Wakati Wa Zakaat-ul-Fitwr Ukipita Ni Lazima Kuitoa?

Wakati wa kutoa Zakaat-ul-Fitwr ni kuanzia pale ambapo Shawwaal inapoingia mpaka pale ambapo imamu na watu wanapohudhuria katika Swalah ya ´Iyd. Akiitoa siku mbili kabla ya Idi haina neno. Asiicheleweshe mpaka wakati wa Swalah ya ´Iyd. Akiichelewesha mpaka wakati wa Swalah ya ´Iyd, itakuwa bado ni lazima kwake kuitoa. Lakini hata hivyo haitokuwa tena ni Swadaqat-ul-Fitwr, bali itakuwa ni Swadaqah ya kawaida. Siku ya ´Iyd ikipita hali ya kuwa hajaitoa, atatakiwa vilevile kuitoa kwa njia ya kuilipa. Kwa hali yoyote ni lazima kuitoa na asiseme kuwa wakati umeshapita. Itapewa mafukara wa mji ambapo mtu anaishi au mawakala wao ikiwa wamewakilisha mtu.