Urukaji Wa Mipaka Kwa Watu Wa Yahyaa al-Hajuuriy

Hapa kuna swali juu ya al-Hajuuriy na kama kumepitika kitu baina yangu mimi na yeye. Hakukupitika kitu. Kilichopitika baina yangu mimi na yeye ni kile mlichosikia. Baina yangu mimi na yeye hakuna ugomvi wowote. Hata hivyo amezidi kuwatukana wanachuoni wa Sunnah, yeye mwenyewe na wanafunzi zake. Ameruka mipaka. Hakuna yeyote aliyesalimika naye. Hakukupitika kitu baina yangu mimi na yeye, si katika heshima wala mali, mpaka niweze kuzungumza. Niliulizwa juu yake na nikasema kuwa ni punguani. Kwa nini mnaenda Dammaaj? Kwake mtajifunza wehu. Yeye ni kama Shaykh Faalih au huenda zaidi. Nilisema mambo matatu. Dalili zote hizi zimesimama kwake. Anawatukana wanachuoni wa Sunnah, vichwa wa Da´wah ya Salafiyyah, katika vikao vyake kunaimbwa mashairi na yeye anawasifu hawa watukanaji. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na hali mbaya baada ya hali nzuri. Ma´had Dammaaj iliasisiwa ili kufunza Sunnah na sio kwa ajili ya kuwatukana na kuwaponda wanachuoni na Mashaykh wa Sunnah. Hivi sasa imekuwa hivo. Mashairi ya kuwatukana Mashaykh wa Sunnah yanasomwa [mbele yake]. Mtu aseme nini juu ya hili? Ikiwa huu sio upungueni basi sijui ni nini upungueni. Waache waseme yakusema. Waache waseme wanayotaka. Hawatudhuru. Tumeamrishwa kusema haki na kusema mambo jinsi yalivo pasina kuzingatia ni nani atayekasirika au kufurahi. Kama jinsi nimevyowaambia hakuna lolote baina yangu mimi na Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy. Lakini wakati hali ilipofikia kiasi hichi, nikasema lile ambalo ninaamini na ninamuabudu Allaah (´Azza wa Jalla) kwalo. Sisemi zaidi ya haya niliyoyasema. Kumeulizwa sana juu yake. Ninayasema haya ilihali ni mwenye kujua kuwa yanasajiliwa na wayasajali kweli. Kwa kuwa walikuja kwenye Msikiti wangu al-Madiynah na wakaniuliza na nikawaambia kuwa maneno haya ni kweli. Mimi sio mwenye kukimbia. Ama kuhusu urukaji wa mipaka kwake (Ghuluw), basi ni sana. [Kunasemwa]: “Kiongozi wa wanaadamu na majini.” “Lau mtu atasafisha viatu vyake kwa muda wa kiasi gani, basi haki yake itakuwa bado haijatimizwa.” “Sikiliza maneno haya ambayo yanapasua usikivu.” “Lau watamyeyusha, nyama zake zingelikuwa ni Sunnah na vilivyobaki ni Aayah za Qur-aan.” La ajabu ni kwamba wanasema: “Mnasikiza uvumi.” Sisi tumesikia hili kwenye mkanda na kwa sauti za wazungumzaji hawa. Kadhalika tumeyasoma katika baadhi ya vitabu ambavyo vimechapishwa na khaswa kitabu cha ´Abdul-Hamiyd al-Hajuuriy “al-Khiyaanah ad-Da´wiyyah”. Mashairi haya yamo humo. Mwishoni Shaykh Rabiy´ [al-Madkhaliy] ametukanywa kwenye mashairi. Kisha baada ya hapo anamwambia mtukanaji: “Allaah Akubariki!” Mtu aseme nini kuhusu hili? Ikiwa huu sio upunguani basi mimi sijui ni nini upunguani. Tuwe waangalifu na sisi pia tusifuate upungueni. Ninasimama hapa, si kwa sababu ya khofu wala kushindwa, isipokuwa ni kwa sababu haitustahikii kwetu kufuata upunguani. Hayo niliyowaambia ni kwa sababu tu mjue baadhi ya magomvi. Ninaapa kwa Allaah kwamba mtu mwenye akili na aliyemakini mwenye heshima na tabia huuchunga ulimi wake kutokana na maneno kama haya. Lakini wakati mwingine mtu anakuwa ni mwenye kulazimika kuyataja. Nimeyasema, au nimesema baadhi yake, ili muweze kujua ni kwa sababu gani nimesema maneno haya matatu.

Hapa kuna swali juu ya al-Hajuuriy na kama kumepitika kitu baina yangu mimi na yeye. Hakukupitika kitu. Kilichopitika baina yangu mimi na yeye ni kile mlichosikia. Baina yangu mimi na yeye hakuna ugomvi wowote. Hata hivyo amezidi kuwatukana wanachuoni wa Sunnah, yeye mwenyewe na wanafunzi zake. Ameruka mipaka. Hakuna yeyote aliyesalimika naye. Hakukupitika kitu baina yangu mimi na yeye, si katika heshima wala mali, mpaka niweze kuzungumza.

Niliulizwa juu yake na nikasema kuwa ni punguani. Kwa nini mnaenda Dammaaj? Kwake mtajifunza wehu. Yeye ni kama Shaykh Faalih au huenda zaidi. Nilisema mambo matatu. Dalili zote hizi zimesimama kwake.

Anawatukana wanachuoni wa Sunnah, vichwa wa Da´wah ya Salafiyyah, katika vikao vyake kunaimbwa mashairi na yeye anawasifu hawa watukanaji. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na hali mbaya baada ya hali nzuri.

Ma´had Dammaaj iliasisiwa ili kufunza Sunnah na sio kwa ajili ya kuwatukana na kuwaponda wanachuoni na Mashaykh wa Sunnah. Hivi sasa imekuwa hivo. Mashairi ya kuwatukana Mashaykh wa Sunnah yanasomwa [mbele yake]. Mtu aseme nini juu ya hili? Ikiwa huu sio upungueni basi sijui ni nini upungueni.

Waache waseme yakusema. Waache waseme wanayotaka. Hawatudhuru. Tumeamrishwa kusema haki na kusema mambo jinsi yalivo pasina kuzingatia ni nani atayekasirika au kufurahi.

Kama jinsi nimevyowaambia hakuna lolote baina yangu mimi na Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy. Lakini wakati hali ilipofikia kiasi hichi, nikasema lile ambalo ninaamini na ninamuabudu Allaah (´Azza wa Jalla) kwalo. Sisemi zaidi ya haya niliyoyasema. Kumeulizwa sana juu yake. Ninayasema haya ilihali ni mwenye kujua kuwa yanasajiliwa na wayasajali kweli. Kwa kuwa walikuja kwenye Msikiti wangu al-Madiynah na wakaniuliza na nikawaambia kuwa maneno haya ni kweli. Mimi sio mwenye kukimbia.

Ama kuhusu urukaji wa mipaka kwake (Ghuluw), basi ni sana. [Kunasemwa]:

“Kiongozi wa wanaadamu na majini.”

“Lau mtu atasafisha viatu vyake kwa muda wa kiasi gani, basi haki yake itakuwa bado haijatimizwa.”

“Sikiliza maneno haya ambayo yanapasua usikivu.”

“Lau watamyeyusha, nyama zake zingelikuwa ni Sunnah na vilivyobaki ni Aayah za Qur-aan.”

La ajabu ni kwamba wanasema:

“Mnasikiza uvumi.”

Sisi tumesikia hili kwenye mkanda na kwa sauti za wazungumzaji hawa. Kadhalika tumeyasoma katika baadhi ya vitabu ambavyo vimechapishwa na khaswa kitabu cha ´Abdul-Hamiyd al-Hajuuriy “al-Khiyaanah ad-Da´wiyyah”. Mashairi haya yamo humo. Mwishoni Shaykh Rabiy´ [al-Madkhaliy] ametukanywa kwenye mashairi. Kisha baada ya hapo anamwambia mtukanaji:

“Allaah Akubariki!”

Mtu aseme nini kuhusu hili? Ikiwa huu sio upunguani basi mimi sijui ni nini upunguani.

Tuwe waangalifu na sisi pia tusifuate upungueni. Ninasimama hapa, si kwa sababu ya khofu wala kushindwa, isipokuwa ni kwa sababu haitustahikii kwetu kufuata upunguani. Hayo niliyowaambia ni kwa sababu tu mjue baadhi ya magomvi. Ninaapa kwa Allaah kwamba mtu mwenye akili na aliyemakini mwenye heshima na tabia huuchunga ulimi wake kutokana na maneno kama haya. Lakini wakati mwingine mtu anakuwa ni mwenye kulazimika kuyataja. Nimeyasema, au nimesema baadhi yake, ili muweze kujua ni kwa sababu gani nimesema maneno haya matatu.