Uvumilivu Wa Allaah Wa Kikamilifu

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema katika Hadiyth Swahiyh : "Hakuna ambaye ni mvumilivu kuliko Allaah. Wanamsifia kuwa na mtoto wakati Anawaponya na kuwapa riziki.” Sifa zote kamilifu zilizotimia zinamstahiki Allaah (Ta´ala). Hili ni jambo limethibitishwa na Shari'ah na akili. Ukamilifu huu kunaingia Majina Yake yote na Sifa Zake. Katika ukamilifu huu kunaingia Subira. Subira iliyotajwa na Mjumbe (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) haifanani na subira ya chengine chochote. Subira Yake ni kamilifu yenye nguvu na yenye nguvu za kuogofya. Inakabiliana na matusi ya viumbe waovu. Hawawezi kuepuka nguvu Zake. Maneno yao yote, riziki zao na mahitaji yao vinatokana na Allaah. Hawachumi chochote isipokuwa kwa ukarimu Wake. Anawaponya na kuwapa riziki. Hakupiti wakati isipokuwa wamezungukwa na ukarimu Wake. Amewafungulia milango ya Tawbah, Akawasahilishia kwalo na Akawaita kwalo. Amewaambia ya kwamba Atawasamehe na madhambi yao makubwa na kuwaingiza katika furaha ikiwa tu watatubu. Himidi zote ni Zako eeh Allaah, Mwenye Uvumilifu. Mwandishi: Imaam 'Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa'diy Chanzo: al-Fataawa as-Sa'diyyah, uk. 22 'Aalam-ul-Kutub, 1415/1995

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema katika Hadiyth Swahiyh :

“Hakuna ambaye ni mvumilivu kuliko Allaah. Wanamsifia kuwa na mtoto wakati Anawaponya na kuwapa riziki.”

Sifa zote kamilifu zilizotimia zinamstahiki Allaah (Ta´ala). Hili ni jambo limethibitishwa na Shari’ah na akili. Ukamilifu huu kunaingia Majina Yake yote na Sifa Zake. Katika ukamilifu huu kunaingia Subira. Subira iliyotajwa na Mjumbe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) haifanani na subira ya chengine chochote. Subira Yake ni kamilifu yenye nguvu na yenye nguvu za kuogofya. Inakabiliana na matusi ya viumbe waovu.

Hawawezi kuepuka nguvu Zake. Maneno yao yote, riziki zao na mahitaji yao vinatokana na Allaah. Hawachumi chochote isipokuwa kwa ukarimu Wake. Anawaponya na kuwapa riziki. Hakupiti wakati isipokuwa wamezungukwa na ukarimu Wake.

Amewafungulia milango ya Tawbah, Akawasahilishia kwalo na Akawaita kwalo. Amewaambia ya kwamba Atawasamehe na madhambi yao makubwa na kuwaingiza katika furaha ikiwa tu watatubu.
Himidi zote ni Zako eeh Allaah, Mwenye Uvumilifu.

Mwandishi: Imaam ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa’diy
Chanzo: al-Fataawa as-Sa’diyyah, uk. 22
‘Aalam-ul-Kutub, 1415/1995


  • Kitengo: Uncategorized , Subira ya Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013