Tunafurahia Vita Vya Dammaaj?

Miongoni mwa maneno yake[1] pia anasema: “Watu wako katika huzuni wakati wao wako katika furaha.” Ninaapa kwa Allaah ya kwamba si kweli. Maneno haya ni uongo. Anayetangamana na sisi anajua hili. Tufurahie nini? Tufurahie ndugu zetu, dada zetu, wavulana wenu na wasichana wetu Dammaaj? Tufurahie nini? Wavulana na wasichana wa Waislamu ambao wameshambuliwa katika manyumba yao? Tufurahie damu isiyokuwa na hatia na safi kumwagwa? Tufurahie manyumba kubomolewa? Tufurahie watu wanaotishwa na kupigwa? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba lau tutafurahia hayo basi kutakuwa hakuna kheri yoyote kwetu. Tulikuwa Sanaa´ wiki ya kwanza wakati vita ya mwisho ilipopamba moto. Ilikuwa katika saa ya mwisho wakati wa Ijumaa. Niliona jinsi kila Shaykh amekaa kwenye kona na akimlilia Allaah (´Azza wa Jalla) afariji Dammaaj. Si wewe, B. Jamaal, al-Hajuuriy wala mtu mwingine anajua hilo. Allaah ndiye Anajua hilo. Tulikuwepo pale. Kila mmoja anamuomba Allaah na kuwaamrisha wengine waliokuwa nje wamuombe Allaah juu ya ndugu zao. Tunafurahia? Mche Allaah! Huu ni uongo unawazushia ndugu zako na unawadhulumu na unawatuhumu ya kwamba wanafurahia. Hakuna furaha. Sisi tunajua ya kwamba watu wa Dammaaj wamefanyiwa uadui na uasi na Huuthiyyah Raafidhwah. Wameshambuliwa kwenye manyumba yao, Misikiti yao na kwenye vijia ni kitu ambacho tumekisema mara nyingi kuwaambia serikali na wengine. ---------------- (1) Muhammad B. Jammaal.

Miongoni mwa maneno yake[1] pia anasema:

“Watu wako katika huzuni wakati wao wako katika furaha.”

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba si kweli. Maneno haya ni uongo. Anayetangamana na sisi anajua hili. Tufurahie nini? Tufurahie ndugu zetu, dada zetu, wavulana wenu na wasichana wetu Dammaaj? Tufurahie nini? Wavulana na wasichana wa Waislamu ambao wameshambuliwa katika manyumba yao? Tufurahie damu isiyokuwa na hatia na safi kumwagwa? Tufurahie manyumba kubomolewa? Tufurahie watu wanaotishwa na kupigwa? Ninaapa kwa Allaah ya kwamba lau tutafurahia hayo basi kutakuwa hakuna kheri yoyote kwetu.

Tulikuwa Sanaa´ wiki ya kwanza wakati vita ya mwisho ilipopamba moto. Ilikuwa katika saa ya mwisho wakati wa Ijumaa. Niliona jinsi kila Shaykh amekaa kwenye kona na akimlilia Allaah (´Azza wa Jalla) afariji Dammaaj. Si wewe, B. Jamaal, al-Hajuuriy wala mtu mwingine anajua hilo. Allaah ndiye Anajua hilo. Tulikuwepo pale. Kila mmoja anamuomba Allaah na kuwaamrisha wengine waliokuwa nje wamuombe Allaah juu ya ndugu zao. Tunafurahia? Mche Allaah! Huu ni uongo unawazushia ndugu zako na unawadhulumu na unawatuhumu ya kwamba wanafurahia. Hakuna furaha. Sisi tunajua ya kwamba watu wa Dammaaj wamefanyiwa uadui na uasi na Huuthiyyah Raafidhwah. Wameshambuliwa kwenye manyumba yao, Misikiti yao na kwenye vijia ni kitu ambacho tumekisema mara nyingi kuwaambia serikali na wengine.

—————-
(1) Muhammad B. Jammaal.