Uongo Dhidi Ya Ibn Taymiyyah Na Kushuka Kwa Allaah

Ahl-us-Sunnah wanasema kwamba Allaah hushuka kwenye mbingu ya chini kama alivyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) bila ya kufikiria hilo. Hawaelezei namna ya Sifa za Allaah kama zilivyo sifa za viumbe. Hawafikirii hata Sifa za Allaah. Mu'attwilah wanaokanusha Kushuka walifanya hivyo baada ya kulifikiria hilo. Wakaona kuwa kushuka kwa Allaah ni kama kushuka kwa viumbe. Kutokana na hili, wakawashutumu Ahl-us-Sunnah ya kwamba wanamfananisha Allaah na viumbe kwa kuthibitisha kwao Kushuka. Baadhi yao wakazusha uongo dhidi ya Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah na kwamba alishuka [teremka] mimbari na kusema: "Allaah hushuka kama jinsi ninavyoshuka mimi." Hili limesemwa na Ibn Batuutah. Huu ni uongo dhidi yake (Rahimahu Allaah). Ibn Taymiyyah alifungwa wakati Ibn Batuutah alipokwenda Damaskus. Yule ambaye anataka kujua ´Aqiydah aliyokuwa nayo Ibn Taymiyyah asome kitabu chake "Sharh Hadiyth-in-Nuzuul". Humo amekataza kufanana kwa kushuka kwa Allaah na viumbe. Sababu ya kumsingizia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengine kwa hili, ni kwa sababu Kushuka wanakokuelewa tu ni kushuka kwa viumbe. Walipoona kuwa Ahl-us-Sunnah wanathibitisha Kushuka, wakawatuhumu kumfananisha Allaah na viumbe. Ametakasika Allaah kwa hili. Mwandishi: Shaykh 'Abdur-Razzaaq bin 'Abdil-Muhsin al-'Abbaad Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 50

Ahl-us-Sunnah wanasema kwamba Allaah hushuka kwenye mbingu ya chini kama alivyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) bila ya kufikiria hilo. Hawaelezei namna ya Sifa za Allaah kama zilivyo sifa za viumbe. Hawafikirii hata Sifa za Allaah.

Mu’attwilah wanaokanusha Kushuka walifanya hivyo baada ya kulifikiria hilo. Wakaona kuwa kushuka kwa Allaah ni kama kushuka kwa viumbe. Kutokana na hili, wakawashutumu Ahl-us-Sunnah ya kwamba wanamfananisha Allaah na viumbe kwa kuthibitisha kwao Kushuka.

Baadhi yao wakazusha uongo dhidi ya Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah na kwamba alishuka [teremka] mimbari na kusema:

“Allaah hushuka kama jinsi ninavyoshuka mimi.”

Hili limesemwa na Ibn Batuutah. Huu ni uongo dhidi yake (Rahimahu Allaah). Ibn Taymiyyah alifungwa wakati Ibn Batuutah alipokwenda Damaskus. Yule ambaye anataka kujua ´Aqiydah aliyokuwa nayo Ibn Taymiyyah asome kitabu chake “Sharh Hadiyth-in-Nuzuul”. Humo amekataza kufanana kwa kushuka kwa Allaah na viumbe. Sababu ya kumsingizia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengine kwa hili, ni kwa sababu Kushuka wanakokuelewa tu ni kushuka kwa viumbe. Walipoona kuwa Ahl-us-Sunnah wanathibitisha Kushuka, wakawatuhumu kumfananisha Allaah na viumbe. Ametakasika Allaah kwa hili.

Mwandishi: Shaykh ‘Abdur-Razzaaq bin ‘Abdil-Muhsin al-‘Abbaad
Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 50


  • Kitengo: Uncategorized , Kushuka (kuteremka) kwa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 27th, October 2013