Wasifu Wa Shaykh ‘Abdur-Razzaaq ‘Afiyfiy

JINA NA KUZALIWA KWAKE Ni Shaykh na mwanachuoni mkubwa 'Abdur-Razzaaq bin 'Afiyfiy bin ´Atiyyah an-Nuubiy katika kijiji kinachopatikana eneo la al-Muunifiyyah Misri katika mwaka wa 1325 B.H. MWANZO WA MASOMO YAKE Shaykh alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha al-Azhar na akachukua Shahaadah yake katika mwaka wa 1351 B.H. Baada ya hapo akatakhasusi katika Fiqh na misingi yake na kuendelea masomo yake mpaka akawa miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Misri. KUFUNZA KWAKE NA KAZI ZAKE Alianza kufundisha katika shule ambazo zilikuwa ni za Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri, baada ya hapo akahama kwenda Saudi Arabia katika 1367 B.H. na kufundisha katika kituo cha Kiislamu Twaa'if, Riyaadh na 'Unayzah. Baadae wakati kitivo cha Shari'ah kilipofunguliwa Riyaadh, hivyo akaanza kufundisha pale na baadae wakati Chuo Kikuu cha mahakama kilipofunguliwa mwaka wa 1385 B.H. Riyaadh, akawa mudiri wake, na alikuwa miongoni mwa wenye majukumu ya kuandika selebasi yake. Katika mwaka wa 1391 B.H. akawa mwanachama wa baraza kuu la fatwa Saudi Arabia na makamu wa raisi mpaka alipofariki. Alikuwa pia ni mwanachama wa baraza la wanachuoni watu wazima (wazee) nchini Saudi Arabia. WANAFUNZI WAKE Wengi katika wanachuoni wakubwa wa leo walikuwa ni wanafunzi wa Shaykh. Miongoni mwa hawa ni: 1) Shaykh Swaalih al-Luhaydaan, ambaye ni mmoja katika wanachuoni wetu wakubwa hivi leo. Alikuwa ni mkuu wa zamani wa baraza la mahakama nchini Saudi Arabia. 2) Shaykh Swaalih al-Fawzaan, ambaye anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wetu wakubwa hivi leo na ni mwanachama wa baraza la kudumu la fatwa nchini Saudi Arabia. 3) Shaykh Swaalih al-Atram, ambaye alikuwa ni mmoja katika wanachuoni aliyekuwa akiishi nchini Saudi Arabia. 4) Shaykh 'Abdullaah bin Qu'uud, ambaye alikuwa ni mwanachama wa baraza la kudumu la fatwa nchini Saudi Arabia. TABIA YAKE Shaykh alikuwa na sifa ambazo mwanachuoni wa kweli lazima awe nazo. Alikuwa mara nyingi akiwa na tabasamu usoni mwake na alikuwa anajulikana kwa upendo wake wa wema na kutaka kuwasaidia watu wengine. Alikuwa ni mwenye Zuhd katika maisha haya na wala alikuwa hajali uzuri wake pamoja na kuwa alikuwa na uwezo wa kufikia hilo. Alikuwa hapendi kupandishwa na kujulikana licha ya elimu yake kubwa (aliokuwa nayo). Alikuwa kamwe hazungumzii wengine vibaya na alikuwa anajulikana kwa ukarimu wake kwa wageni wake. Alikuwa anachunga wakati wake kwa kusoma Qur-aan na kujishughulisha na elimu yenye manufaa. Alikuwa vilevile akijali sana juu ya yale yanayotokea na ulimwengu wa Waislamu. UGONJWA WAKE NA KIFO CHAKE Shaykh alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na mafigo, moyo wa maini, na mwisho wake akafa tarehe 25 Rabiy´-ul-Awwal mwaka wa 1415 B.H. Wasifu huu ni mukhtasari wa yale ambayo Dr. Faalih as-Saghiyr aliyoandika katika kitabu al-Ḩadaa'iq al-Bahiyyah fiy Siyar ba'dh-ul-'Ulamaa al-Mu'asiriyn (uk. 105-128) na baadhi ya nyongeza.

JINA NA KUZALIWA KWAKE
Ni Shaykh na mwanachuoni mkubwa ‘Abdur-Razzaaq bin ‘Afiyfiy bin ´Atiyyah an-Nuubiy katika kijiji kinachopatikana eneo la al-Muunifiyyah Misri katika mwaka wa 1325 B.H.

MWANZO WA MASOMO YAKE
Shaykh alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha al-Azhar na akachukua Shahaadah yake katika mwaka wa 1351 B.H. Baada ya hapo akatakhasusi katika Fiqh na misingi yake na kuendelea masomo yake mpaka akawa miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Misri.

KUFUNZA KWAKE NA KAZI ZAKE
Alianza kufundisha katika shule ambazo zilikuwa ni za Chuo Kikuu cha al-Azhar nchini Misri, baada ya hapo akahama kwenda Saudi Arabia katika 1367 B.H. na kufundisha katika kituo cha Kiislamu Twaa’if, Riyaadh na ‘Unayzah. Baadae wakati kitivo cha Shari’ah kilipofunguliwa Riyaadh, hivyo akaanza kufundisha pale na baadae wakati Chuo Kikuu cha mahakama kilipofunguliwa mwaka wa 1385 B.H. Riyaadh, akawa mudiri wake, na alikuwa miongoni mwa wenye majukumu ya kuandika selebasi yake.

Katika mwaka wa 1391 B.H. akawa mwanachama wa baraza kuu la fatwa Saudi Arabia na makamu wa raisi mpaka alipofariki. Alikuwa pia ni mwanachama wa baraza la wanachuoni watu wazima (wazee) nchini Saudi Arabia.

WANAFUNZI WAKE
Wengi katika wanachuoni wakubwa wa leo walikuwa ni wanafunzi wa Shaykh. Miongoni mwa hawa ni:

1) Shaykh Swaalih al-Luhaydaan, ambaye ni mmoja katika wanachuoni wetu wakubwa hivi leo. Alikuwa ni mkuu wa zamani wa baraza la mahakama nchini Saudi Arabia.

2) Shaykh Swaalih al-Fawzaan, ambaye anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wetu wakubwa hivi leo na ni mwanachama wa baraza la kudumu la fatwa nchini Saudi Arabia.

3) Shaykh Swaalih al-Atram, ambaye alikuwa ni mmoja katika wanachuoni aliyekuwa akiishi nchini Saudi Arabia.

4) Shaykh ‘Abdullaah bin Qu’uud, ambaye alikuwa ni mwanachama wa baraza la kudumu la fatwa nchini Saudi Arabia.

TABIA YAKE
Shaykh alikuwa na sifa ambazo mwanachuoni wa kweli lazima awe nazo. Alikuwa mara nyingi akiwa na tabasamu usoni mwake na alikuwa anajulikana kwa upendo wake wa wema na kutaka kuwasaidia watu wengine. Alikuwa ni mwenye Zuhd katika maisha haya na wala alikuwa hajali uzuri wake pamoja na kuwa alikuwa na uwezo wa kufikia hilo. Alikuwa hapendi kupandishwa na kujulikana licha ya elimu yake kubwa (aliokuwa nayo). Alikuwa kamwe hazungumzii wengine vibaya na alikuwa anajulikana kwa ukarimu wake kwa wageni wake.

Alikuwa anachunga wakati wake kwa kusoma Qur-aan na kujishughulisha na elimu yenye manufaa. Alikuwa vilevile akijali sana juu ya yale yanayotokea na ulimwengu wa Waislamu.

UGONJWA WAKE NA KIFO CHAKE
Shaykh alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu na mafigo, moyo wa maini, na mwisho wake akafa tarehe 25 Rabiy´-ul-Awwal mwaka wa 1415 B.H.

Wasifu huu ni mukhtasari wa yale ambayo Dr. Faalih as-Saghiyr aliyoandika katika kitabu al-Ḩadaa’iq al-Bahiyyah fiy Siyar ba’dh-ul-‘Ulamaa al-Mu’asiriyn (uk. 105-128) na baadhi ya nyongeza.


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 3rd, November 2013