Tawhiyd Inavyopuuzwa Leo

´Allaamah al-Jaamiy: Huu ubabaishaji wametumbukia humo wengi wanaodai wana elimu. Wameichukua Dini kuwa Bid´ah, wameichukua Tawhiyd ambayo ni kumpwekesha Allaah na ´Ibaadah kuwa ni Bid´ah, wanasema Dini mpya. Imetoka Hijaaz (Saudi Arabia). Hawa watu ndo wamekuja na hii Dini mpya na Tawhiyd mpya ni Bid´ah. Waislamu wa mwanzo walikuwa hawafahamu hilo. Wanaposikia hivi watu wasiokuwa na elimu, "Waislamu wa mwanzo", wanahesabu Maswahabah, Taabi´iyn na waliombele yao. Waislamu wa mwanzo, watu wa Ikhlaasw, watu wa Tawhiyd; lakini Shirki hii wameanguka humo Waislamu wa mwisho [waliokuja baadaye]. Na huu ni katika ubabaishaji na utatizi kwa watu. Wanawaharibia watu kwa kuwaelekeza kwenye haya makaburi na kuwakataza watu kwa ´Ibaadah ya Dini mpya [ambayo ni ya Tawhiyd]. Mara ngapi utatizi huu umeleta madhara kwa watu wasiokuwa na elimu, na kuwapoteza? Hii sio Dini mpya bali ndio Dini ya tangu zamani aliyokuja nayo Muhammad Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio dalili ya neno ambalo umelihifadhi "ash-Hadu anlaa ilaaha illa Allaah" isipokuwa ni kwa kuwa hufahamu maana yake. Na unawakataza wanaoilingania, makatazo makubwa. Na huenda hata ukawakufurisha [wanaoilingania].

´Allaamah al-Jaamiy:

Huu ubabaishaji wametumbukia humo wengi wanaodai wana elimu. Wameichukua Dini kuwa Bid´ah, wameichukua Tawhiyd ambayo ni kumpwekesha Allaah na ´Ibaadah kuwa ni Bid´ah, wanasema Dini mpya. Imetoka Hijaaz (Saudi Arabia). Hawa watu ndo wamekuja na hii Dini mpya na Tawhiyd mpya ni Bid´ah. Waislamu wa mwanzo walikuwa hawafahamu hilo. Wanaposikia hivi watu wasiokuwa na elimu, “Waislamu wa mwanzo”, wanahesabu Maswahabah, Taabi´iyn na waliombele yao. Waislamu wa mwanzo, watu wa Ikhlaasw, watu wa Tawhiyd; lakini Shirki hii wameanguka humo Waislamu wa mwisho [waliokuja baadaye]. Na huu ni katika ubabaishaji na utatizi kwa watu. Wanawaharibia watu kwa kuwaelekeza kwenye haya makaburi na kuwakataza watu kwa ´Ibaadah ya Dini mpya [ambayo ni ya Tawhiyd]. Mara ngapi utatizi huu umeleta madhara kwa watu wasiokuwa na elimu, na kuwapoteza? Hii sio Dini mpya bali ndio Dini ya tangu zamani aliyokuja nayo Muhammad Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ndio dalili ya neno ambalo umelihifadhi “ash-Hadu anlaa ilaaha illa Allaah” isipokuwa ni kwa kuwa hufahamu maana yake. Na unawakataza wanaoilingania, makatazo makubwa. Na huenda hata ukawakufurisha [wanaoilingania].