Wasifu Wa Shaykh ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa’diy

JINA LAKE NA KUZALIWA KWAKE Jina lake lilikuwa ni 'Abdur-Rahmaan bin Naaswir bin 'Abdillaah bin Naaswir Aal Sa'diy kutoka katika kabila la Banuu Tamiym. Alizaliwa katika mji wa ´Unayzah tarehe 12 ya Muharram katika mwaka wa 1307 B.H. Mama yake alifariki pindi alipokuwa na umri wa miaka 4, na baba yake alifariki pindi alipokuwa na umri wa miaka 7, hivyo mke wa baba yake akamtunza na akawa anampenda sana zaidi alivyokuwa akiwapenda watoto wake mwenyewe na hivyo akamtunza vizuri sana. MWANZO WA MASOMO YAKE Wakati alipokuwa kijana, aliishi katika nyumba ya mkubwa wake na akaanza kutafuta elimu kwa njia ya bidii. Alihifadhi Qur-aan nzima katika umri wa miaka 12 katika shule ya Sulaymaan bin Daamigh. Kisha baada ya hapo akaanza kusoma kwa wanachuoni waliokuwa katika eneo alipokuwa akiishi. Ilidhihiri kwa haraka ya kwamba ni mwanafunzi mwenye bidii kuliko wanafunzi wenzake, hivyo wakaanza kusoma kwake. Miongoni mwa vitabu alivyohifadhi ni Qur-aan, 'Umdat-ul-Ahkaam, Daliyl-ut-Twalib, mkusanyo wa mashairi mengi ya Ibn ´Abdil-Qawiyy na kitabu cha Ibn al-Qayyim an-Nuuniyyah. WAALIMU WAKE Alikuwa na takriban wanachuoni 10 ambao walikuwa walimu wake, miongoni mwa wale maarufu: 1) Shaykh Swaalih bin 'Uthmaan al-Qaadhiy, huyu ndiye ambaye Shaykh alisoma kwake kwa muda mrefu. 2) Shaykh Muhammad bin 'Abdil-´Aziyz al-Maaniy´. 3) Shaykh Ibraahiym bin Swaalih bin 'Isaa. WANAFUNZI WAKE Alikuwa na wanafunzi wengi sana, ambao baadae wamekuja kuwa katika wanachuoni wakubwa, miongoni mwao ni: 1) Shaykh Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn. Mwanachuoni mkubwa, anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa katika wakati wetu huu, khaswa katika Fiqh . 2) Shaykh 'Abdullaah bin 'Abdil-´Aziyz al-´Aqiyl. Alikuwa ni jaji mkuu wa zamani wa Saudi Arabia na anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia. 3) Shaykh 'Abdullaah al-Bassaam. Ni mmoja katika wanachuoni wakubwa ambao wameandika vitabu vingi maarufu. VITABU VYAKE Shaykh alikuwa ni mwandishi mkubwa na amejulikana kwa ajili ya vitabu vyake vizuri alivyoandika. Aliandika zaidi ya vitabu 40, na vingi katika hivyo vinafundishwa hivi leo na wanachuoni wakubwa. Miongoni mwa vitabu hivyo: 1) Manhaj-us-Saalikiyn. Kitabu kifupi katika Fiqh, ambacho kilikuwa kikifunzwa katika Misikiti. 2) Taysiyr-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan. Hii ni katika Tafsiyr maarufu ya Shaykh inayochukuliwa ni moja katika vitabu bora vimevyoandikwa katika Tafsiyr katika wakati wetu. 3) al-Qawaa´id al-Hisaan li-Tafsiyr-ul-Qur-aan. Kitabu muhimu juu ya misingi ya jinsi mtu ataifahamu Tafsiyr. 4) al-Qawl as-Sadiyd fiy Maqaasid at-Tawhiyd. Hii ni Sharh ya Shaykh ya Kitaab-ut-Tawhiyd cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE: 1) Shaykh Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn kasema kuhusu tafsiri yake: "Hakika, ni kweli kwamba tafsiri ya Shaykh wetu ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa'diy iitwayo Taysiyr-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan huzingatiwa ni moja katika vitabu bora vya tafsiri... na hivyo ninamshauri kila mtu mtu ambaye anataka kujifunza Tafsiyr, basi Maktabah yake isikose kuwa na kitabu hiki." (Utangulizi wa Taysir-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan (uk. wa 7) 2) Dr. Twariq al-Khuwaytir ambaye ameandika wasifu wa Shaykh kasema: "Wanachuoni wamemsifu na kusema ya kwamba alikuwa ni al-'Allaamah al- Mufassir al-Faqiyh al-Usuuliy an-Nahwiy". KIFO CHAKE Shaykh alifariki usiku wa Alkhamisi 23 Juumaadah al-Aakhir mwaka wa 1376 B.H. na wakamzika baada ya kumswalia Swalah ya janaza baada ya Swalah ya Dhuhr. Vijana wote kukiwemo wazee katika mji wa ´Unayzah walihudhuria mazishi yake na watu walikuwa na masikitiko makubwa. Mukhtasari kutoka kitabu cha al-Ḩadaa'iq al-Bahiyyah (19-45) cha Dr. Twaariq al-Khuwaytir, na wasifu umeandikwa na Shaykh ´Abdullaah al-Bassaam, na baadhi ya nyongeza.

JINA LAKE NA KUZALIWA KWAKE
Jina lake lilikuwa ni ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir bin ‘Abdillaah bin Naaswir Aal Sa’diy kutoka katika kabila la Banuu Tamiym. Alizaliwa katika mji wa ´Unayzah tarehe 12 ya Muharram katika mwaka wa 1307 B.H. Mama yake alifariki pindi alipokuwa na umri wa miaka 4, na baba yake alifariki pindi alipokuwa na umri wa miaka 7, hivyo mke wa baba yake akamtunza na akawa anampenda sana zaidi alivyokuwa akiwapenda watoto wake mwenyewe na hivyo akamtunza vizuri sana.

MWANZO WA MASOMO YAKE
Wakati alipokuwa kijana, aliishi katika nyumba ya mkubwa wake na akaanza kutafuta elimu kwa njia ya bidii. Alihifadhi Qur-aan nzima katika umri wa miaka 12 katika shule ya Sulaymaan bin Daamigh. Kisha baada ya hapo akaanza kusoma kwa wanachuoni waliokuwa katika eneo alipokuwa akiishi. Ilidhihiri kwa haraka ya kwamba ni mwanafunzi mwenye bidii kuliko wanafunzi wenzake, hivyo wakaanza kusoma kwake.
Miongoni mwa vitabu alivyohifadhi ni Qur-aan, ‘Umdat-ul-Ahkaam, Daliyl-ut-Twalib, mkusanyo wa mashairi mengi ya Ibn ´Abdil-Qawiyy na kitabu cha Ibn al-Qayyim an-Nuuniyyah.

WAALIMU WAKE
Alikuwa na takriban wanachuoni 10 ambao walikuwa walimu wake, miongoni mwa wale maarufu:

1) Shaykh Swaalih bin ‘Uthmaan al-Qaadhiy, huyu ndiye ambaye Shaykh alisoma kwake kwa muda mrefu.
2) Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-´Aziyz al-Maaniy´.
3) Shaykh Ibraahiym bin Swaalih bin ‘Isaa.

WANAFUNZI WAKE
Alikuwa na wanafunzi wengi sana, ambao baadae wamekuja kuwa katika wanachuoni wakubwa, miongoni mwao ni:

1) Shaykh Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn. Mwanachuoni mkubwa, anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa katika wakati wetu huu, khaswa katika Fiqh .
2) Shaykh ‘Abdullaah bin ‘Abdil-´Aziyz al-´Aqiyl. Alikuwa ni jaji mkuu wa zamani wa Saudi Arabia na anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia.
3) Shaykh ‘Abdullaah al-Bassaam. Ni mmoja katika wanachuoni wakubwa ambao wameandika vitabu vingi maarufu.

VITABU VYAKE
Shaykh alikuwa ni mwandishi mkubwa na amejulikana kwa ajili ya vitabu vyake vizuri alivyoandika. Aliandika zaidi ya vitabu 40, na vingi katika hivyo vinafundishwa hivi leo na wanachuoni wakubwa. Miongoni mwa vitabu hivyo:

1) Manhaj-us-Saalikiyn. Kitabu kifupi katika Fiqh, ambacho kilikuwa kikifunzwa katika Misikiti.
2) Taysiyr-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan. Hii ni katika Tafsiyr maarufu ya Shaykh inayochukuliwa ni moja katika vitabu bora vimevyoandikwa katika Tafsiyr katika wakati wetu.
3) al-Qawaa´id al-Hisaan li-Tafsiyr-ul-Qur-aan. Kitabu muhimu juu ya misingi ya jinsi mtu ataifahamu Tafsiyr.
4) al-Qawl as-Sadiyd fiy Maqaasid at-Tawhiyd. Hii ni Sharh ya Shaykh ya Kitaab-ut-Tawhiyd cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab.

SIFA ZA WANACHUONI JUU YAKE:

1) Shaykh Muhammad bin Swaalih Ibn ´Uthaymiyn kasema kuhusu tafsiri yake: “Hakika, ni kweli kwamba tafsiri ya Shaykh wetu ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa’diy iitwayo Taysiyr-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan huzingatiwa ni moja katika vitabu bora vya tafsiri… na hivyo ninamshauri kila mtu mtu ambaye anataka kujifunza Tafsiyr, basi Maktabah yake isikose kuwa na kitabu hiki.” (Utangulizi wa Taysir-ul-Kariym-ur-Rahmaan fiy Tafsiyr Kalaam-ul-Mannan (uk. wa 7)

2) Dr. Twariq al-Khuwaytir ambaye ameandika wasifu wa Shaykh kasema: “Wanachuoni wamemsifu na kusema ya kwamba alikuwa ni al-‘Allaamah al- Mufassir al-Faqiyh al-Usuuliy an-Nahwiy”.

KIFO CHAKE
Shaykh alifariki usiku wa Alkhamisi 23 Juumaadah al-Aakhir mwaka wa 1376 B.H. na wakamzika baada ya kumswalia Swalah ya janaza baada ya Swalah ya Dhuhr. Vijana wote kukiwemo wazee katika mji wa ´Unayzah walihudhuria mazishi yake na watu walikuwa na masikitiko makubwa.

Mukhtasari kutoka kitabu cha al-Ḩadaa’iq al-Bahiyyah (19-45) cha Dr. Twaariq al-Khuwaytir, na wasifu umeandikwa na Shaykh ´Abdullaah al-Bassaam, na baadhi ya nyongeza.


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 3rd, November 2013