Viumbe Hawana Nguvu Na Uwezo Wa Kumuona Allaah Duniani

Allaah Hatoonekana katika dunia hii. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Yuko juu ya viumbe wote, juu ya mbingu saba, Amestawaa juu ya ´Arshi Yake, nje ya viumbe Wake, pazia Yake ni nuru. Muusa (´alayhis-Salaam) ambaye alimuomba kumuona hakumuona. Kadhalika kutokana na kauli sahihi Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuona usiku wa Israa´ na Mi´iraaj. Alichoona ni nuru. Kwa kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika Makkah aliulizwa: “Je, umemuona Mola Wako?” Akasema: “Ni Nuru, vipi nitaweza kumuona?” Pazia Yake ni nuru. Kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amejizuia katika dunia hii kwa nuru. Nguvu za maono haziwezi kuwa na uthibiti wa kumuona wakati Anapojionyesha. Dalili ya wazi juu ya kauli hii ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwishoni wa kisa cha ad-Dajjaal: “Tambueni kuwa hamtomuona Mola Wenu mpaka pale mtapokufa.” Hii ni dalili ya wazi ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Hatoonekana katika dunia hii. Lakini Allaah Atawapa viumbe nguvu za kuweza kumuona siku ya Qiyaamah na Peponi wakati Atapojionyesha kwao. Atajionyesha kwao na watamuona bila ya kuweza kumzunguka. Kama jinsi wanavyomjua hivi sasa bila ya kumzunguka kwa ujuzi wao, kadhalika watamuona bila ya kumzunguka katika kumuona kwao. Kwa kuwa kiumbe hawezi kumzunguka Muumba. Muumba ndiye mwenye kuwazunguka viumbe wote. Yeye ndiye Anayejua kuhusu wao kila kitu. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 52 Toleo la: 25-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Allaah Hatoonekana katika dunia hii. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Yuko juu ya viumbe wote, juu ya mbingu saba, Amestawaa juu ya ´Arshi Yake, nje ya viumbe Wake, pazia Yake ni nuru. Muusa (´alayhis-Salaam) ambaye alimuomba kumuona hakumuona. Kadhalika kutokana na kauli sahihi Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuona usiku wa Israa´ na Mi´iraaj. Alichoona ni nuru. Kwa kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika Makkah aliulizwa:

“Je, umemuona Mola Wako?”

Akasema:

“Ni Nuru, vipi nitaweza kumuona?”

Pazia Yake ni nuru. Kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Amejizuia katika dunia hii kwa nuru. Nguvu za maono haziwezi kuwa na uthibiti wa kumuona wakati Anapojionyesha. Dalili ya wazi juu ya kauli hii ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwishoni wa kisa cha ad-Dajjaal:

“Tambueni kuwa hamtomuona Mola Wenu mpaka pale mtapokufa.”

Hii ni dalili ya wazi ya kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Hatoonekana katika dunia hii. Lakini Allaah Atawapa viumbe nguvu za kuweza kumuona siku ya Qiyaamah na Peponi wakati Atapojionyesha kwao. Atajionyesha kwao na watamuona bila ya kuweza kumzunguka. Kama jinsi wanavyomjua hivi sasa bila ya kumzunguka kwa ujuzi wao, kadhalika watamuona bila ya kumzunguka katika kumuona kwao. Kwa kuwa kiumbe hawezi kumzunguka Muumba. Muumba ndiye mwenye kuwazunguka viumbe wote. Yeye ndiye Anayejua kuhusu wao kila kitu.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 52
Toleo la: 25-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 25th, May 2014