Vitavyopimwa Kwenye Mizani Ni Vitu Vitatu

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: “Kuamini mizani siku ya Qiyaamah kama ilivyokuja (katika Hadiyth): “... mja atapimwa siku ya Qiyaamah. Atakuwa hapimi uzito wa mbawa ya nzi. Na yatapimwa matendo ya mja kama ilivyokuja katika Athar. [Katika Sunnah ni] kuamini hivo na kulisadikisha. Kumpuuza mwenye kukataa hilo na kuacha kujadiliana naye.” Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuamini mizani ni wajibu. Kwa kuwa maandiko yamepokelewa kutaja hilo. Kama ilivyo katika Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ “Na kipimo Siku hiyo (ya Qiyaamah) kitakuwa ni Haki. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu... ” mpaka mwisho wa Aayah. (07:08) وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ “Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah; basi haitodhulumiwa nafsi yoyote (ile) kitu chochote (kile). Na japokuwa ni uzito wa mbegu ya hardali, Tutaileta. Na inatosheleza Kwetu kuwa Haasibiyn (Wenye kuhesabu).” (21:47) Imethibiti vilevile katika Sunnah twaharifu kwamba matendo ya waja yatapimwa, daftari zao zitapimwa na wao wenyewe watapimwa. Vitakavyopimwa ni vitu vitatu: 1- Mtendaji, 2- Matendo yake, na 3- Daftari lake. Hayo yamethibiti kwa maandiko sahihi. Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy Chanzo: Usuul-us-Sunnah Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=998&size=2h&ext=.rm

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuamini mizani siku ya Qiyaamah kama ilivyokuja (katika Hadiyth): “… mja atapimwa siku ya Qiyaamah. Atakuwa hapimi uzito wa mbawa ya nzi. Na yatapimwa matendo ya mja kama ilivyokuja katika Athar. [Katika Sunnah ni] kuamini hivo na kulisadikisha. Kumpuuza mwenye kukataa hilo na kuacha kujadiliana naye.”

Katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kuamini mizani ni wajibu. Kwa kuwa maandiko yamepokelewa kutaja hilo. Kama ilivyo katika Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
“Na kipimo Siku hiyo (ya Qiyaamah) kitakuwa ni Haki. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu… ” mpaka mwisho wa Aayah. (07:08)

وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ
“Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah; basi haitodhulumiwa nafsi yoyote (ile) kitu chochote (kile). Na japokuwa ni uzito wa mbegu ya hardali, Tutaileta. Na inatosheleza Kwetu kuwa Haasibiyn (Wenye kuhesabu).” (21:47)

Imethibiti vilevile katika Sunnah twaharifu kwamba matendo ya waja yatapimwa, daftari zao zitapimwa na wao wenyewe watapimwa. Vitakavyopimwa ni vitu vitatu:

1- Mtendaji,
2- Matendo yake, na
3- Daftari lake.

Hayo yamethibiti kwa maandiko sahihi.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal ash-Shaybaaniy
Chanzo: Usuul-us-Sunnah
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=998&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 29th, March 2014