Tofauti Ya Shafaa´ah Mbele Ya Allaah Na Kati Ya Viumbe

Uombezi kwa Allaah hauwi isipokuwa kwa mwasharti mawili: 1- Allaah Ampe idhini mwenye kuombea aombee. 2- Mwenye kuombewa awe ni katika wafanya madhambi wapwekeshaji. Ama viumbe wanaweza kuombeana hata kama hakukupa idhini ya kuombea hata kama hakuridhia kuombewa anayeombewa. Anaweza kuwa anamchukia yule anayeombewa na anatamani hata kumuua, hamridhii, lakini pamoja na hivyo akakubaliwa uombezi juu yake kwa kulazimika kutokana na haja yake kwa watu, mawaziri na wasaidizi wake. Lau atakataa uombezi wao juu yake, watamkatalia. Hivyo anakuwa analazimika kuwawia mpole na kukubali uombezi wao hata kama hakuwapa idhini na hakumridhia muombewaji. Ama Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakuna yeyote anayeombea Kwake isipokuwa kwa idhini Yake kwanza, na wala haombewi Kwake isipokuwa katika Ahl-ut-Tawhiyd, walofanya madhambi katika wapwekeshaji. Hii ndio tofauti kati ya Shafaa´ah hizi mbili (kwa Allaah na kwa viumbe). Uombezi mbele ya Allaah ni haki kwa sharti hizi mbili na ndio uombezi sahihi (unaokubaliwa). Ama uombezi wenye kukataliwa ni uombezi (kuwaombea) makafiri au uombezi unaokuwa pasina idhini ya Allaah. Uombezi uko aina mbil – kama walivyosema wanachuoni: 1- Uombezi sahihi (unaokubaliwa). 2- Uombezi unaokataliwa: فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ “Basi hautowafaa uombezi wa waombezi wowote.” (al-Muddaththir:48) مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ “Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa.” (Ghaafir:18) Anaweza kuja mtu na kusema: “Uombezi haukubaliwi (hakuna) kutokana na dalili hizi mbili”. Mwambie kuna Aayah zinazotolea dalili kwa kukubaliwa kwa uombezi. Kwa mfano Kauli Yake (Ta´ala): مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ “Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake.” (al-Baqarah:255) وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ “Na wala hawamuombei shafaa’ah (yeyote yule) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia.” (al-Anbiyaa:28) وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ “Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote shafaa’ah yao (uombezi) isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametolea idhini kwa Amtakaye na kumridhia.” (an-Najm:26) Ni dalili zinaonesha kukubaliwa kwa uombezi kwa masharti haya mawili: a) Kwa idhini ya Allaah. b) Allaah Aridhie juu ya muombewaji. Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy Chanzo: al-Haaiyyah Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: "Sharh al-Haaiyyah", uk. 174-175

Uombezi kwa Allaah hauwi isipokuwa kwa mwasharti mawili:

1- Allaah Ampe idhini mwenye kuombea aombee.
2- Mwenye kuombewa awe ni katika wafanya madhambi wapwekeshaji.

Ama viumbe wanaweza kuombeana hata kama hakukupa idhini ya kuombea hata kama hakuridhia kuombewa anayeombewa. Anaweza kuwa anamchukia yule anayeombewa na anatamani hata kumuua, hamridhii, lakini pamoja na hivyo akakubaliwa uombezi juu yake kwa kulazimika kutokana na haja yake kwa watu, mawaziri na wasaidizi wake. Lau atakataa uombezi wao juu yake, watamkatalia. Hivyo anakuwa analazimika kuwawia mpole na kukubali uombezi wao hata kama hakuwapa idhini na hakumridhia muombewaji.

Ama Allaah (Jalla wa ´Alaa) hakuna yeyote anayeombea Kwake isipokuwa kwa idhini Yake kwanza, na wala haombewi Kwake isipokuwa katika Ahl-ut-Tawhiyd, walofanya madhambi katika wapwekeshaji. Hii ndio tofauti kati ya Shafaa´ah hizi mbili (kwa Allaah na kwa viumbe).

Uombezi mbele ya Allaah ni haki kwa sharti hizi mbili na ndio uombezi sahihi (unaokubaliwa). Ama uombezi wenye kukataliwa ni uombezi (kuwaombea) makafiri au uombezi unaokuwa pasina idhini ya Allaah. Uombezi uko aina mbil – kama walivyosema wanachuoni:

1- Uombezi sahihi (unaokubaliwa).
2- Uombezi unaokataliwa:

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ
“Basi hautowafaa uombezi wa waombezi wowote.” (al-Muddaththir:48)

مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ
“Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, na wala mwombezi anayetiiwa.” (Ghaafir:18)

Anaweza kuja mtu na kusema: “Uombezi haukubaliwi (hakuna) kutokana na dalili hizi mbili”. Mwambie kuna Aayah zinazotolea dalili kwa kukubaliwa kwa uombezi. Kwa mfano Kauli Yake (Ta´ala):

مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ
“Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake.” (al-Baqarah:255)

وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ
“Na wala hawamuombei shafaa’ah (yeyote yule) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia.” (al-Anbiyaa:28)

وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ
“Na Malaika wangapi mbinguni haitowafaa kitu chochote shafaa’ah yao (uombezi) isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametolea idhini kwa Amtakaye na kumridhia.” (an-Najm:26)

Ni dalili zinaonesha kukubaliwa kwa uombezi kwa masharti haya mawili:

a) Kwa idhini ya Allaah.
b) Allaah Aridhie juu ya muombewaji.

Mwandishi: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Daawuud as-Sijistaaniy
Chanzo: al-Haaiyyah
Mshereheshaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: “Sharh al-Haaiyyah”, uk. 174-175


  • Kitengo: Uncategorized , Aakhirah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 22nd, February 2014