Utata Wa Ahl-ut-Ta´atwiyl, Mushabbihah Na Mumatthilah Na Radd Juu Yake

Ama Ahl-ut-Ta´atwiyl, nao ni wale ambao wanakanusha Allaah (Jalla wa ´Alaa) kuwa na Mikono – kama jinsi wanavopinga kuwa na Sifa zingine zote – wanaziwekea taawili kwa kusema maana ya “Mkono” ni uwezo au “Mkono” ni neema. Wanaiwekea taawili kwa kusema maana yake ni uwezo. Wanasema maana ya: لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ “... Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75) yaani uwezo wangu. Waambie Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ametaja Mikono kwa lafdhi ya at-Tathniyah, je Allaah (Jalla wa ´Alaa) na uwezo uili au ana uwezo mmoja? Hakuna jibu jengine zaidi ya kusema kwamba Allaah ana Uwezo mmoja. Si sahihi kusema kwamba Allaah ana uwezo uili. Katika Kauli Yake: لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ “... Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75) Je, mtu anaweza kusema maana yake ni: “Bi qudratayyah”, uwezo wangu uili? Hakuna yeyote awezae kusema hivi. Ama kuiwekea taawili kwa kusema kwamba (maana ya Mikono) ni neema, itakuwa “Wewe una mkono kutoka kwangu (niliyouumba)”, bi maana “Wewe una neema kutoka kwangu”. Akisema mwenye kusema ya kwamba maana ya: لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ “... Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75) Neema zangu mbili! Muulize swali “Je, Allaah ana neema mbili tu?” Sivyo hivyo bali neema zote ni Zake Yeye (Subhaanahu wa Ta´aa). Isitoshe ni kwamba, itakuwa hakuna tofauti kati ya Aadam na (viumbe) wengine ikiwa kama Mikono (ya Allaah) itafasiriwa kuwa ni uwezo. Bi maana itakuwa Allaah Ameumba viumbe vyote kwa Uwezo Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) wakati Allaah Amemtofautisha Aadam na viumbe wengine katika wanaadamu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amemtofautisha kwa dalili ya Kauli Yake: لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ “... Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75) Namna hii ndivyo jinsi ya kuwaraddi watu hawa. Ama Mumatthilah, Qur-aan yao yenyewe inawaraddi kwa Kauli Yake: لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ “Hakuna chochote kinachofanana Naye.” (ash-Shuuraa:11) Kauli Yake tena: وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ “Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.” (al-Ikhlaasw:04) Kauli Yake: هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا “Je, unamjua (mwengine) mwenye Jina Lake?.” (Maryam:65) Kauli Yake: فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ “Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).” (al-Baqarah:22) “an-Nidd”, ni anayeshabihiana na kufanana Naye. Allaah Amekataa kufanyiwa wa kushabihiana Naye na wa kufanana Naye katika viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah hakuna chochote kinachofanana Naye. Haya ndio madhehebu ya Jahmiyyah katika masuala ya Mikono ya Allaah (´Azza wa Jalla). Hii ndio Radd kwao kutokana na yale waliyoyafanyia taawili. Madhehebu ya Mumatthilah na Mushabbihah vilevile ni Radd kwao kutoka katika Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 93-94

Ama Ahl-ut-Ta´atwiyl, nao ni wale ambao wanakanusha Allaah (Jalla wa ´Alaa) kuwa na Mikono – kama jinsi wanavopinga kuwa na Sifa zingine zote – wanaziwekea taawili kwa kusema maana ya “Mkono” ni uwezo au “Mkono” ni neema. Wanaiwekea taawili kwa kusema maana yake ni uwezo. Wanasema maana ya:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ
“… Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

yaani uwezo wangu. Waambie Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ametaja Mikono kwa lafdhi ya at-Tathniyah, je Allaah (Jalla wa ´Alaa) na uwezo uili au ana uwezo mmoja? Hakuna jibu jengine zaidi ya kusema kwamba Allaah ana Uwezo mmoja. Si sahihi kusema kwamba Allaah ana uwezo uili. Katika Kauli Yake:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ
“… Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

Je, mtu anaweza kusema maana yake ni:

“Bi qudratayyah”, uwezo wangu uili? Hakuna yeyote awezae kusema hivi.

Ama kuiwekea taawili kwa kusema kwamba (maana ya Mikono) ni neema, itakuwa “Wewe una mkono kutoka kwangu (niliyouumba)”, bi maana “Wewe una neema kutoka kwangu”. Akisema mwenye kusema ya kwamba maana ya:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ
“… Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

Neema zangu mbili! Muulize swali “Je, Allaah ana neema mbili tu?” Sivyo hivyo bali neema zote ni Zake Yeye (Subhaanahu wa Ta´aa).

Isitoshe ni kwamba, itakuwa hakuna tofauti kati ya Aadam na (viumbe) wengine ikiwa kama Mikono (ya Allaah) itafasiriwa kuwa ni uwezo. Bi maana itakuwa Allaah Ameumba viumbe vyote kwa Uwezo Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) wakati Allaah Amemtofautisha Aadam na viumbe wengine katika wanaadamu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amemtofautisha kwa dalili ya Kauli Yake:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ
“… Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?” (38:75)

Namna hii ndivyo jinsi ya kuwaraddi watu hawa.

Ama Mumatthilah, Qur-aan yao yenyewe inawaraddi kwa Kauli Yake:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye.” (ash-Shuuraa:11)

Kauli Yake tena:

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.” (al-Ikhlaasw:04)

Kauli Yake:

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua (mwengine) mwenye Jina Lake?.” (Maryam:65)

Kauli Yake:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa Allaah Hana Anayelingana nae).” (al-Baqarah:22)

“an-Nidd”, ni anayeshabihiana na kufanana Naye. Allaah Amekataa kufanyiwa wa kushabihiana Naye na wa kufanana Naye katika viumbe Vyake (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah hakuna chochote kinachofanana Naye.

Haya ndio madhehebu ya Jahmiyyah katika masuala ya Mikono ya Allaah (´Azza wa Jalla). Hii ndio Radd kwao kutokana na yale waliyoyafanyia taawili. Madhehebu ya Mumatthilah na Mushabbihah vilevile ni Radd kwao kutoka katika Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 93-94


  • Kitengo: Uncategorized , Ashaa´irah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 15th, February 2014