Waliojikakama Mambo Ya Jarh na Ta´diyl Ndio Sababu Ya Kuangamia Kwa Dammaaj

Sababu nyingine iliyofanya Dammaaj kuangamia ni mlango wa Jarh na Ta´diyl kufunguliwa kwa watu wote. Walimjeruhi kila yule asiyekubaliana nao. Pasina kujali ni nani. Walimsifu kila mwenye kukubaliana nao hata kama watakuwa wabaya. Kukatokea yakutokea. Hii ndio sababu ya kuangamia kwa Dammaaj. Hatutaki lijirudi. Hatutaki kosa hili lije kwetu. Wanafunzi wenye busara, walinganizi na wanachuoni watahadhari kutumbukia kwenye kosa la al-Hajuuriy. Mwenye busara na mwenye uoni wa mbali ni yule anayepata mafunzo kwa wengine. Tukipitikiwa na mawaidha pasina kuwaidhika, maana ya hili ni kwamba nyoyo zetu ni ngumu na pofu. Mawaidha ni makubwa kama mfano wa jibali, lakini hata hivyo hatuwaidhiki. Ni kitu gani kimeiangamiza Dammaaj? Jibu liko wapi? Kila mmoja mwenye akili na busara anaweza kuja na sababu nyingi juu ya kuangamia kwa Dammaaj. Moja wapo ni suala hili. Jarh na Ta´diyl ilifunguliwa kwa kila mtu. Walimjeruhi waliokuwa wanamtaka na kumsifu waliokuwa wanamtaka. Sababu nyingine ni kuzungumza juu ya Allaah pasina elimu. Inahusiana na Fataawaa. Sawa ikiwa ni Yahyaa al-Hajuuriy anayezungumza au mwengine katika wanafunzi zake, kukatokea. Tuhuma za kuwa Hizbiy, mwengine ni kadhaa na mwengine ni kadhaa. Kulisemwa mengi. Kulizungumziwa juu ya Allaah pasina elimu. Kana kwamba walikuwa wanateremshiwa Wahyi. Walikuwa wanazungumzia mambo yaliyofichana na moyo. Kana kwamba walikuwa wanateremshiwa Wahyi kama alivyokuwa anateremshiwa Wahyi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna sababu nyingi juu ya kuangamia kwa Dammaaj na lililo juu yetu ni kupata mafunzo. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy Chanzo: Dammaaj - Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 13-14 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Sababu nyingine iliyofanya Dammaaj kuangamia ni mlango wa Jarh na Ta´diyl kufunguliwa kwa watu wote. Walimjeruhi kila yule asiyekubaliana nao. Pasina kujali ni nani. Walimsifu kila mwenye kukubaliana nao hata kama watakuwa wabaya. Kukatokea yakutokea. Hii ndio sababu ya kuangamia kwa Dammaaj. Hatutaki lijirudi. Hatutaki kosa hili lije kwetu. Wanafunzi wenye busara, walinganizi na wanachuoni watahadhari kutumbukia kwenye kosa la al-Hajuuriy. Mwenye busara na mwenye uoni wa mbali ni yule anayepata mafunzo kwa wengine. Tukipitikiwa na mawaidha pasina kuwaidhika, maana ya hili ni kwamba nyoyo zetu ni ngumu na pofu. Mawaidha ni makubwa kama mfano wa jibali, lakini hata hivyo hatuwaidhiki.

Ni kitu gani kimeiangamiza Dammaaj? Jibu liko wapi? Kila mmoja mwenye akili na busara anaweza kuja na sababu nyingi juu ya kuangamia kwa Dammaaj. Moja wapo ni suala hili. Jarh na Ta´diyl ilifunguliwa kwa kila mtu. Walimjeruhi waliokuwa wanamtaka na kumsifu waliokuwa wanamtaka.

Sababu nyingine ni kuzungumza juu ya Allaah pasina elimu. Inahusiana na Fataawaa. Sawa ikiwa ni Yahyaa al-Hajuuriy anayezungumza au mwengine katika wanafunzi zake, kukatokea. Tuhuma za kuwa Hizbiy, mwengine ni kadhaa na mwengine ni kadhaa. Kulisemwa mengi. Kulizungumziwa juu ya Allaah pasina elimu. Kana kwamba walikuwa wanateremshiwa Wahyi. Walikuwa wanazungumzia mambo yaliyofichana na moyo. Kana kwamba walikuwa wanateremshiwa Wahyi kama alivyokuwa anateremshiwa Wahyi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna sababu nyingi juu ya kuangamia kwa Dammaaj na lililo juu yetu ni kupata mafunzo.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
Chanzo: Dammaaj – Ja´aluuhaa Shu´lah min Naar ba´d an kaanat Shu´lah min Nuur, uk. 13-14
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , al-Hajuuriy, Yahyaa
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 13th, April 2014