Tofauti Ya Elimu Na Maarifa

Ni ipi tofauti kati ya elimu na maarifa? Kwa nini Shaykh amefasiri elimu kwa maarifa? Maarifa (ni neno) lililoenea zaidi kuliko elimu. Elimu ni jambo maalum ambalo halikutanguliwa na ujinga. Kwa haki ya Allaah kunatumiwa (neno) Elimu. Hakutumiwi maarifa juu ya haki ya Allaah. Kwa kuwa maarifa yametanguliwa na ujinga, bi maana ni uwezo uliyochumwa baada ya kutokuwepo. Hivyo kwa nisba yetu kunasemwa elimu na maarifa. Kwa haki ya Allaah (Ta´ala) kunasemwa Elimu tu. Kwa ajili hiyo ndio maana amefasiri elimu kwa maarifa wakati aliposema kuwa, makusudio ya elimu ni kumjua Allaah kwa Majina na Sifa Zake, kumjua Allaah kwa Utukufu na neema Zake na kumjua Allaah kwa Aayah Zake zinazosomwa na Aayah Zake za kilimwengu. Maarifa ambayo yatawajibisha kumpenda (Subhanaahu wa Ta´ala). Maarifa ambayo yatawajibisha kumuogopa, kumuadhimisha, kuadhimisha maamrisho Yake na kuadhimisha Shari´ah Yake. Maarifa ambayo yatawajibisha kujua kuwa Allaah Anakuona na kumkhofu. Mwisho wake iwe mepenzi kwa kuwa kumpenda Allaah (Ta´ala) ndio roho ya imani. Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 05-06 Toleo la: 24-05-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Ni ipi tofauti kati ya elimu na maarifa? Kwa nini Shaykh amefasiri elimu kwa maarifa? Maarifa (ni neno) lililoenea zaidi kuliko elimu. Elimu ni jambo maalum ambalo halikutanguliwa na ujinga. Kwa haki ya Allaah kunatumiwa (neno) Elimu. Hakutumiwi maarifa juu ya haki ya Allaah. Kwa kuwa maarifa yametanguliwa na ujinga, bi maana ni uwezo uliyochumwa baada ya kutokuwepo. Hivyo kwa nisba yetu kunasemwa elimu na maarifa. Kwa haki ya Allaah (Ta´ala) kunasemwa Elimu tu. Kwa ajili hiyo ndio maana amefasiri elimu kwa maarifa wakati aliposema kuwa, makusudio ya elimu ni kumjua Allaah kwa Majina na Sifa Zake, kumjua Allaah kwa Utukufu na neema Zake na kumjua Allaah kwa Aayah Zake zinazosomwa na Aayah Zake za kilimwengu. Maarifa ambayo yatawajibisha kumpenda (Subhanaahu wa Ta´ala). Maarifa ambayo yatawajibisha kumuogopa, kumuadhimisha, kuadhimisha maamrisho Yake na kuadhimisha Shari´ah Yake. Maarifa ambayo yatawajibisha kujua kuwa Allaah Anakuona na kumkhofu. Mwisho wake iwe mepenzi kwa kuwa kumpenda Allaah (Ta´ala) ndio roho ya imani.

Mwandishi: ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
Chanzo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 05-06
Toleo la: 24-05-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Elimu (Ujuzi) wa Allaah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 24th, May 2014