakati mwingine tulikuwa tukitoka nje na baadhi ya safari zetu zilikuwa na magari takriban 15!

Kipindi cha muda huu, Da´wah ilikuwa inaendelea kwa namna nzuri kwa sababu – himidi zote ni za Allaah – nilikuwa na umri mkubwa. Pengine katika hatua hii nilikuwa nimefikisha umri wa miaka 62. Hivyo kulikuwa na ukimya na mashauri kutoka kwa watu ambao wanapenda Da´wah jambo ambalo lilinipelekea katika wema na kunihifadhi dhidi ya maadui, ambao hawakuwa na lolote zaidi ya matusi na uvukaji mipaka.

Wakati wa duruus zangu pia, kuandika na kutoa Da´wah, sikuwa na uwezo wa kupata muda wa kushughulika na hawa maadui. Hivyo niliwaacha waseme watakalo kwani madhambi yangu ni mengi, pengine kwa sababu ya kashfa (matusi) yao, dhambi zangu zitakuwa zikifutwa na badala yake zikianguka juu ya mabega yao.

DURUUS ZANGU NA WAALIMU WANGU:

Nilisoma katika shule mpaka nilipokamilisha mtaala wa shule. Kisha muda mrefu ukapita bila ya mimi kutafuta elimu tangu wakati ambapo kulikuwa hakuna mtu ambaye angeweza kunihamasisha au kunisaidia katika kutafuta elimu. Hivyo nikatafuta elimu katika Msikiti wa al-Haadiy lakini sikusaidiwa kwa hilo.

Baada ya muda fulani, niliiacha nchi yangu (ya Yemen) na nikaenda katika ardhi tukufu (Makkah/Madiynah) na Najd. Nilikuwa nikisikiliza wahubiri na nikipenda Khutbah zao. Hivyo nikatafuta ushauri kwa baadhi ya wahubiri juu ya vitabu gani naweza kununua? Wakanishauri niweze kupata Swahiyh al-Bukhaariy, Buluwgh al-Maraam, Riyaadh asw-Swaalihiyn, na Fath-ul-Majiyd, Sharh ya Kitaab at-Tawhiyd. Na wakanipa nakala ya vitabu vya kozi ya Tawhiyd.

Wakati huo, nilikuwa nikifanya kazi kama mlinzi wa jengo moja huko Makkah, na hivyo nilikuwa nikishikamana barabara na vitabu hivyo, na hivyo nilikuwa nikichanganyikiwa kwa sababu mambo waliyokuwa wakifanya watu katika nchi yetu yalikuwa yakienda kinyume na mambo yaliyokuwa katika vitabu hivi; khaswa Fath-ul-Majiyd.

Baada ya muda kupita, nikarudi katika nchi yangu na nikaanza kukemea kila kitu nilichokuwa naona kinaenda kinyume na yaliyokuwemo katika vitabu hivyo; kama vile kuchinja kwao badala ya kumchinjia Allaah, kuyajengea makaburi, na kuwaomba marehemu. Hivyo habari hizi zikawafikia Mashia na wakaanza kushambulia vikali yale niliyosimamia. Mmoja wao alikuwa anaweza kusema (Hadiyth): “Yeyote ambaye atabadilisha Dini yake, basi muueni.” Mwengine akatuma barua kwa watu wa familia yangu kusema: “Ikiwa hamtomzuia, basi tutamfunga jela.” Lakini baada ya hilo, wakakubaliana mimi kuingia Msikiti wa Haadiy ili kusoma pamoja nao, ili pengine waweze kuondoa fikira potofu zilizonipata kwenye moyo wangu!

Hivyo, baada ya hilo, nilikubali kusoma pamoja nao katika Msikiti wa Haadiy. Kiongozi wa elimu alikuwa ni Jaji Mutahhir Hanash. Nilisoma kitabu cha al-´Aqd-uth-Thamiyn na ath-Thalaathiyn Mas-alah, pamoja na maelezo ya Haabis. Miongoni mwa waalimu walionifundisha alikuwa ni Muhammad bin Hasan al-Mutamayyiz. Siku moja tulikuwa tukijadili mada ya kuhusu kuonekana kwa Allaah Aakhirah, hivyo akaanza maskhara na kumkejeli Ibn Khuzaymah na ma-Imaam wengine wa Ahl-us-Sunnah, lakini nilikuwa nikificha Iymaan yangu. Pamoja na kwamba, nilikuwa dhaifu mno kwa kuweka mkono wangu wa kulia juu ya mkono wangu wa kushoto wakati wa Swalah, na nilikuwa nikiswali kwa kuiachilia mikono yangu. Tulisoma nakala za al-Azhaar hadi katika sehemu ya ndoa.

Nilisoma maelezo ya Shari´ah kuhusu Mirathi kutoka katika kitabu kikubwa kilichokuwa katika kiwango cha ngazi ya juu, lakini sikustafidi kwacho. Hivyo nikaona ya kwamba vitabu vilivyotolewa havikuwa na manufaa, isipokuwa Sarufi, tangu niliposoma vitabu al-Aajruumiyyah na Qatr an-Nadaa na wao. Kisha nikamuomba Jaji, Qaasim bin Yahyaa ash-Shuwayl, kunifundisha Buluwgh al-Maraam. Hivyo tukakianza, lakini baadae harukukubaliwa, hivyo tukakiacha.

Hivyo, nilipoona vitabu vinavyotolewa kwa ajili ya masomo vilikuwa ni vitabu vyenye asili ya Kishia na Mu´tazilah, nikakubali tu kuchukua vitabu vya Sarufi. Hivyo nikasoma Qatr an-Nadaa mara kadhaa chini ya Ismaa´iyl al-Hatbah (Rahimahu Allaah), katika Msikiti ambapo nilikuwa nikiishi na nikiswali humo. Alikuwa akitupa muda mwingi na umakini. Wakati mmoja, Muhammad bin Huuriyyah alikuja Msikitini na nikamshauri kuachana na utabiri wa nyota. Hivyo akawaambia watu hapo wanitupe nje ya barnamiji za masomo, lakini wakaniombea kwa niaba yangu na akanyamaza kimya.

Baadhi ya Mashia walikuwa wakinipita wakati mimi nilipokuwa nasoma Qatr an-Nadaa na kutoa maneno ya kwamba elimu haitokuwa na athari yoyote kwangu. Lakini sikuwajali, nilikuwa nikibaki zangu kimya na kunufaika na vitabu vya Sarufi. Niliendelea hivyo hadi mapinduzi yalipoanza Yemen, wakati tuliacha nchi na makazi yetu Najraan. Huko nilisoma na Abul-Husayn Majd-ud-Diyn al-Mu´iyd na nikastafidi kutoka kwake khaswa katika lugha ya Kiarabu. Nikabaki Najraan kwa muda wa miaka miwili. Baada ya mimi kuwa na uhakika kwamba vita kati vyama vya kisiasa (Yemen) ilikuwa ni kwa ajili ya sababu za kidunia, nikaamua kwenda katika ardhi tukufu (Makkah/Madiynah) na Najd. Niliishi Najd kwa mwezi mmoja na nusu katika shule ya kuhifadhi Qur-aan, iliyokuwa ikiendeshwa na Shaykh Muhammad bin Sinaan al-Hadaa´iy. Alikuwa mkarimu sana kwangu kwa sababu aliona kuwa nastafidi kwa elimu. Akanishauri nibaki kwa muda mpaka aliponituma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu (cha Madiynah). Lakini mazingira ya Riyaadh yalinibadilikia na nikaamua kufasiri kwenda Makkah.

Nilikuwa nafanya kazi wakati nilipokuwa nikiipata, na nilikuwa natafuta elimu wakati wa usiku, nikihudhuria duruus za Shaykh Yahyaa bin ´Uthmaan al-Paakistaaniy za Tafsiyr ya Ibn Kathiyr, Swahiyh al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim.

Nilikuwa nikipitia vitabu kadhaa na huko nilikutana na Mashaykh watukufu wawili katika Wanachuoni wa kutoka Yemen:

Wa kwanza: Jaji, Yahyaa al-Ashwal. Nilisoma Subul-us-Salaam cha Swan´aaniy pamoja naye na akinifunza somo lolote nililokuwa nikimuomba.

Wa pili: Shaykh ´Abd-ur-Razzaaq ash-Shaahidhiy al-Muhwaytiy. Alikuwa akinifunza pia kitu chochote nilichokuwa ninamuomba kwacho.

Kisha taasisi ya elimu Makkah ikafunguliwa na nikafanya mtihani wa kujiunga pamoja na kundi la wanafunzi, na mimi nikapasi, himidi zote ni za Allaah.

Aliyekuwa akijulikana sana katika waalimu wetu alikuwa ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz as-Subayyal. Mimi, pamoja na kundi la wanafunzi kutoka Chuo hicho, tulikuwa tunasoma pia na Shaykh ´Abdullaah bin Muhammad bin Humayd (Rahimahu Allaah), kitabu at-Tuhfah as-Saniyyah baada ya ´Ishaa katika Haram. Alikuwa (Rahimahu Allaah) akileta nukta nyingi zenye faida kutoka kwa Ibn ´Aqiyl na maelezo mengine ya Wanachuoni. Masomo yalikuwa katika kiwango cha juu kwa wenzangu, wakaanza kukimbia mpaka hapo aliposimamisha darasa.

Nilisoma pia pamoja na kundi la wanafunzi na Shaykh Muhammad as-Subayyal (Rahimahu Allaah), somo la Shari´ah kuhusu Mirathi.

Baada ya kukaa katika Chuo kwa muda fulani, nilitoka kwenda katika familia yangu Najraan. Kisha nikawaleta kuishi pamoja nami Makkah. Tukaishi huko pamoja kwa muda mrefu wa masomo yangu katika Chuo na katika Haram yenyewe, ambayo ilidumu kwa miaka sita.

Baraka ya kusoma katika Misikiti inajulikana. Usiulize kuhusu mazingira ya kirafiki na utulivu tuliyokuwa tukihisi katika Misikiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kweli wakati aliposema:

“Kundi la watu halikusanyiki katika moja ya Nyumba (Msikiti wa) Allaah, wakisoma Kitabu cha Allaah na wakakizingatia baina yao, isipokuwa huteremka juu yao utulivu, Malaika huwazunguka, Rahmah huwaenea, na Allaah Huwakumbuka kwa wale walioko pamoja naye.”

Hivyo nilikuwa natumia siku kusoma katika Chuo hicho, na masomo yote yalinisaidia Iymaan yangu na Dini. Kisha kutoka baada ya ´Aswr mpaka baada ya Swalah ya ´Ishaa, nilikuwa nikienda Haram na kunywa maji ya Zamzam, ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kuhusu maji hayo:

“Kwa hakika, ni kinywaji kinachoshibisha na ni tiba ya maradhi.”

Na tulikuwa tunasikiliza wahubiri wanaokuja Makkah kutoka katika nchi mbalimbali kufanya Hajj au ´Umrah.

Miongoni mwa waalimu tuliojifunza kutoka Haram kati ya Maghrib na ´Ishaa ni Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Raashid an-Najdiy, mwandishi wa kitabu Taysiyr-ul-Wahyayn fil-Iqtiswaar ´alal-Qur-aani wasw-Swahiyhayn, ambacho kina makosa na hatukubaliani na yeye kwacho. Alikuwa akisema (Rahimahu Allaah): “Ahaadiyth ambazo ni Swahiyh ambazo hazipatikani katika mkusanyiko wa Swahiyhayn (al-Bukhaariy na Muslim) zinaweza kuhesabika na vidole vya mtu mmoja.” Hii kauli yake haikutoka akilini mwangu tangu nilipokitilia umuhimu. Hii ilikuwa njia yote mpaka nilipoamua kuandika as-Swahiyh-ul-Musnad mimmaa laysa fiys-Swahiyhayn baada ya kuwa na uhakika kuhusu ubatili wa kauli yake (Rahimahu Allaah).

Miongoni mwa waalimu wangu wa Msikiti Mkuu (Haram) wa Makkah ambaye nilistafidi kutoka kwake ni Shaykh Muhammad bin ´Abdillaah as-Sumaaliy, kwa maana nilihudhuria masomo yake kwa miezi saba au zaidi. Na alikuwa ni ishara katika istilaha ya elimu ya wapokezi wanaotumiwa na Mashaykh wawili (al-Bukhaariy na Muslim). Nilistafidi kiasi kikubwa kutoka kwake katika Sayansi ya Hadiyth. Himidi zote ni za Mola Wangu, tangu nilipoanza kutafuta elimu, sipendi kitu chochote isipokuwa elimu ya Kitabu na Sunnah.

Baada ya kumaliza ngazi za kati na sekondari ya taasisi ya elimu Makkah, na baada ya kumaliza masomo yangu yote ya Dini, nikaenda Madiynah katika Chuo Kikuu cha Kiislamu huko. Wengi wetu walihamishwa katika Kitivo cha Da´wah na Usuul-ud-Diyn.Katika wale wanaojulikana sana waliotufunza ni: Shaykh as-Sa´iyd Muhammad al-Hakiym na Shaykh Mahmuud ´Abdul-Wahhaab Faa´iyd, wote ni kutoka Misri. Wakati wa likizo unapokuja, nakhofia wakati usipotee bure hivyo najiunga na Kitivo cha Shari´ah, kutokana na sababu mbili, ya kwanza ambayo ilikuwa ni kupata elimu:

Hii ilikuwa wakati tangu baadhi ya madarasa huko yalikuwa ni yakupasi wakati mengine yalikuwa yakikutana (na nilivyosema hapo kabla). Hivyo ilikuwa ni kama marudio ya yale tuliyosoma katika Kitivo cha Da´wah. Nilikamilisha Kitivo cha kazi zote mbili, himidi zote ni za Allaah, na nilipewa digrii mbili. Hata hivyo, sifa zote ni za Allaah, sivipi umuhimu vyeti; kile nilichokuwa najali mimi ni elimu.

Katika mwaka huo huo nilipomaliza kozi katika vyuo viwili, nilisonga mbele, na masomo ya juu ya shahada ya pili ambayo ilikuwa imefunguliwa katika Chuo Kikuu cha Kiislamu. Basi, nikawa nimeenda kwa ajili ya mtihani wa mahojiano na nikapita, himidi zote ni za Allaah. Masomo ya kiwango cha juu ilikuwa ni Sayansi ya Hadiyth. Himidi zote ni za Allaah, nikasoma somo ambalo nilikuwa nalipenda zaidi. Watu maarufu zaidi katika wale waliokuwa wakitufundisha ilikuwa ni Shaykh Muhammad al-Amiyn al-Misriy (Rahimahu Allaah), Shaykh as-Sa´iyd Muhammad al-Hakiym al-Misriy, na wakati wa sehemu ya mwisho ya masomo yangu, Shaykh Hammaad bin Muhammad al-Answaariy. Katika baadhi ya usiku, nilikuwa napenda kuhudhuria duruus za Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz kwenye Msikiti wa Mtume (Madiynah) juu ya somo la Swahiyh Muslim. Nilikuwa napenda pia kuhudhuria mkusanyiko wa vikao vya Shaykh Al-Albaaniy, ambavyo vilikuwa ni maalum kwa watafutaji wa elimu tu, ili kujifunza kutoka kwake.

Pindi nilipokuwa Makkah, nilikuwa nafundisha baadhi ya watafutaji wa elimu kutoka katika vitabu Qatr-un-Nadaa na at-Tuhfah as-Saniyyah. Na wakati nilipokuwa Madiynah, nilikuwa nafundisha baadhi ya ndugu zangu kitabu at-Tuhfah as-Saniyyah kwenye Msikiti wa Mtume. Kisha nikawaahidi ndugu zangu Waislamu kwamba nitashikilia duruus katika Jaamiy´ (Sunan) ya at-Tirmidhiy, Qatr-un-Nadaa na al-Baa´ith-ul-Hathiyth kwa ajili yao katika nyumba yangu baada ya ´Aswr.

Hivyo, wimbi kubwa la Da´wah likaenea Madiynah, ambalo lilijaza dunia kwa muda wa miaka sita. Ilikuwa ni baadhi ya watu wa haki ndio walichukua jukumu la kugharamia, wakati Muqbil bin Haadiy na ndugu zake Waislamu ndio walichukua jukumu la kuwafundisha ndugu zao wengine. Ama kusafiri kwa madhumuni ya kulingania kwa Allaah katika mikoa yote ya Mamlaka (Saudi), hili lilikuwa wakisaidizana ndugu wote watafutaji wa elimu ili mtu aweze kupata elimu na kunufaisha wengine, na mtu wa kawaida ili naye aweze kujifunza. Hii ilikuwa kama kwamba wengi wa watu wa kawaida wananufaika kwalo na kuzidi kuipenda Da´wah (ya Salafi).

Mmoja katika ndugu zetu Waislamu miongoni mwa watafutaji wa elimu alikuwa ni Imaam wa Msikiti wa Riyaadh. Siku moja baadhi ya watu watafutaji wa elimu walimkemea kwa kutumia kwake Sutrah. Basi akasema: “Hatuna uwezo mbele yenu, lakini naapa, si mwengine zaidi isipokuwa mtu wa kawaida ndiye ambaye anaweza kukufundisha Ahaadiyth kuhusiana na Sutrah.” Basi, akaita ndugu katika watu wa ujumla aliyekuwa akipenda Da´wah na alikuwa amehifadhi Ahaadiyth kuhusiana na Sutrah kutoka katika al-Lu´lu´ wal-Marjaan fiymataffaqa ´alayhi ash-Shaykhaan. Basi akajitokeza na akasimulia Ahaadiyth hizi, baada ya hapo wapinzani wakaona aibu na kukaa kimya.

Baada ya hili, wafuasi wanaofuata kipofu na Wanachuoni wa uovu wakaanza kujipanga, na sababu hii wakachochea wafuasi vipofu, ambaye alikuwa anachukuliwa kuwa ni Mwanachuoni katika macho ya watu, kwa sababu ilikuwa wakati wowote wanapopata mwanafunzi kijana mtafutaji wa elimu miongoni mwa wanafunzi wetu na anaweza kutumia Hadiyth kama dalili, mwanafunzi huyu anawaambia: Mpokezi wa Hadiyth? Na hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa la kawaida. Kisha alikuwa akiwaambia: Daraja ya Hadiyth? Hili lilikuwa pia ni jambo lisilokuwa la kawaida. Basi walikuwa wakiwaaibisha mbele ya watu. Wakati mwingine mwanafunzi anawaambia: Hii ni Hadiyth dhaifu. Hali ni hivi na hivi na mlolongo wake wa upokezi na vivyo hivyo kuihukumu kuwa ni dhaifu. Hivyo juu ya kusikia hivi, ni kama kwamba dunia isingekuwa na wapinzani wengi wafuataji kipofu. Na wakawa wanaenda kueneza uongo kwamba wanafunzi hawa ni Khawaarij, wakati kwa kweli ndugu hawakuwa katika Khawaarij ambao wanahalalisha kumwaga damu ya Waislamu na ambao wanawachukulia Waislamu kuwa ni makafiri kwa sababu ya hesabu ya madhambi.

Hata hivyo, huko kulikuwa kunaweza kutokea baadhi ya makosa kwa upande wa baadhi ya ndugu wapya, na hii ilikuwa ni kwa sababu wanaoanza huzidiwa kila mara na bidii nyingi. Katika wakati huo, nilikuwa naandaa mtihani wangu wa shahada ya pili, ghafla usiku mmoja, kabla ya mimi kujua kitachotokea, wakanitia mbaroni mimi na wengine waliokamatwa karibu watu mia moja na khamsini. Baadhi ya watu walikuwa wako tayari kutoroka, lakini dunia ikatetemeka kati ya wale ambao wanapinga na wale wanaokubaliana na kukamatwa kwetu. Tukabaki gerezani kwa muda wa mwezi mzima au mwezi mmoja na nusu. Baada ya hapo tukaachwa huru, himidi zote ni za Allaah.

Muda mfupi baada ya tukio hili, maandiko ya kundi la Juhaymaan yakatolewa na kundi katika sisi likakamatwa tena.[2] Wakati wa kuhojiwa, wakaniuliza: Je, ni wewe ndiye uliandika hivi? Nini, Juhaymaan hawezi kuandika? Hivyo nikakanusha hili, na Allaah Anajua kwamba sikuandika hivi na wala mimi sikushiriki sehemu yoyote katika hili. Lakini baada ya kukaa jela kwa miezi mitatu, amri ilitolewa ya kuwarejesha wageni makwao.

Nilipofika Yemen, nikarudi kijijini kwetu na nikakaa huko kwa muda nikifundisha watoto Qur-aan. Kabla ya kujua hilo, ilionekana kama dunia nzima ilikuwa nje kwa vita dhidi yangu. Ilikuwa ni kama vile nimetoka nje kwa ajili ya kuharibu nchi, Dini na utawala. Wakati huo, sikuwa najua kiongozi yeyote au mkuu wa kikabila. Hivyo nilikuwa nikisema: “Allaah Ananitosheleza na ni Mlinzi wangu bora.” Wakati mambo yalipokuwa magumu, nilikuwa naenda San´aa au Haashid au Dhimmaar, na pia Tayiz, Ibb na Hudaydah kutoa Da´wah na kutembelea ndugu Waislamu.

Baada ya siku kadhaa, baadhi ya watu wema walinitumia Maktabah yangu kutoka Madiynah. Wakatuma vitabu Sa´adah ambapo Sunnah ilikuwa imepamba moto. Baadhi ya wenzetu wakaenda kuomba vitabu vyangu, wakaambiwa: Njoo baada ya Dhuhr, In Shaa Allaah. Lakini aliyetoa ahadi ya kutoa vitabu hakurudi baada ya Dhuhr. Badala yake, baadhi ya waliohamasishwa na Mashia na walinzi wa usalama wakazuia hivyo vitabu kwa sababu vilikuwa ni vitabu walivyoita vya ‘Wahaabiy’!

Usiulize kuhusu ada ya fedha, shida na dhuluma niliyokuwa nafanyiwa kama matokeo ya kujaribu kupata vitabu vyangu! Ndugu wengi wakaazi wa nchi yangu walifanya juhudi kubwa kufuatilia hilo, akiweno Shaykh ´Abdullaah bin Husayn al-Ahmar, Shaykh Hazaa´iy Dab´iyaan, msimamizi wa Kituo cha mwaongozo na ushauri, kama vile Jaji Yahyaa al-Fasayyal (Rahimahu Allaah), na ndugu ´Aa´iyd bin ´Aliy Mismaar. Baada ya shida ya muda mrefu, watu wa Sa´adah walituma telegrafu kwa Rais ´Aliy bin ´Abdillaah bin Swaalih, hivyo akampa kesi hakimu, ´Aliyas-Samaan. Jaji akanitumia barua na kuniahidi kwamba atanirudishia Maktabah yangu. Na akasema: Watu wa Sa´adah ni wakali sana. Wanawaita Wanachuoni wa Sa´adah kuwa ni makafiri. Hivyo nikaenda San´aa kuchukua vitabu vyangu. Allaah Aliamuru vitabu vyangu kufika huko wakati hakimu ´Aliy Samaan alikuwa nje ya nchi juu ya kazi fulani. Hivyo wakati baadhi ya ndugu walienda kuviomba, mkuu wa Wizara ya Waqf akawaambia: Vitabu hivi vinahitajia kuchunguzwa. Hivyo, baadhi ya ndugu zetu Waislamu katika Kituo cha Ushauri na uongofu wakahamasishwa na kwenda kuomba vitabu. Wakasema: Vitabu hivi viko chini ya mamlaka yetu. Lazima tuvichunguze. Tutavipeleka mpaka al-Waadi´iy na chochote kitachokiuka Dini, tutavichukua. Hivyo kwa kufanya hivyo, wakaja kugundua ya kwamba vitabu vilikuwa kweli ni vya kidini na wakanipa bila ya kuvikagua, Allaah Awalipe.

Nikaleta vitabu kwenye mji wangu, himidi zote ni za Allaah. Na mtu wangu wa karibu, Allaah Amhifadhi, akajenga Maktabah ndogo na Msikiti mdogo. Na wakasema: Tutaswali Ijumaa hapa ili kuepuka uzito na matatizo. Wakati mwingine tulikuwa tunaswali hapo na (Jamaa´ah ya) watu wa sita waliohudhuria.

Wakati mmoja gavana Haadiy al-Hashiyshi alinihitajia, hivyo nikaenda kwa Shaykh Qaa´iyd Majliy (Rahimahu Allaah), ambaye alimpigia simu na kumwambia: Unataka nini kutoka kwa al-Waadi´iy? Akasema: Hakuna, isipokuwa tu nataka kumjua. Hivyo akasema: Tutamtazama na Chuo chake.

Katika hali nyingine, baadhi ya viongozi wengine waliniulizia na hivyo Husayn bin Qaa´iyd Majliy akaenda pamoja na mimi kumuona mtu huyo. Huyo (Majliy) akaanza kuzungumzia dhidi ya Mashia na akamuelewesha ya kwamba sisi tunalingania katika Qur-aan na Sunnah na kwamba Mashia wanatuchukia kwa sababu wanakhofia haki itatoka kuwahusu wao, hivyo kiongozi huyu akasema: Kwa hakika, Mashia wamechafua historia ya Yemen, hivyo maadamu Da´wah yenu ni kama mnavyosema, basi mlinganie na sisi tuko pamoja nanyi.

Baada ya tukio hili, nikawa natumia muda katika Maktabah yangu. Baada tu ya siku chache kupita wakati baadhi ya ndugu wa Misri walipokuja na tukaanza duruus ya baadhi ya vitabu vya Hadiyth na lugha ya Kiarabu. Baada ya hili, wanafunzi wakaendelea kuja kutoka Misri, Kuwait, Ardhi Takatifu (Makkah na Madiynah), Najd, ´Aden, Hadhramaut, Algeria, Libya, Somalia, Ubelgiji, na nchi nyingine za Waislamu na zisizokuwa za Waislamu.

Idadi ya wanafunzi imefikia sasa kati ya mia sita mpaka mia saba ya wanafunzi, miongoni mwao ni familia mia na sabini.[3] Na Allaah ndiye Ambaye Alikuwa Akiwapa riziki. Na yote haya haikuwa kwa sababu ya nguvu zetu au utukufu wetu, wala kutokana na kiasi cha elimu yetu tuliyokuwa nayo au ujasiri wetu au ufasaha wa Khutbah. Badala yake, hili ni jambo ambalo Allaah Alipenda liwe. Hivyo alikuwa ni Yeye peke Yake (Sifa zote ni za Allaah) Ambaye Alitupatia baraka hii.

[Mwisho wa Tafsiri ya maelezo ya wasifu wa Shaykh Muqbil kutoka kwake mwenyewe]

KIFO CHAKE:

Shaykh Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy alifariki tarehe 2 ya Jumaadal-Uwlaa, 1422H (07/21/2001) kutokana na ugonjwa wa ini ambalo lilimletea mateso kwa muda mrefu, na ambalo lilimfanya akasafiri kwenda Marekani, Ujerumani na Saudi Arabia wakati wa sehemu ya mwisho ya maisha yake kwa ajili ya kutafuta matibabu. Alikuwa takriban na umri wa miaka sabini alipokufa Jeddah. Swalah yake ya janaza iliswaliwa Makkah na alizikwa katika makaburi ya al-´Adl karibu na kaburi la Shaykh Ibn Baaz na Ibn al-´Uthaymiyn (Rahimahumu Allaah).

SIFA ZA WANACHUONI KWAKE:

Shaykh Muhammad bin Swaalih al-´Uthaymiyn kasema: “Mwambie ya kwamba mimi namchukulia yeye kuwa ni Mujaddid (Mwenye kuhuisha Diyn).”

Shaykh Al-Albaaniy kasema:

“Sisi, bila shaka tunamhimidi Allaah (´Azza wa Jalla) Kujaalia katika Da´wah hii njema, iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa Manhaj ya Salafus-Swaalih Ma-Du´aat katika miji mbali mbali ya Kiislamu ambao wanasimama kwa Fardh al-Kifaayah, faradhi ambayo wamekuwa wachache wenye kusimama kwayo katika ulimwengu wa Kiislamu wa leo.

Kwa hivyo, hawa Mashaykh wawili watukufu, Madu´aat wawili wanaolingania katika Qur-aan na Sunnah na juu ya yale waliyosimamia Salafus-Swaalih, na kupigana vita na wale ambao wanakwenda kinyume na Manhaj hii sahihi, ni kama mnavyojua nyote (kuhusiana na watu hawa wanaowaponda) ni mmoja ya watu wawili, ima ni:

1) Jaahil (Mjinga), au
2) Swaahibu Hawaa (mtu wa matamanio)

Mjinga kama nilivyotangulia kusema, anaweza kuongozwa kwa urahisi, kwa kuwa mtu aina hii hudhani ana elimu fulani – na wakati itambainikia elimu sahihi ataongoka…
Ama kwa mtu wa matamanio, hatuna juu yetu njia nyingine isipokuwa ikiwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atamuongoza.

Hawa watu wanaowasema vibaya (wanaoponda) hawa Mashaykh wawili, ni kama tulivyosema, ima ni mjinga afunzwe; na ima ni mtu wa matamanio, Aombwe Allaah Atukinge na shari yake na tunamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ima Amuongoze au amvunje mgongo wake.”
[Mfululizo Silsilah al-Hudaa wan-Nuur: 1/851].

Shaykh Yahyaa al-Hajuwriy kapokea ya kwamba Shaykh Rabiy´al-Madkhaliy kasema juu yake: “Ni Mujaddid katika nchi ya Yemen na kwamba kasema: Hakuwezi kupatikana kutoka katika zama za ´Abdur-Razaaq as-Swan´aaniy katika zama zetu hizi mtu ambaye anasimamisha Da´wah imara na kuihuisha kama mfano wa al-Waadi´iy.”[4

Chanzo: Tarjamah Abiy ´Abdir-Rahmaan (uk. 16-29, pamoja na Mukhtaswar kidogo) [Toloe la pili; 1999]

—————————–
[1] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Katika aliyoandika kuhusiana na historia ya baba yake, Umm ´Abdillaah al-Waadi´iyyah kasema, Baba yake alikufa wakati alipokuwa kijana mdogo na hakuwa anamjua. Hivyo alikua kama yatima na chini ya uangalizi wa mama yake kwa kipindi cha muda. Alikuwa (mama) akimuomba (baba) afanye kazi ili apate pesa, na akimuamrisha kuangalia hali ya jamii yake ili aweze kuwa kama wao. Lakini alikuwa akiyapuuza haya na kumwambia: Nitaenda kusoma. Hivyo (mama) akimwambia: Allaah Akuongoze. Akimuombea aongoke, kwa wanawake kadhaa ambao walikuwa wakati ule ndio walivyonambia. Pengine Du´aa yake ilikutana na wakati ambapo Du´aa hupokelewa tangu alipokuwa mmoja aliyeongozwa, na akaongoza wengine. [Nubdhah Mukhtaswarah: uk. 18].

[2] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Hili linamhusu Juhaymaan bin Muhammad al-´Utaybiy, mpotofu kutoka Saudi Arabia ambaye aliuteka nyara Msikiti Mkuu wa Makkah na mamia ya wafuasi katika mwaka wa 1979, na akaushikilia kwa siku kadhaa, baada ambapo Wanachuoni waheshimiwa wakaruhusu nguvu zitumike katika eneo tukufu la Ka´bah ili kurejesha Msikiti huo. Kundi la Walinzi wa Saudi la Taifa likawazingira takriban mnamo wiki mbili, baadaye baada ya damu nyingi kumwagika, na wengine kujeruhiwa katika mapambano ya waasi na jeshi la Saudi. Waasi waliobaki na kushikwa, walihukumiwa kuuawa. Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kamtaja huyu Juhaymaan katika kitabu chake as-Swahiyhah (5/872) akisema: Na mfano wa wafuasi wa Juhaymaan wa Saudi, ambaye alisababisha fitinakwenye Msikiti Mkuu wa Makkah mwanzoni wa mwaka 1400 (Hijriy). Alidai ya kwamba Mahdiy anayesubiriwa yuko pamoja naye na alitaka kutoka kwa wale waliopo Msikitini kumpa bay´ah (utiifu). Baadhi ya watu wenye akili fupi, wakaghafilika na watu waovu wakamfuata. Kisha Allaah Akamaliza fitinah hii baada ya kumwagika kiasi kikubwa cha damu ya Waislamu.

[3] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Inatakikana ijulikane ya kwamba maneno haya hapa yamekuja tangu toleo la pili la wasifu wake, ambayo ilichapishwa mwaka wa 1.999. Tangu wakati huo idadi hii iliendelea kuongeza, kama ilivyo wakati wa sasa katika shule ya Shaykh, ambayo kwa sasa inafundisha na kusimamiwa na Shaykh Yahyaa al-Hajuuriyna ina wanafunzi karibu 1.000 na familia 500, himidi zote ni za Allaah.

[4] Maelezo ya mkusanyaji wa historia hii: Maneno haya ni kutoka katika kitabu Nubdhah Mukhtaswarah cha bint wa Shaykh Muqbil, Umm ´Abdillaah (uk. 46).


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 8th, December 2013