Tukinyamaza Sote, Watu Watajua Haki Ni Ipi?

´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy: Sisi tunapoongelea kundi lolote, hatunukuu ila kutoka kwenye vitabu vyao - In Shaa Allaah. Makosa tunayatoa kwenye mihadhara yao, mawaidha yao na kwenye vitabu vyao. Yule mwenye kunukuu kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh, ananukuu kutoka kwenye vitabu vyao kwa dalili. Yule mwenye kunukuu kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun sawa ikiwa ni kundi au mtu binafsi, ananukuu kutoka kwenye vitabu vyao. Salafiyyuun ndio bora katika hili, wala hutowakuta wakifanya ghushi, wakisema uongo, wakizusha, sawa ikiwa ni Ibn Taymiyyah, Ibn ´Abdil-Wahhaab au wale waliofuata Manhaj yao. Isipokuwa Ahl-ul-Bid´ah ndio wenye tabia hii. Wao ni kweli yatakiwa kuthibitisha maneno yao kwanza (kabla ya kuyafanyia kazi), kwa kuwa maneno yao mara nyingi wakuta yana uongo, na yale wanayoyanukuu wanayabadili kama wanavyotaka wao. Vitabu hivi hapa vya Salafiyyah katika kila zama na kila mahala, hata katika wakati wetu huu yule mwenye kupambana na Ahl-ul-Bid´ah anajadiliana nao mjadala wa kielimu na dalili mpaka kosa lake libainike wazi. Sisi tunaita vipote hivi wajumuike juu ya Qur-aa na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye itathibiti upotevu wake, basi ni wajibu kubainisha upotevu wake na makosa alionayo, ili watu wajue uhakika wa aliomo (upotevu)wajiepushe na mtu huyo, au kwa yule mwenye kuwafikishwa na Allaah ajirudi na kuchukua njia ya sawa. Huu ni katika wajibu wa kutoa nasaha na ni wajibu kubainisha hilo, na Allaah Amechukua ahadi kutoka kwa Ahl-ul-Kitaab wawabainishie watu (haki) na wala wasinyamaze. Sisi tunaona watu wengi wa Bid´ah bila kujali kundi lolote lile, hawataki kukubali (upotevu) waliomo. Kwa hivyo, ndio maana tunaona ni wajibu wetu kubainisha batili hii, na wakati huo huo tunawapa nasaha watu kushikamana na haki aliyoiweka Allaah katika Shari´ah na Akawakalifisha kwayo waifuate. Wanachuoni wanatakiwa wawe imara katika hili. Na hivi hapa vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah vimejaa kwenye Maktabah, vyote vimebainisha na kuiweka wazi haki na kuiponda batili. Na nataraji tutafuata Manhaj ya mtu huyu katika kupambana nakupigana vita na shari na Bid´ah, kwa kuwa watu hawajui waliomo. Kila kundi linaona lenyewe ndio liko katika haki, hivyo watu wengi wanafuata njia hii potevu, huku wakiona kuwa ndio njia sahihi ya Kiislamu ifikishayo Peponi. Lakini mkiwabainishia ya kwamba wako katika makosa na upotevu - na mtu huyo anataka haki - bila shaka atarejea na kufuata Njia sahihi Anayoiridhia Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala). Tunamuomba Allaah Tawfiyq na tunamuomba Allaah Awawafikishe wanachuoni wasimame kwa wajibu huu mpaka watu wastafidi. Atapoongelea mwanachuoni mmoja tu (masuala haya) haitoshelezi, na wanachuoni wengi hawashiriki katika wajibu huu (wa kupiga Radd vipote potevu), bila ya shaka haki itakuja kuteketea. Haya aliyosema (Shaykh Ibn ´Uthaymiyn) ni nasaha kutoka kwa Shaykh wetu na wanachuoni wetu ya kwamba vijana leo wako huku na kule, imefikia kiasi kwamba vijana wetu wengi wa Salafiy wanafuata njia za Ahl-ul-Bid´ah, kwa kuwa wanakosa ubainisho wa kutosheleza kwa yale waliomo Ahl-ul-Bi´dah ya upotevu ambayo ni wajibu kujiepusha nayo. Wala hawapati ubainisho wa kutosheleza kuhusu ni ipi haki na Manhaj ya Salafiyyah, ili waweza kushikamana nayo imara. Wengi katika Salafiy wanapotea, kwa kuwa hatuwalei kwa Manhaj kama ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na tukawaambia "Hii ndio haki na hii ndio batili." Ni wajibu wetu kuwabainishia vijana haki. Ni Madu´aat (walinganiaji) wangapi leo ni waongo, wanawaambia watu shikamaneni na upotevu, analingania katika njia ya Khawaarij na kukufurisha Ummah mzima na kushambulia Misikiti yao, kisha haitoshi, wakuta ana rai za Ki-Jahmiyyah, Mu´tazilah, Khawaarij, Rawaafidhw (Mashia) katika vitabu vya mtu huyu. Vipi tutamfanya mtu huyu kuwa Kiongozi na Mujaddid, [... sauti haiko wazi...], na watu wataacha Manhaj ya Salafiy. Na Allaah Kaiita Qur-aan hii kuwa ni Furqaan, kwa kuwa inapambanua baina ya haki na batili. Na Mtume Muhammad (´alayhis-Salaam) alifarakanisha baina ya watu kiasi kikubwa. Ni wajibu kwa warithi wake wawe ni wafarakanishi baina ya watu, na tufarakanishe baina ya aliye na haki na mkosevu. Na kwa hili wamepotea vijana wetu. Imekuwa huyu ni Tabliyghiy na huyu Ikhwaaniy, na wakati huo huo anadai anafuata Manhaj ya Salafiy. Kwa nini yawa hivyo? Ndio, ni kwa sababu hatuwabainishii vijana wa Ki-Salafiy washikamane nayo (Manhaj hii) kwa magego yao na kuwaambia hii ndio haki, na kuwaambia wahadhari kwa waliomo vipote hivi. Hii ni haki ni wajibu tuiseme, na tunamuomba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atuwafikishe sote kushikamana bara bara na haki, na tupambanue baina ya haki na batili, na tupambanue baina ya aliye katika haki na mkosevu na mtu Sunniy na Mubtadi´ah. Vinginevyo watapotea vijana na watafuata kila mpotevu. Tunamuomba Allaah Tawfiyq. Muhadhara uliotoa Shaykh Ibn ´Uthaymiyn na Shaykh Rabiy´ Chanzo: http://youtu.be/QdeuQf48KFM

´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:

Sisi tunapoongelea kundi lolote, hatunukuu ila kutoka kwenye vitabu vyao – In Shaa Allaah. Makosa tunayatoa kwenye mihadhara yao, mawaidha yao na kwenye vitabu vyao. Yule mwenye kunukuu kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh, ananukuu kutoka kwenye vitabu vyao kwa dalili. Yule mwenye kunukuu kuhusu al-Ikhwaan al-Muslimuun sawa ikiwa ni kundi au mtu binafsi, ananukuu kutoka kwenye vitabu vyao.

Salafiyyuun ndio bora katika hili, wala hutowakuta wakifanya ghushi, wakisema uongo, wakizusha, sawa ikiwa ni Ibn Taymiyyah, Ibn ´Abdil-Wahhaab au wale waliofuata Manhaj yao. Isipokuwa Ahl-ul-Bid´ah ndio wenye tabia hii. Wao ni kweli yatakiwa kuthibitisha maneno yao kwanza (kabla ya kuyafanyia kazi), kwa kuwa maneno yao mara nyingi wakuta yana uongo, na yale wanayoyanukuu wanayabadili kama wanavyotaka wao. Vitabu hivi hapa vya Salafiyyah katika kila zama na kila mahala, hata katika wakati wetu huu yule mwenye kupambana na Ahl-ul-Bid´ah anajadiliana nao mjadala wa kielimu na dalili mpaka kosa lake libainike wazi.

Sisi tunaita vipote hivi wajumuike juu ya Qur-aa na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye itathibiti upotevu wake, basi ni wajibu kubainisha upotevu wake na makosa alionayo, ili watu wajue uhakika wa aliomo (upotevu)wajiepushe na mtu huyo, au kwa yule mwenye kuwafikishwa na Allaah ajirudi na kuchukua njia ya sawa. Huu ni katika wajibu wa kutoa nasaha na ni wajibu kubainisha hilo, na Allaah Amechukua ahadi kutoka kwa Ahl-ul-Kitaab wawabainishie watu (haki) na wala wasinyamaze.

Sisi tunaona watu wengi wa Bid´ah bila kujali kundi lolote lile, hawataki kukubali (upotevu) waliomo. Kwa hivyo, ndio maana tunaona ni wajibu wetu kubainisha batili hii, na wakati huo huo tunawapa nasaha watu kushikamana na haki aliyoiweka Allaah katika Shari´ah na Akawakalifisha kwayo waifuate.

Wanachuoni wanatakiwa wawe imara katika hili. Na hivi hapa vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah vimejaa kwenye Maktabah, vyote vimebainisha na kuiweka wazi haki na kuiponda batili. Na nataraji tutafuata Manhaj ya mtu huyu katika kupambana nakupigana vita na shari na Bid´ah, kwa kuwa watu hawajui waliomo. Kila kundi linaona lenyewe ndio liko katika haki, hivyo watu wengi wanafuata njia hii potevu, huku wakiona kuwa ndio njia sahihi ya Kiislamu ifikishayo Peponi. Lakini mkiwabainishia ya kwamba wako katika makosa na upotevu – na mtu huyo anataka haki – bila shaka atarejea na kufuata Njia sahihi Anayoiridhia Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).
Tunamuomba Allaah Tawfiyq na tunamuomba Allaah Awawafikishe wanachuoni wasimame kwa wajibu huu mpaka watu wastafidi. Atapoongelea mwanachuoni mmoja tu (masuala haya) haitoshelezi, na wanachuoni wengi hawashiriki katika wajibu huu (wa kupiga Radd vipote potevu), bila ya shaka haki itakuja kuteketea. Haya aliyosema (Shaykh Ibn ´Uthaymiyn) ni nasaha kutoka kwa Shaykh wetu na wanachuoni wetu ya kwamba vijana leo wako huku na kule, imefikia kiasi kwamba vijana wetu wengi wa Salafiy wanafuata njia za Ahl-ul-Bid´ah, kwa kuwa wanakosa ubainisho wa kutosheleza kwa yale waliomo Ahl-ul-Bi´dah ya upotevu ambayo ni wajibu kujiepusha nayo. Wala hawapati ubainisho wa kutosheleza kuhusu ni ipi haki na Manhaj ya Salafiyyah, ili waweza kushikamana nayo imara. Wengi katika Salafiy wanapotea, kwa kuwa hatuwalei kwa Manhaj kama ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na tukawaambia “Hii ndio haki na hii ndio batili.” Ni wajibu wetu kuwabainishia vijana haki.

Ni Madu´aat (walinganiaji) wangapi leo ni waongo, wanawaambia watu shikamaneni na upotevu, analingania katika njia ya Khawaarij na kukufurisha Ummah mzima na kushambulia Misikiti yao, kisha haitoshi, wakuta ana rai za Ki-Jahmiyyah, Mu´tazilah, Khawaarij, Rawaafidhw (Mashia) katika vitabu vya mtu huyu. Vipi tutamfanya mtu huyu kuwa Kiongozi na Mujaddid, [… sauti haiko wazi…], na watu wataacha Manhaj ya Salafiy. Na Allaah Kaiita Qur-aan hii kuwa ni Furqaan, kwa kuwa inapambanua baina ya haki na batili. Na Mtume Muhammad (´alayhis-Salaam) alifarakanisha baina ya watu kiasi kikubwa.

Ni wajibu kwa warithi wake wawe ni wafarakanishi baina ya watu, na tufarakanishe baina ya aliye na haki na mkosevu. Na kwa hili wamepotea vijana wetu. Imekuwa huyu ni Tabliyghiy na huyu Ikhwaaniy, na wakati huo huo anadai anafuata Manhaj ya Salafiy. Kwa nini yawa hivyo? Ndio, ni kwa sababu hatuwabainishii vijana wa Ki-Salafiy washikamane nayo (Manhaj hii) kwa magego yao na kuwaambia hii ndio haki, na kuwaambia wahadhari kwa waliomo vipote hivi. Hii ni haki ni wajibu tuiseme, na tunamuomba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atuwafikishe sote kushikamana bara bara na haki, na tupambanue baina ya haki na batili, na tupambanue baina ya aliye katika haki na mkosevu na mtu Sunniy na Mubtadi´ah. Vinginevyo watapotea vijana na watafuata kila mpotevu. Tunamuomba Allaah Tawfiyq.

Muhadhara uliotoa Shaykh Ibn ´Uthaymiyn na Shaykh Rabiy´
Chanzo: http://youtu.be/QdeuQf48KFM


  • Kitengo: Uncategorized , Msimamo juu ya wapinzani na mafundisho yao
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Friday 25th, October 2013