Uongo Wa Hizbiyyuun Dhidi Ya Ahl-us-Sunnah Na Agenda Ya Ihyaa´ at-Turaath Na al-Ikhwaan al-Muslimuun

Wallaahi naapa ya kwamba tumepata neema chungunzima na zaidi ya tunavyostahiki. Ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwenu, Ahl-us-Sunnah. Jinsi ya Da´wah inavyozidi kuwa kubwa na nguvu, ndio jinsi mnavyozidi kusikia kelele na njama mbaya kutoka katika Da´wah za maadui. Wanakimbiza katika Da´wah ya Ahl-us-Sunnah kwa kutumia uongo. Hata hivyo hawatudhuru: وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا "Na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao." (03:120) Tukisubiri, tukamcha Allaah, tukajisalimisha kwa Allaah na maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, njama zao mbaya hazitotudhuru kitu. Badala yake njama zao zitawadhuru wao wenyewe na himidi zote ni Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Jumuiya Ihyaa´ at-Turaath agenda yao ya kwanza ni kukusanya pesa. Kisha baadaye wakusanye watu na kulingania katika demokrasia. Tofauti baina yetu sisi na wao sio kwa ajili ya pesa, majumba wala nafasi katika jeshi. Tofauti yetu sisi na wao inahusiana na demokrasia. Ndio, wanalingania [watu] katika demokrasia na kadhalika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Wanalingania katika demokrasia na wanajaribu kuwafanya watu wafahamu kuwa ni Uislamu.

Wallaahi naapa ya kwamba tumepata neema chungunzima na zaidi ya tunavyostahiki. Ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwenu, Ahl-us-Sunnah.

Jinsi ya Da´wah inavyozidi kuwa kubwa na nguvu, ndio jinsi mnavyozidi kusikia kelele na njama mbaya kutoka katika Da´wah za maadui. Wanakimbiza katika Da´wah ya Ahl-us-Sunnah kwa kutumia uongo. Hata hivyo hawatudhuru:

وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا
“Na mkisubiri na mkawa na taqwa haitokudhuruni chochote katika hila zao.” (03:120)

Tukisubiri, tukamcha Allaah, tukajisalimisha kwa Allaah na maamrisho Yake na kujiepusha na makatazo Yake, njama zao mbaya hazitotudhuru kitu. Badala yake njama zao zitawadhuru wao wenyewe na himidi zote ni Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Jumuiya Ihyaa´ at-Turaath agenda yao ya kwanza ni kukusanya pesa. Kisha baadaye wakusanye watu na kulingania katika demokrasia. Tofauti baina yetu sisi na wao sio kwa ajili ya pesa, majumba wala nafasi katika jeshi. Tofauti yetu sisi na wao inahusiana na demokrasia. Ndio, wanalingania [watu] katika demokrasia na kadhalika al-Ikhwaan al-Muslimuun. Wanalingania katika demokrasia na wanajaribu kuwafanya watu wafahamu kuwa ni Uislamu.