Wafuasi Wa al-Hajuuriy Wanaopelekwa Na Matamanio Na Hisia

Ninawaambia ndugu ambao wamedanganyika naye ambao ni wapenzi wa kheri wamche Allaah. Qadhiya sio ya hisia. Hakuna kuwa na hisia katika Dini. Ukiona wanachuoni wako upande huu na wewe uko upande mwingine basi tambua kuwa uko katika upotevu. Ukimuona mtu yuko upande huu na wanachuoni wako upande mwingine basi usifurahie juu ya mtu huyo. Hii ni Dini. Kwa nini mtu uwe na hisia na kufuata hisia? Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema: فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ “Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli.” (04:59) Hutomsikia Allaah wala Mtume Wake wakituzungumzisha katika qadhiya yetu hii. Makusudio ni kurudi katika Qur-aan na Sunnah. Qur-aan na Sunnah havitamki, bali wanachuoni ndio wenye kutamka kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Ni wanachuoni wepi?: فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ “... basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli.” (04:59) Makusudio ya kurudi katika Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake ni wanachuoni wanaozungumza kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake. Hivyo sasa, ni wepi hawa? Ina maana leo hakukubaki isipokuwa mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa al-Hajuuriy. Ina maana hakukubaki mwingine zaidi yake yeye. Ndugu! Tuache kuwa na hisia. Tuweni ni wenye Ikhlaasw kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

Ninawaambia ndugu ambao wamedanganyika naye ambao ni wapenzi wa kheri wamche Allaah. Qadhiya sio ya hisia. Hakuna kuwa na hisia katika Dini. Ukiona wanachuoni wako upande huu na wewe uko upande mwingine basi tambua kuwa uko katika upotevu. Ukimuona mtu yuko upande huu na wanachuoni wako upande mwingine basi usifurahie juu ya mtu huyo. Hii ni Dini. Kwa nini mtu uwe na hisia na kufuata hisia? Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ
“Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli.” (04:59)

Hutomsikia Allaah wala Mtume Wake wakituzungumzisha katika qadhiya yetu hii. Makusudio ni kurudi katika Qur-aan na Sunnah. Qur-aan na Sunnah havitamki, bali wanachuoni ndio wenye kutamka kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Ni wanachuoni wepi?:

فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ
“… basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli.” (04:59)

Makusudio ya kurudi katika Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake ni wanachuoni wanaozungumza kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake. Hivyo sasa, ni wepi hawa? Ina maana leo hakukubaki isipokuwa mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa al-Hajuuriy. Ina maana hakukubaki mwingine zaidi yake yeye.

Ndugu! Tuache kuwa na hisia. Tuweni ni wenye Ikhlaasw kwa Allaah (´Azza wa Jalla).