Wasifu Wa Shaykh ‘Abdullaah bin Humayd

JINA LAKE Alikuwa ni mwanachuoni mkubwa, bahari ya elimu, bingwa katika Fiqh Abu ´Abdir-Rahmaan Abu Muhammad 'Abdullaah bin Muhammad bin 'Abdil-´Aziyz bin ´Abdir-Rahmaan bin Hussayn bin Humayd. Ni Kutoka katika kabila maarufu la Baniy Khaalid. KUZALIWA KWAKE NA MWANZO WA MASOMO YAKE Kazaliwa katika mji wa Riyaadh tarehe 29 Dhul-Hijjah katika mwaka wa1329 B.H. Baba yake alifariki alipokuwa na umri wa miaka miwili na mama yake alifariki wakati alipokuwa na umri wa miaka 6. Akawa kipofu akiwa mtoto mdogo kwa kuambukizwa na ndui (vijiupele). Pamoja na hivyo, alianza kuhifadhi Qur-aan kwa msomaji wa Qur-aan ´Aliy bin Muhammad bin Yamiygh. Baada ya yeye kuhifadhi Qur-aan, alianza kusoma kwa wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia. WAALIMU WAKE 1) Shaykh Swaalih bin 'Abdil-´Aziyz Aal ash-Shaykh, ambaye alikuwa jaji Riyaadh. Alisoma 'Aqiydah na Fiqh kwake. 2) Shaykh Muhammad bin 'Abdil-Latwiyf. Alisoma 'Aqiydah na Fiqh kwake. 3) Shaykh Muhammad bin Ibraahiym, Muftiy wa zamani wa Saudi Arabia. Alikuwa akichukuliwa kama mwalimu mkubwa wa Shaykh Ibn Humayd. Alisoma 'Aqiydah, Fiqh, Hadiyth, Musttwalah, sarufi ya Kiarabu na masuala ya mirathi katika Uislamu. Baadae ilikuja kuonekana kuwa mmoja katika wanafunzi wa Shaykh Muhammad bin Ibraahiym wenye bidii zaidi, jambo ambalo lilipelekea Shaykh Muhammad bin Ibraahiym kumfanya kuwa naibu wake wakati ambapo alikuwa hawezi kuja kusomesha katika Msikiti wake. KUFUNDISHA KWAKE Shaykh Ibn Humayd alikuwa akifundisha sana na alikuwa na darsa baada ya Fajr, Dhuhr, ´Aswr na Maghrib. Alikuwa na wanafunzi wengi sana waliosoma na kujifunza mengi kutoka kwake. Alikuwa akifundisha vitabu vikubwa na vidogo. Alikuwa akifundisha ´Aqiydah, Fiqh, sarufi ya Kiarabu, Siyrah, Musttwalah, maadili na tabia ya Kiislamu, mirathi ya Kiislamu na mada zingine. WANAFUNZI WAKE Shaykh alikuwa na wanafunzi wengi ambao baadaye wamekuja kuhesabika kuwa miongoni mwa wanachuoni wakubwa, katika wao: 1) Shaykh Swaalih al-Fawzan, ambaye anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa leo na ni mwanachama wa baraza la kudumu la kutoa fatwa nchini Saudi Arabia. 2) Shaykh Swaalih al-Luhaydaan, ambaye ni mmoja katika wanachuoni wakubwa katika wakati wetu huu. Alikuwa mkuu wa zamani wa baraza la mahakama nchini Saudi Arabia. 3) Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Swaalih. Alikuwa imamu wa zamani wa Msikiti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakimu mkuu wa Madiynah. 4) Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh. Muftiy wa Saudi Arabia wa sasa na ndiye mkuu wa baraza la kudumu la kutoa fatwa nchini Saudi Arabia. KAZI ZAKE 1) Alikuwa hakimu wa Riyaadh, Sudayr, Qaasim na Hijaaz. 2) Alikuwa mshauri binafsi wa mfalme ´Abdul-´Aziyz kuhusiana na masuala ya Dini Saudi Arabia. 3) Yeye ndiye ambaye alikuwa na majukumu ya masuala ya Dini katika Msikiti mkubwa wa Makkah. 4) Alikuwa mkuu wa baraza kuu la mahakama nchini Saudi Arabia. KIFO CHAKE Shaykh alipata kansa katika mwaka wa 1401 B.H. Hata hivyo, Shaykh kamwe hakuwa ni mtu wa kulalamika na alikuwa na subra sana. Katika mwaka wa 1402 B.H ugonjwa ukazidi na hatimaye akapoteza fahamu na akafa tarehe 20 Dhul-Qi'dah mwaka huo huo. Wasifu huu ni mukhtasari wa wasifu uliyoandikwa na mtoto wa Shaykh Dr. Swaalih bin 'Abdillaah bin Humayd katika kitabu al-Ḩadaa'iq al-Bahiyyah fiy Siyar ba'dh-il- 'Ulamaa al-Mu'aasiriyn (uk. 77-102 )

JINA LAKE
Alikuwa ni mwanachuoni mkubwa, bahari ya elimu, bingwa katika Fiqh Abu ´Abdir-Rahmaan Abu Muhammad ‘Abdullaah bin Muhammad bin ‘Abdil-´Aziyz bin ´Abdir-Rahmaan bin Hussayn bin Humayd. Ni Kutoka katika kabila maarufu la Baniy Khaalid.

KUZALIWA KWAKE NA MWANZO WA MASOMO YAKE
Kazaliwa katika mji wa Riyaadh tarehe 29 Dhul-Hijjah katika mwaka wa1329 B.H. Baba yake alifariki alipokuwa na umri wa miaka miwili na mama yake alifariki wakati alipokuwa na umri wa miaka 6. Akawa kipofu akiwa mtoto mdogo kwa kuambukizwa na ndui (vijiupele). Pamoja na hivyo, alianza kuhifadhi Qur-aan kwa msomaji wa Qur-aan ´Aliy bin Muhammad bin Yamiygh. Baada ya yeye kuhifadhi Qur-aan, alianza kusoma kwa wanachuoni wakubwa wa Saudi Arabia.

WAALIMU WAKE
1) Shaykh Swaalih bin ‘Abdil-´Aziyz Aal ash-Shaykh, ambaye alikuwa jaji Riyaadh. Alisoma ‘Aqiydah na Fiqh kwake.

2) Shaykh Muhammad bin ‘Abdil-Latwiyf. Alisoma ‘Aqiydah na Fiqh kwake.

3) Shaykh Muhammad bin Ibraahiym, Muftiy wa zamani wa Saudi Arabia. Alikuwa akichukuliwa kama mwalimu mkubwa wa Shaykh Ibn Humayd. Alisoma ‘Aqiydah, Fiqh, Hadiyth, Musttwalah, sarufi ya Kiarabu na masuala ya mirathi katika Uislamu. Baadae ilikuja kuonekana kuwa mmoja katika wanafunzi wa Shaykh Muhammad bin Ibraahiym wenye bidii zaidi, jambo ambalo lilipelekea Shaykh Muhammad bin Ibraahiym kumfanya kuwa naibu wake wakati ambapo alikuwa hawezi kuja kusomesha katika Msikiti wake.

KUFUNDISHA KWAKE
Shaykh Ibn Humayd alikuwa akifundisha sana na alikuwa na darsa baada ya Fajr, Dhuhr, ´Aswr na Maghrib. Alikuwa na wanafunzi wengi sana waliosoma na kujifunza mengi kutoka kwake. Alikuwa akifundisha vitabu vikubwa na vidogo. Alikuwa akifundisha ´Aqiydah, Fiqh, sarufi ya Kiarabu, Siyrah, Musttwalah, maadili na tabia ya Kiislamu, mirathi ya Kiislamu na mada zingine.

WANAFUNZI WAKE
Shaykh alikuwa na wanafunzi wengi ambao baadaye wamekuja kuhesabika kuwa miongoni mwa wanachuoni wakubwa, katika wao:

1) Shaykh Swaalih al-Fawzan, ambaye anahesabiwa ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa leo na ni mwanachama wa baraza la kudumu la kutoa fatwa nchini Saudi Arabia.

2) Shaykh Swaalih al-Luhaydaan, ambaye ni mmoja katika wanachuoni wakubwa katika wakati wetu huu. Alikuwa mkuu wa zamani wa baraza la mahakama nchini Saudi Arabia.

3) Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Swaalih. Alikuwa imamu wa zamani wa Msikiti Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakimu mkuu wa Madiynah.

4) Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh. Muftiy wa Saudi Arabia wa sasa na ndiye mkuu wa baraza la kudumu la kutoa fatwa nchini Saudi Arabia.

KAZI ZAKE
1) Alikuwa hakimu wa Riyaadh, Sudayr, Qaasim na Hijaaz.

2) Alikuwa mshauri binafsi wa mfalme ´Abdul-´Aziyz kuhusiana na masuala ya Dini Saudi Arabia.

3) Yeye ndiye ambaye alikuwa na majukumu ya masuala ya Dini katika Msikiti mkubwa wa Makkah.

4) Alikuwa mkuu wa baraza kuu la mahakama nchini Saudi Arabia.

KIFO CHAKE
Shaykh alipata kansa katika mwaka wa 1401 B.H. Hata hivyo, Shaykh kamwe hakuwa ni mtu wa kulalamika na alikuwa na subra sana. Katika mwaka wa 1402 B.H ugonjwa ukazidi na hatimaye akapoteza fahamu na akafa tarehe 20 Dhul-Qi’dah mwaka huo huo.

Wasifu huu ni mukhtasari wa wasifu uliyoandikwa na mtoto wa Shaykh Dr. Swaalih bin ‘Abdillaah bin Humayd katika kitabu al-Ḩadaa’iq al-Bahiyyah fiy Siyar ba’dh-il- ‘Ulamaa al-Mu’aasiriyn (uk. 77-102 )


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 5th, November 2013