Unataka Mtawala Mzuri? Wako Wapi Sasa Rai Wazuri!

Watu wengi wanataka viongozi wao wawe wakamilifu kabisa kiasi wanavyoweza. Bila ya shaka tunataka hivi. Tunataka watawala wawe wakamilifu kiasa na wanavyoweza. Lakini hata hivyo sisi hatutangamani nao kikamilifu kiasi na tunavyoweza. Kwa msemo mwingine baadhi ya rai wanataka watawala wawe wakamilifu kiasi na wanavyoweza na wakati rai wao wenyewe ni wapungufu kiasi na inavyowezekana! Je, huu ni uadilifu? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sio uadilifu. Ikiwa unataka upewe haki kikamilifu na wewe unatakiwa kutoa haki ilio juu yako kikamilifu. Vinginevyo hutakiwi kuomba kitu. Katika hekima ya Allaah (´Azza wa Jalla) ni kwamba watawala wanakuwa kama jinsi rai wanavokuwa. Ni hekima mtawala kuwa kama jinsi rai walivo. Akiwa bora, wanakuwa wabora. Akiwa mbaya, wanakuwa wabaya. Katika upokezi: “Kama mtavyokuwa ndivyo mtavyotawaliwa.” Ina maana ya kwamba mtawala anawaongoza watu kutokana na hali zao. Mapokezi haya hata kama sio sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata hivyo yana maana sahihi. Soma Kauli ya Allaah: وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ “Na hivyo ndivyo Tunavyowaelekeza baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wao kwa wao, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” (06:129) Rai wakiwa madhalimu watawala wanawaendea juu. Rai wakiwa wazuri watawala na wao pia wanakuwa wazuri na kinyume chake. Ikiwa mtawala ni mzuri rai na wao pia wanakuwa wazuri. Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn Chanzo: al-Liqaa' ash-Shahriy (51 A) Toleo la: 08-07-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Watu wengi wanataka viongozi wao wawe wakamilifu kabisa kiasi wanavyoweza. Bila ya shaka tunataka hivi. Tunataka watawala wawe wakamilifu kiasa na wanavyoweza. Lakini hata hivyo sisi hatutangamani nao kikamilifu kiasi na tunavyoweza. Kwa msemo mwingine baadhi ya rai wanataka watawala wawe wakamilifu kiasi na wanavyoweza na wakati rai wao wenyewe ni wapungufu kiasi na inavyowezekana! Je, huu ni uadilifu? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba sio uadilifu. Ikiwa unataka upewe haki kikamilifu na wewe unatakiwa kutoa haki ilio juu yako kikamilifu. Vinginevyo hutakiwi kuomba kitu.

Katika hekima ya Allaah (´Azza wa Jalla) ni kwamba watawala wanakuwa kama jinsi rai wanavokuwa. Ni hekima mtawala kuwa kama jinsi rai walivo. Akiwa bora, wanakuwa wabora. Akiwa mbaya, wanakuwa wabaya. Katika upokezi:

“Kama mtavyokuwa ndivyo mtavyotawaliwa.”

Ina maana ya kwamba mtawala anawaongoza watu kutokana na hali zao. Mapokezi haya hata kama sio sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata hivyo yana maana sahihi. Soma Kauli ya Allaah:

وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
“Na hivyo ndivyo Tunavyowaelekeza baadhi ya madhalimu kuwa marafiki wao kwa wao, kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.” (06:129)

Rai wakiwa madhalimu watawala wanawaendea juu. Rai wakiwa wazuri watawala na wao pia wanakuwa wazuri na kinyume chake. Ikiwa mtawala ni mzuri rai na wao pia wanakuwa wazuri.

Mzungumzaji: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Chanzo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (51 A)
Toleo la: 08-07-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Kukufurisha na Kuhukumu
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Tuesday 8th, July 2014