Umuhimu Wa Swalah Ya Jamaa´ah

Imaam Ibn Baaz: Makusudio ya haya ni kuwa ni wajibu kwa waumini kukimbilia Swalah ya Jamaa´ah, na haijuzu kuchukulia hilo sahali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaka kuchoma nyumba za wale wasiohudhuria Jamaa´ah [Msikitini]. Ni wajibu kwa Waislamu kujitahidi kuhudhuria Swalah ya Jamaa´ah na wajiepushe na kuichukulia sahali na kuswali nyumbani. Watu wengi wanachukulia sahali na kuswali nyumbani - Swalah ya alfajiri na huenda hata ´Ishaa anaswali nyumbani. Huu ni munkari. Ni wajibu kwenda Misikitini na kuswali na Waislamu katika vipindi vyote vitano. Na kwa hili alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Abdullaah bin Ummi Maktuum [ambaye alikuwa kipofu]: "Unasikia adhaana?". Akajibu "Ndio" Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: "Ni wajibu kwako". Na akasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Atakayesikia adhaana na asiitikie (asende), basi hana Swalah isipokuwa kama ana udhuru." Aliulizwa Ibnu ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): "Ni udhuru upi unaokusudiwa?" Akasema: "Ni khofo au maradhi.” Kitendo cha kutaka kuchoma nyumba zao [wanaume wasiohudhuria Swalah Msikitini] inaonesha kuwa ni jambo kubwa. Anasema Ibnu Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu): "Hatujaona anaepuuzia Swalah ya Jamaa´ah ila mnafiki mwenye unafiki maalumu."

Imaam Ibn Baaz:

Makusudio ya haya ni kuwa ni wajibu kwa waumini kukimbilia Swalah ya Jamaa´ah, na haijuzu kuchukulia hilo sahali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaka kuchoma nyumba za wale wasiohudhuria Jamaa´ah [Msikitini]. Ni wajibu kwa Waislamu kujitahidi kuhudhuria Swalah ya Jamaa´ah na wajiepushe na kuichukulia sahali na kuswali nyumbani. Watu wengi wanachukulia sahali na kuswali nyumbani – Swalah ya alfajiri na huenda hata ´Ishaa anaswali nyumbani. Huu ni munkari. Ni wajibu kwenda Misikitini na kuswali na Waislamu katika vipindi vyote vitano. Na kwa hili alisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Abdullaah bin Ummi Maktuum [ambaye alikuwa kipofu]:

“Unasikia adhaana?”. Akajibu “Ndio” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
“Ni wajibu kwako”. Na akasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayesikia adhaana na asiitikie (asende), basi hana Swalah isipokuwa kama ana udhuru.”

Aliulizwa Ibnu ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Ni udhuru upi unaokusudiwa?” Akasema: “Ni khofo au maradhi.”

Kitendo cha kutaka kuchoma nyumba zao [wanaume wasiohudhuria Swalah Msikitini] inaonesha kuwa ni jambo kubwa.

Anasema Ibnu Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Hatujaona anaepuuzia Swalah ya Jamaa´ah ila mnafiki mwenye unafiki maalumu.”