Udhuru Kwa Sababu Ya Ujinga (02)

Imaam al-Albaaniy: Kwa mfano yule anayeishi Jordan, Syria na Misri ambapo wengi katika maulamaa wao hawajui hii ´Aqiydah - kuwa Allaah yuko juu ya Arshi - Je watapewa udhuru hawa watu? Tunasema "ndio" Lakini sivyo kwa mgeni ambaye anaishi kwenye mji huu (Saudi Arabia) ambao Allaah Kawapatia zawadi nyingi. Moja muhimu sana ni Da´wah ya Tawhiyd. Allaah Kafanya sahali kwenye mji huu kiasi cha miaka 100 kupitia Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Akaihuisha Da´wah ya Tawhiyd baada ya kuwa Shirki uabudu wa mathanamu ulikuwa umekithiri takriban kwenye miji yote ya Kiislamu na kwenye mji huu wa Saudi. Allaah Akawaokoa waja wake kupitia mtu huyu. Kisha harakati zake zikasambaa kwenye miji mingine ya Kiislamu, lakini kwa tofauti na kwa uchache kabisa. Mgeni hapa, katika wale wasiowaarabu na waarabu, anasikia usiku na mchana ´Aqiydah ya Tawhiyd na kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake, na kulingana Kwake sawa hakujulikani namna gani na kwamba ni Bid´ha kuuliza namna alivyolingana sawa, huyu hapewi udhuru. Kwa kuwa anaishi kwenye mazingira ambayo yanafanana na mazingira ya kijakazi yule [wa zama za Mtume]. Wapi alijua yule kijakazi ´Aqiydah (sahihi)? Katika jamii aliyokuwa akiishi. Bwana zake na watoto wao wote walikuwa wakiiongelea ´Aqiydah sahihi. Kwa nini na yeye asiwi na ´Aqiydah sahhi? Kwa nini na yeye ´Aqiydah yake isiwe sahihi?

Imaam al-Albaaniy:

Kwa mfano yule anayeishi Jordan, Syria na Misri ambapo wengi katika maulamaa wao hawajui hii ´Aqiydah – kuwa Allaah yuko juu ya Arshi – Je watapewa udhuru hawa watu? Tunasema “ndio” Lakini sivyo kwa mgeni ambaye anaishi kwenye mji huu (Saudi Arabia) ambao Allaah Kawapatia zawadi nyingi. Moja muhimu sana ni Da´wah ya Tawhiyd. Allaah Kafanya sahali kwenye mji huu kiasi cha miaka 100 kupitia Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). Akaihuisha Da´wah ya Tawhiyd baada ya kuwa Shirki uabudu wa mathanamu ulikuwa umekithiri takriban kwenye miji yote ya Kiislamu na kwenye mji huu wa Saudi. Allaah Akawaokoa waja wake kupitia mtu huyu. Kisha harakati zake zikasambaa kwenye miji mingine ya Kiislamu, lakini kwa tofauti na kwa uchache kabisa. Mgeni hapa, katika wale wasiowaarabu na waarabu, anasikia usiku na mchana ´Aqiydah ya Tawhiyd na kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake, na kulingana Kwake sawa hakujulikani namna gani na kwamba ni Bid´ha kuuliza namna alivyolingana sawa, huyu hapewi udhuru. Kwa kuwa anaishi kwenye mazingira ambayo yanafanana na mazingira ya kijakazi yule [wa zama za Mtume]. Wapi alijua yule kijakazi ´Aqiydah (sahihi)? Katika jamii aliyokuwa akiishi. Bwana zake na watoto wao wote walikuwa wakiiongelea ´Aqiydah sahihi. Kwa nini na yeye asiwi na ´Aqiydah sahhi? Kwa nini na yeye ´Aqiydah yake isiwe sahihi?