Ufafanuzi Juu Ya Masuala Ya Kwamba Matamshi Ya Qur-aan Yameumbwa

5- Usiseme Qur-aan ni kiumbe (imeumbwa) kwa kule kusomwa hakika maneno ya Allaah yanawekwa wazi kwa kule kutamkwa --------------------------- MAELEZO Haya ni madhehebu ya tatu katika masuala haya. 1- Madhebu ya kwanza wao wanaweka wazi kwamba Qur-aan imeumbwa. 2- Madhehebu ya pili wanasimama, bi maana hawasemi kuwa imeumbwa au haikuumbwa. 3- Madhehebu ya tatu wanasema kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa. Anasema mwenye kusema “matamshi ya Qur-aan yameumbwa.” Hili kwa hakika ni udanganyifu wa kutaka kusema kwamba imeumbwa. Haijuzu kwako kusema kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa kama jinsi haijuzu vilevile kusema kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa. Bali ni lazima kufafanua hilo. Ukisema matamshi ya Qur-aan yameumbwa na wala usifafanue hilo, haya ni madhehebu ya Jahmiyyah. Ukisema vilevile kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa, huku ni kuipa nguvu kauli ya Jahmiyyah. Kwa kuwa ukisema kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa, utakuwa umeingiza matendo yako wewe pamoja na Matendo ya Allaah na umefanya kuwa tendo lako halikuumbwa. Haya ni madhehebu ya Qadariyyah ambao wanapinga kuwepo kwa Qadar na wamewafanya viumbe wao wenyewe ndio wenye kuvumbua na kuumba matendo yao. Ni lazima kuweka wazi na kufafanua hilo kwa kusema “unataka kukusudia nini kwa kusema “matamshi ya Qur-aan”, je, unakusudia utamshi na sauti au unakusudia kile kinachotamkwa? - Ikiwa unakusudia kile kinachotamkwa basi haikuumbwa. Kinachotamkwa ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa). - Ama ikiwa unakusudia utamshi unaotamkwa na ulimi wako, hili limeumbwa. Ulimi wako umeumbwa, sauti yako imeumbwa na utamshi wako umeumbwa. Lakini kile kinachotamkwa na kufanyiwa kazi, hakikuumbwa. Ni lazima kulifafanua. Wao wanachotaka ni kusema kwa jumla ya kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa au useme hayakuumbwa. Ukifanya hivyo, basi wanaingia kwa kupitia njia hii. Ni lazima ufafanue ili uwakoseshe njia ya kupita. Kwa ajili hii ndio maana wanasema Ahl-us-Sunnah: “Sauti ni sauti ya msomaji na Maneno ni Maneno ya Al-Baariy.” yaani kinachotamkwa ni Maneno ya Allaah. Ama utamshi na utendaji, haya ni maneno ya kiumbe. Sauti yake imeumbwa na utamko wake (msomaji) umeumbwa. Kwa ajili hii ndio maana usomaji na sauti yakatofautiana. Baadhi ya sauti ni nzuri sana na sauti zingine sio nzuri sana. Baadhi ya zingine ni nzuri kiasi na zingine sio nzuri kiasi. Hii ni dalili inayoonesha kwamba sauti zimeumbwa na wasomaji wanatofautiana, baadhi yao wamepewa sauti nzuri zaidi na wengine wamepewa chini ya hapo. Ama Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni lazima yawe katika hali ya juu kabisa ya ukamilifu. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 76-77

5- Usiseme Qur-aan ni kiumbe (imeumbwa) kwa kule kusomwa

hakika maneno ya Allaah yanawekwa wazi kwa kule kutamkwa
—————————

MAELEZO

Haya ni madhehebu ya tatu katika masuala haya.

1- Madhebu ya kwanza wao wanaweka wazi kwamba Qur-aan imeumbwa.

2- Madhehebu ya pili wanasimama, bi maana hawasemi kuwa imeumbwa au haikuumbwa.

3- Madhehebu ya tatu wanasema kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa. Anasema mwenye kusema “matamshi ya Qur-aan yameumbwa.”

Hili kwa hakika ni udanganyifu wa kutaka kusema kwamba imeumbwa. Haijuzu kwako kusema kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa kama jinsi haijuzu vilevile kusema kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa. Bali ni lazima kufafanua hilo. Ukisema matamshi ya Qur-aan yameumbwa na wala usifafanue hilo, haya ni madhehebu ya Jahmiyyah. Ukisema vilevile kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa, huku ni kuipa nguvu kauli ya Jahmiyyah. Kwa kuwa ukisema kwamba matamshi ya Qur-aan hayakuumbwa, utakuwa umeingiza matendo yako wewe pamoja na Matendo ya Allaah na umefanya kuwa tendo lako halikuumbwa. Haya ni madhehebu ya Qadariyyah ambao wanapinga kuwepo kwa Qadar na wamewafanya viumbe wao wenyewe ndio wenye kuvumbua na kuumba matendo yao. Ni lazima kuweka wazi na kufafanua hilo kwa kusema “unataka kukusudia nini kwa kusema “matamshi ya Qur-aan”, je, unakusudia utamshi na sauti au unakusudia kile kinachotamkwa?

– Ikiwa unakusudia kile kinachotamkwa basi haikuumbwa. Kinachotamkwa ni Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa).

– Ama ikiwa unakusudia utamshi unaotamkwa na ulimi wako, hili limeumbwa. Ulimi wako umeumbwa, sauti yako imeumbwa na utamshi wako umeumbwa. Lakini kile kinachotamkwa na kufanyiwa kazi, hakikuumbwa. Ni lazima kulifafanua.

Wao wanachotaka ni kusema kwa jumla ya kwamba matamshi ya Qur-aan yameumbwa au useme hayakuumbwa. Ukifanya hivyo, basi wanaingia kwa kupitia njia hii. Ni lazima ufafanue ili uwakoseshe njia ya kupita. Kwa ajili hii ndio maana wanasema Ahl-us-Sunnah:

“Sauti ni sauti ya msomaji na Maneno ni Maneno ya Al-Baariy.”

yaani kinachotamkwa ni Maneno ya Allaah. Ama utamshi na utendaji, haya ni maneno ya kiumbe. Sauti yake imeumbwa na utamko wake (msomaji) umeumbwa. Kwa ajili hii ndio maana usomaji na sauti yakatofautiana. Baadhi ya sauti ni nzuri sana na sauti zingine sio nzuri sana. Baadhi ya zingine ni nzuri kiasi na zingine sio nzuri kiasi. Hii ni dalili inayoonesha kwamba sauti zimeumbwa na wasomaji wanatofautiana, baadhi yao wamepewa sauti nzuri zaidi na wengine wamepewa chini ya hapo. Ama Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni lazima yawe katika hali ya juu kabisa ya ukamilifu.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 76-77


  • Kitengo: Uncategorized , Jahmiyyah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 14th, February 2014