Wasifu Wa Shaykh ‘Abdullaah al-Ghudayaan

JINA LAKE NA KUZALIWA KWAKE Alikuwa ni mwanachuoni mkubwa katika Fiqh na misingi yake, 'Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin 'Abdir-Razzaaq bin Qaasim al-Ghudayaan kutoka katika kabila la 'Amr bin Tamiym kwa upande wa baba yake na kutoka katika kabila la ´Utaybiy kwa upande wa mama yake. Alizaliwa katika mji wa Zulfi nchini Saudi Arabia mwaka wa 1345 B.H. MASOMO YAKE Alianza masomo yake kwa kuanza kujifunza kusoma na kuandika akiwa ni kijana kwa 'Abdullaah as-Suhaymiy, ´Abdullaah al-Ghayth na Faalih ar-Ruumiy. Kisha akaanza kujifunza misingi katika Fiqh, ´Aqiydah, sarufi ya Kiarabu na masuala ya mirathi katika Uislamu kwa Hamdaan bin Ahmad al-Baatil. Baada ya hapo akasafiri kwenda Riyaadh mwaka wa 1363 B.H. Alikuwa kishamaliza shule ya msingi katika mwaka wa 1368 B.H. na kuanza kusoma katika al-Ma'had al-'Ilmiy mwaka wa 1371 B.H. na kusoma chini ya Shaykh Muhammad bin Ibraahim na wanachuoni wengine. Baadaye alisoma katika kitivo cha Shari´ah na akachukua Shahaadah yake katika mwaka wa 1376 B.H WAALIMU WAKE Shaykh alisoma chini ya wanachuoni wengi sana wakubwa, baadhi yao wamekwishatajwa, na miongoni mwa hao wengine: 1) Shaykh 'Abdul-Aziyz bin Baaz, Muftiy wa Saudi Arabia wa kabla na ni mmoja katika wanachuoni wakubwa wa mbali katika zama hizi. Alisoma Fiqh kwake. 2) Shaykh ´Abdul-´Aziyz ar-Rashiyd, kiongozi wa zamani wa mahakama Riyaadh. Alisoma Fiqh, ´Aqiydah na masuala ya mirathi kwake. 3) Shaykh Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy, mwanachuoni mkubwa wa zama hizi katika Tafsiyr. Alisoma Usuul-ul-Fiqh, mada mbalimbali kuhusiana na Quran na Tafsiyr kwake. 4) Shaykh 'Abdur-Rahmaan al-Afriyqiy, mwanachuoni mkubwa katika Hadiyth. Alisoma Mustwalah na Hadiyth kwake. KAZI ZAKE 1) Kiongozi wa mahakama katika mji wa al-Khobar . 2) Ni mwanachama katika Baraza kuu la Fatwa nchini Saudi Arabia katika mwaka wa 1391 B.H. hadi alipokufa. 3) Ni mwanachama katika Baraza la wanachuoni watu wazima (wazee) nchini Saudi Arabia katika mwaka wa 1386 B.H. mpaka alipokufa. 4) Mwalimu katika kitivo cha Shari´ah katika Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Su'uud Riyaadh. 5) Alikuwa akifutu (akitoa fatwa) katika barnamiji ya an-Nuur 'alaa ad-Darb katika redio ya Saudi Arabia. MAFUNDISHO YAKE Shaykh alikuwa akifundisha tokea mwaka wa 1389 B.H mpaka alipokufa takriban miaka 40 iliopita katika Fiqh, Usuul-ul-Fiqh, al-Qawaa'id al-Fiqhiyyah , Hadiyth, Mustwalah, Tafsiyr, ´Aqiydah katika masiku mengi ya wiki baada ya Maghrib na ´Ishaa na wakati mwingine baada ya Fajr. KIFO CHAKE Shayk alikufa katika mwaka wa 1431 B.H. sawa na tarehe 1 julai mwaka wa 2010 na akizingatiwa wakati wa kifo chake kuwa mmoja katika wanachuoni wakubwa nchini Saudi Arabia. Chanzo: Mukhtasari wa wasifu wa Shaykh kutoka wikipedia kwa lugha ya Kiarabu na baadhi ya nyongeza.

JINA LAKE NA KUZALIWA KWAKE
Alikuwa ni mwanachuoni mkubwa katika Fiqh na misingi yake, ‘Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin ‘Abdir-Razzaaq bin Qaasim al-Ghudayaan kutoka katika kabila la ‘Amr bin Tamiym kwa upande wa baba yake na kutoka katika kabila la ´Utaybiy kwa upande wa mama yake. Alizaliwa katika mji wa Zulfi nchini Saudi Arabia mwaka wa 1345 B.H.

MASOMO YAKE
Alianza masomo yake kwa kuanza kujifunza kusoma na kuandika akiwa ni kijana kwa ‘Abdullaah as-Suhaymiy, ´Abdullaah al-Ghayth na Faalih ar-Ruumiy. Kisha akaanza kujifunza misingi katika Fiqh, ´Aqiydah, sarufi ya Kiarabu na masuala ya mirathi katika Uislamu kwa Hamdaan bin Ahmad al-Baatil. Baada ya hapo akasafiri kwenda Riyaadh mwaka wa 1363 B.H. Alikuwa kishamaliza shule ya msingi katika mwaka wa 1368 B.H. na kuanza kusoma katika al-Ma’had al-‘Ilmiy mwaka wa 1371 B.H. na kusoma chini ya Shaykh Muhammad bin Ibraahim na wanachuoni wengine. Baadaye alisoma katika kitivo cha Shari´ah na akachukua Shahaadah yake katika mwaka wa 1376 B.H

WAALIMU WAKE
Shaykh alisoma chini ya wanachuoni wengi sana wakubwa, baadhi yao wamekwishatajwa, na miongoni mwa hao wengine:

1) Shaykh ‘Abdul-Aziyz bin Baaz, Muftiy wa Saudi Arabia wa kabla na ni mmoja katika wanachuoni wakubwa wa mbali katika zama hizi. Alisoma Fiqh kwake.
2) Shaykh ´Abdul-´Aziyz ar-Rashiyd, kiongozi wa zamani wa mahakama Riyaadh. Alisoma Fiqh, ´Aqiydah na masuala ya mirathi kwake.
3) Shaykh Muhammad al-Amiyn ash-Shanqiytwiy, mwanachuoni mkubwa wa zama hizi katika Tafsiyr. Alisoma Usuul-ul-Fiqh, mada mbalimbali kuhusiana na Quran na Tafsiyr kwake.
4) Shaykh ‘Abdur-Rahmaan al-Afriyqiy, mwanachuoni mkubwa katika Hadiyth. Alisoma Mustwalah na Hadiyth kwake.

KAZI ZAKE
1) Kiongozi wa mahakama katika mji wa al-Khobar .
2) Ni mwanachama katika Baraza kuu la Fatwa nchini Saudi Arabia katika mwaka wa 1391 B.H. hadi alipokufa.
3) Ni mwanachama katika Baraza la wanachuoni watu wazima (wazee) nchini Saudi Arabia katika mwaka wa 1386 B.H. mpaka alipokufa.
4) Mwalimu katika kitivo cha Shari´ah katika Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Su’uud Riyaadh.
5) Alikuwa akifutu (akitoa fatwa) katika barnamiji ya an-Nuur ‘alaa ad-Darb katika redio ya Saudi Arabia.

MAFUNDISHO YAKE
Shaykh alikuwa akifundisha tokea mwaka wa 1389 B.H mpaka alipokufa takriban miaka 40 iliopita katika Fiqh, Usuul-ul-Fiqh, al-Qawaa’id al-Fiqhiyyah , Hadiyth, Mustwalah, Tafsiyr, ´Aqiydah katika masiku mengi ya wiki baada ya Maghrib na ´Ishaa na wakati mwingine baada ya Fajr.

KIFO CHAKE
Shayk alikufa katika mwaka wa 1431 B.H. sawa na tarehe 1 julai mwaka wa 2010 na akizingatiwa wakati wa kifo chake kuwa mmoja katika wanachuoni wakubwa nchini Saudi Arabia.

Chanzo: Mukhtasari wa wasifu wa Shaykh kutoka wikipedia kwa lugha ya Kiarabu na baadhi ya nyongeza.


  • Kitengo: Uncategorized , Wasifu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 3rd, November 2013