Soko Ambayo Kila Mmoja Ataiingia

Mwezi huu mtukufu una kheri nyingi na neema kubwa. Allaah Ameutofautisha kati ya miezi mingine na kuufanya kuwa maalum kwa fadhila zisizohesabika. Mwezi huu bila ya shaka ni soko katika masoko ya Aakhirah. Kila mmoja ataingia katika mwezi huu. Ni soko. Wataingia sawa wakipenda hilo au wasipende. Hata hivyo kuna ambao wamezifungamanisha nyoyo zao na Aakhirah. Wanatumia fursa hii na kuhifadhi muda wao ambapo ndani yake wanafanya matendo ya kheri na kujiepusha na ya haramu. Wanajiandaa kukutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) jambo ambalo liko karibu: وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ “Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.” (03:185) Ni adimu. Mtu kama huyu ndio mwenye kuwafikishwa. Amenufaika na mwezi huu na fadhila zake. Maisha yake ni kheri kwake. Kuna watu wanaoingia katika mwezi na soko hili likubwa pasina kunufaika na lolote. Wanatoka kama jinsi walivyoingia – pasina faida yoyote. Huku ni kunyimwa pasina shaka. Mtu ndio mwenye kujichaguliwa mwenyewe ima kuwa katika wale ambao wanapigania Aakhirah na akafaidika na misimu yake kama mwezi huu na mingine, au kuwa katika wale ambao wanapigania dunia na haufungamanishi moyo wake na Aakhirah. Anachojali tu ni dunia. Anaikusanya na kuikimbilia. Anatilia nguvu nyingi katika kuitafuta. Hatimae anaiwaachia wengine na anaenda akiwa hana lolote. Hii ndio khasara ya wazi.

Mwezi huu mtukufu una kheri nyingi na neema kubwa. Allaah Ameutofautisha kati ya miezi mingine na kuufanya kuwa maalum kwa fadhila zisizohesabika. Mwezi huu bila ya shaka ni soko katika masoko ya Aakhirah. Kila mmoja ataingia katika mwezi huu. Ni soko. Wataingia sawa wakipenda hilo au wasipende. Hata hivyo kuna ambao wamezifungamanisha nyoyo zao na Aakhirah. Wanatumia fursa hii na kuhifadhi muda wao ambapo ndani yake wanafanya matendo ya kheri na kujiepusha na ya haramu. Wanajiandaa kukutana na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) jambo ambalo liko karibu:

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ
“Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.” (03:185)

Ni adimu.

Mtu kama huyu ndio mwenye kuwafikishwa. Amenufaika na mwezi huu na fadhila zake. Maisha yake ni kheri kwake.

Kuna watu wanaoingia katika mwezi na soko hili likubwa pasina kunufaika na lolote. Wanatoka kama jinsi walivyoingia – pasina faida yoyote. Huku ni kunyimwa pasina shaka. Mtu ndio mwenye kujichaguliwa mwenyewe ima kuwa katika wale ambao wanapigania Aakhirah na akafaidika na misimu yake kama mwezi huu na mingine, au kuwa katika wale ambao wanapigania dunia na haufungamanishi moyo wake na Aakhirah. Anachojali tu ni dunia. Anaikusanya na kuikimbilia. Anatilia nguvu nyingi katika kuitafuta. Hatimae anaiwaachia wengine na anaenda akiwa hana lolote. Hii ndio khasara ya wazi.