Wasifu Wa Shaykh Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn

JINA LAKE: Abu 'Abdillaah Muhammad bin Swaalih bin Sulaymaan bin 'Abdir-Rahmaan bin 'Uthmaan al-Wuhaybiy at-Tamiymiy. Babu wa baba yake wa zamani 'Uthmaan alikuwa anaitwa 'Uthaymiyn na hivyo ndio akawa akijulikana kwa jina hilo. KUZALIWA KWAKE: Alizaliwa katika mji wa 'Unayzah katika wilaya ya Qasiym Saudi Arabia tarehe 27, Ramadhaan katika mwaka wa 1347 B.H. WAALIMU WAKE: 1) Shaykh al-' Allaamah al-Mufassir 'Abdur-Rahmaan bin Naaswir as- Sa'diy. Alisoma kwake chini ya kipindi cha miaka 16. 2) Shaykh al-´Allaamah ' Abdul-´Aziyz bin Baaz, ambaye alikuwa Muftiy wa Saudi Mufti wa kabla (ya ambaye yuko hivi sasa). Alisoma kwake Swahiyh al-Bukhaariy na vitabu vya Fiqh. 3) Shaykh al-Mufassir Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy. Alisoma kwake al-Ma'had al-'Ilmiy Riyaadh. 4) Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Aziyz al-Mutawwa´. Alikuwa hakimu hapo kabla wa 'Unayzah. Alisoma kwake 'Aqiydah, Fiqh na lugha. WANAFUNZI WAKE: Shaykh alisomesha kwa muda wa miaka 45, mpaka alipofariki, na alikuwa na wanafunzi wengi kiasi kwamba ni vigumu kuwahesabu wote, lakini miongoni mwao ni: 1) Shaykh Hamad al-'Uthmaan: ni mmoja katika wanachuoni wa Kuwait na mwalimu katika chuo kikuu cha Kuwait. 2) Shaykh Sulaymaan Abaal-Khayl: ni mudiri wa sasa wa chuo kikuu cha Imaam Muhammad bin Su'uud. 3) Shaykh 'Abdus-Salaam bin Barjas: alikuwa ni mmoja katika wanachuoni wa Riyaadh ambaye anajulikana kwa vitabu vyake vizuri alivyoandika. 4) Shaykh 'Issaam as-Sinaaniy: mmoja katika wanachuoni wa Qasiym. 5) Shaykh 'Abdullaah al-Musallam: mmoja katika wanachuoni wa Qasiym. VITABU VYAKE: Shaykh mpaka katika mwaka wa 1422 B.H. ana vitabu 115 vinavyochapishwa alivyoandika na ambavyo wanafunzi wake wameandika kutoka kwenye mikanda yake. MIONGONI MWA VITABU MAARUFU NI: 1) Sharh-ul- Mumtiy´ ambacho ni Sharh ya Zaad-ul-Mustaqniy', kimechapishwa mijaladi 16. 2) Sharh Riyaadh-us-Swaalihiyn ambacho ni mijaladi 7 kwa urefu. 3) Mkusanyiko wa vitabu vya Shaykh vifupi na fataawa ambazo ni kiasi na mijaladi 30. SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE: 1) Shaykh al-Muhaddith ' Abdul-Muhsin al-'Abbaad alisema: "Nitakuelezeni ndugu zangu jioni hii ya leo kuhusu Shaykh muheshimiwa wa Saudi Arabia, na mmoja katika wanachuoni wakubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Aliweka juhudi nyingi kwenye elimu, katika kuisambaza na kuwapa faida wanafunzi. Na si mwingine ni Shaykh al-'Allaamah Muhammad bin Swaalih al-'Uthaymiyn... " (Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn minal-´Ulamaa ar-Rabbaaniyiyn, ambacho ni sehemu ya mkusanyiko wa vitabu vya Shaykh ´Abdul-Muhsiyn (6/473) 2) Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy akasema: "Je, unaweza kupata katika dunia hii kama vile Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn 'Uthaymiyn..." (Ahl-ul- Hadiyth hum at-Twaa'ifat-ul-Mansuurah wal-Firqat-un-Naajiyah 90-91) KIFO CHAKE: Shaykh alikufa tarehe 15 mwezi wa Shawwaal mwaka wa 1421 B.H., sawa na tarehe 10 Januari 2001. Serikali ya Saudi Arabia ililazimika kuleta askari 1,500 ili kuweka nidhamu juu ya watu zaidi ya 500 000 waliomswalia Shaykh Swalah ya Janaza. Mbele alikuwa amesimama waziri wa mambo ya ndani wa Saudi Arabia Prince Nayif bin 'Abdil-Aziyz na waziri wa mambo ya Dini Shaykh Swaalih Aal ash-Shaykh pamoja na wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia.

JINA LAKE:
Abu ‘Abdillaah Muhammad bin Swaalih bin Sulaymaan bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Uthmaan al-Wuhaybiy at-Tamiymiy. Babu wa baba yake wa zamani ‘Uthmaan alikuwa anaitwa ‘Uthaymiyn na hivyo ndio akawa akijulikana kwa jina hilo.

KUZALIWA KWAKE:
Alizaliwa katika mji wa ‘Unayzah katika wilaya ya Qasiym Saudi Arabia tarehe 27, Ramadhaan katika mwaka wa 1347 B.H.

WAALIMU WAKE:
1) Shaykh al-‘ Allaamah al-Mufassir ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir as- Sa’diy. Alisoma kwake chini ya kipindi cha miaka 16.
2) Shaykh al-´Allaamah ‘ Abdul-´Aziyz bin Baaz, ambaye alikuwa Muftiy wa Saudi Mufti wa kabla (ya ambaye yuko hivi sasa). Alisoma kwake Swahiyh al-Bukhaariy na vitabu vya Fiqh.
3) Shaykh al-Mufassir Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy. Alisoma kwake al-Ma’had al-‘Ilmiy Riyaadh.
4) Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Aziyz al-Mutawwa´. Alikuwa hakimu hapo kabla wa ‘Unayzah. Alisoma kwake ‘Aqiydah, Fiqh na lugha.

WANAFUNZI WAKE:
Shaykh alisomesha kwa muda wa miaka 45, mpaka alipofariki, na alikuwa na wanafunzi wengi kiasi kwamba ni vigumu kuwahesabu wote, lakini miongoni mwao ni:
1) Shaykh Hamad al-‘Uthmaan: ni mmoja katika wanachuoni wa Kuwait na mwalimu katika chuo kikuu cha Kuwait.
2) Shaykh Sulaymaan Abaal-Khayl: ni mudiri wa sasa wa chuo kikuu cha Imaam Muhammad bin Su’uud.
3) Shaykh ‘Abdus-Salaam bin Barjas: alikuwa ni mmoja katika wanachuoni wa Riyaadh ambaye anajulikana kwa vitabu vyake vizuri alivyoandika.
4) Shaykh ‘Issaam as-Sinaaniy: mmoja katika wanachuoni wa Qasiym.
5) Shaykh ‘Abdullaah al-Musallam: mmoja katika wanachuoni wa Qasiym.

VITABU VYAKE:
Shaykh mpaka katika mwaka wa 1422 B.H. ana vitabu 115 vinavyochapishwa alivyoandika na ambavyo wanafunzi wake wameandika kutoka kwenye mikanda yake.

MIONGONI MWA VITABU MAARUFU NI:
1) Sharh-ul- Mumtiy´ ambacho ni Sharh ya Zaad-ul-Mustaqniy’, kimechapishwa mijaladi 16.
2) Sharh Riyaadh-us-Swaalihiyn ambacho ni mijaladi 7 kwa urefu.
3) Mkusanyiko wa vitabu vya Shaykh vifupi na fataawa ambazo ni kiasi na mijaladi 30.

SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE:
1) Shaykh al-Muhaddith ‘ Abdul-Muhsin al-‘Abbaad alisema: “Nitakuelezeni ndugu zangu jioni hii ya leo kuhusu Shaykh muheshimiwa wa Saudi Arabia, na mmoja katika wanachuoni wakubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Aliweka juhudi nyingi kwenye elimu, katika kuisambaza na kuwapa faida wanafunzi. Na si mwingine ni Shaykh al-‘Allaamah Muhammad bin Swaalih al-‘Uthaymiyn… ” (Shaykh Muhammad bin ´Uthaymiyn minal-´Ulamaa ar-Rabbaaniyiyn, ambacho ni sehemu ya mkusanyiko wa vitabu vya Shaykh ´Abdul-Muhsiyn (6/473)

2) Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy akasema: “Je, unaweza kupata katika dunia hii kama vile Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn…” (Ahl-ul- Hadiyth hum at-Twaa’ifat-ul-Mansuurah wal-Firqat-un-Naajiyah 90-91)

KIFO CHAKE:
Shaykh alikufa tarehe 15 mwezi wa Shawwaal mwaka wa 1421 B.H., sawa na tarehe 10 Januari 2001.

Serikali ya Saudi Arabia ililazimika kuleta askari 1,500 ili kuweka nidhamu juu ya watu zaidi ya 500 000 waliomswalia Shaykh Swalah ya Janaza. Mbele alikuwa amesimama waziri wa mambo ya ndani wa Saudi Arabia Prince Nayif bin ‘Abdil-Aziyz na waziri wa mambo ya Dini Shaykh Swaalih Aal ash-Shaykh pamoja na wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia.


  • Author: Muhtasari wa kitabu al-Jaamiy' li Hayaat al-'Allaamah Muhammad bin Swaalih al-'Uthaymiyn cha Waliyd al-Hussayn, pamoja na baadhi nyongeza.
  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 9th, December 2013