Unamjua Mtu Huyu?

Kuna mtu alitujia katika chuo kikuu cha Kiislamu. Mmoja miongoni mwa waliomuhoji akamuuliza kuhusu mapote. Bila ya shaka muulizaji alikuwa akilenga mapote yanayojulikana kama Jahmiyyah, Mu´tazilah, ´Ashaa´irah, Maaturiydiyyah, al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Mwanafunzi huyo hakuwa anajua [kundi] lolote katika hayo. Badala yake akasema: “Pote ambalo ni khatari zaidi ni Jaamiyyah.” Alikuwa ni mwanafunzi kijana ambaye amehifadhi Qur-aan. Anakuja kutoka katika mji moja wapo katika miji yetu. Ndugu yetu akamwambia: “Mwanangu mpenzi! Wewe ni kijana mwenye akili. Umehifadhi Qur-aan. Unaonesha alama nzuri. Ni nani aliekwambia kwamba kuna pote linaloitwa Jaamiyyah?” Kijana huyo akamuelekeza kwa Qaadhiy mmoja hivi. Mtu huyo akamuuliza kijana huyo kama anamjua Shaykh huyo ambaye watu wanajinasibisha naye. Kijana huyo akasema kwamba hamjui. Akamuuliza kama anajua ni nani Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy? Kijana huyo akasema kwamba hamfahamu. Akamuuliza kama anajua vitabu vyake? Kijana huyo akasema hamjui. Akamuuliza kama anajua kuwa yeye ndiye alikuwa ni msimamizi wa kitivo cha Hadiyth. Akamuuliza kama anajua kuwa yeye ndiye alikuwa raisi wa kitivo cha ´Aqiydah katika chuo kikuu. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym [Aal ash-Shaykh]. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa akitoa darsa kwenye Msikiti mtukufu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka alipokufa. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa anafuata Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na analingania katika hilo. Kijana huyo akasema kuwa hajui kitu katika hayo. Ndugu huyo aliyemuhoji akasema: “Utaposimama mbele ya Allaah kesho siku ya Qiyaamah ukiwa pamoja na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy na akakuuliza “Kutokana na dalili ipi katika Qur-aan au Sunnah unanitukana na unawanasibisha watu na jina langu?” Utasema nini kumwambia Mola Wako?” Mtu huyo aliyemuhoji anasema kwamba kijana huyo akaanza kupasuka kwa kulia na kumwambia kwamba amemuamsha na akamueleza jinsi alivyokuwa anamtukana mwanachuoni huyu zaidi ya miaka khamsini. Akamuomba Allaah Amjaze kheri na amuoneshe vitabu vyake ili astafidi navyo.

Kuna mtu alitujia katika chuo kikuu cha Kiislamu. Mmoja miongoni mwa waliomuhoji akamuuliza kuhusu mapote. Bila ya shaka muulizaji alikuwa akilenga mapote yanayojulikana kama Jahmiyyah, Mu´tazilah, ´Ashaa´irah, Maaturiydiyyah, al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Mwanafunzi huyo hakuwa anajua [kundi] lolote katika hayo. Badala yake akasema:

“Pote ambalo ni khatari zaidi ni Jaamiyyah.”

Alikuwa ni mwanafunzi kijana ambaye amehifadhi Qur-aan. Anakuja kutoka katika mji moja wapo katika miji yetu. Ndugu yetu akamwambia:

“Mwanangu mpenzi! Wewe ni kijana mwenye akili. Umehifadhi Qur-aan. Unaonesha alama nzuri. Ni nani aliekwambia kwamba kuna pote linaloitwa Jaamiyyah?”

Kijana huyo akamuelekeza kwa Qaadhiy mmoja hivi. Mtu huyo akamuuliza kijana huyo kama anamjua Shaykh huyo ambaye watu wanajinasibisha naye. Kijana huyo akasema kwamba hamjui. Akamuuliza kama anajua ni nani Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy? Kijana huyo akasema kwamba hamfahamu. Akamuuliza kama anajua vitabu vyake? Kijana huyo akasema hamjui. Akamuuliza kama anajua kuwa yeye ndiye alikuwa ni msimamizi wa kitivo cha Hadiyth. Akamuuliza kama anajua kuwa yeye ndiye alikuwa raisi wa kitivo cha ´Aqiydah katika chuo kikuu. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym [Aal ash-Shaykh]. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa akitoa darsa kwenye Msikiti mtukufu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka alipokufa. Akamuuliza kama anajua kuwa alikuwa anafuata Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na analingania katika hilo. Kijana huyo akasema kuwa hajui kitu katika hayo. Ndugu huyo aliyemuhoji akasema:

“Utaposimama mbele ya Allaah kesho siku ya Qiyaamah ukiwa pamoja na Shaykh Muhammad Amaan al-Jaamiy na akakuuliza “Kutokana na dalili ipi katika Qur-aan au Sunnah unanitukana na unawanasibisha watu na jina langu?” Utasema nini kumwambia Mola Wako?”

Mtu huyo aliyemuhoji anasema kwamba kijana huyo akaanza kupasuka kwa kulia na kumwambia kwamba amemuamsha na akamueleza jinsi alivyokuwa anamtukana mwanachuoni huyu zaidi ya miaka khamsini. Akamuomba Allaah Amjaze kheri na amuoneshe vitabu vyake ili astafidi navyo.