Sijui – Ni Nusu Ya Elimu

Kama mwalimu anaulizwa juu ya suala na akashindwa kulijibu aseme kuwa hajui. Ni katika elimu kusema kuwa hajui. Baadhi wamesema kuwa neno "Sijui" ni nusu ya elimu. Imesemekana kuwa mwalimu anatakiwa kuwafunza wanafunzi wake kusema ya kwamba hajui kwa sababu yeye mwenyewe anasema hilo mara nyingi. Muhammad bin ´Abdil-Hakam amesema: "Nilimuuliza ash-Shaafi´iy kuhusu Mut´ah na kama mtu anaweza kuachika katika ndoa kama hii, kama mtu anarithi, kama matumizi ni wajibu na kama ni lazima ishuhudiwe. Akasema: "Wallaahi sijui." Shikamana na elimu yako ya kwamba manzilah ya mtu haiteremki kwa mtu kusema kuwa hajui. Wale wanaomdharau mtu kama huyu ni baadhi ya watu wajinga. Kusema hivyo kunamnyanyua mtu na kuthibitisha manzilah yake kubwa, mtu wa Dini ya nguvu, mchaji Allaah, moyo msafi, elimu kamilifu na tabia nzuri. Tumepokea kutoka kwa baadhi ya Salaf juu ya maana yake. Mtu ambaye anaona fakhari kutosema kuwa hajui ni mtu mwenye Dini dhaifu na kutokuwa na elimu. Anaogopa wasikilizaji wasipoteze heshima kwake. Hili linathibitisha ujinga wake na Dini yake nyembamba. Kuna khatari kosa lake likaenea kati ya watu na akatumbukia katika yale aliyotaka kuepuka na akawa maarufu kwa yale aliyokuwa anaogopa.

Kama mwalimu anaulizwa juu ya suala na akashindwa kulijibu aseme kuwa hajui. Ni katika elimu kusema kuwa hajui. Baadhi wamesema kuwa neno “Sijui” ni nusu ya elimu. Imesemekana kuwa mwalimu anatakiwa kuwafunza wanafunzi wake kusema ya kwamba hajui kwa sababu yeye mwenyewe anasema hilo mara nyingi. Muhammad bin ´Abdil-Hakam amesema:

“Nilimuuliza ash-Shaafi´iy kuhusu Mut´ah na kama mtu anaweza kuachika katika ndoa kama hii, kama mtu anarithi, kama matumizi ni wajibu na kama ni lazima ishuhudiwe. Akasema: “Wallaahi sijui.”

Shikamana na elimu yako ya kwamba manzilah ya mtu haiteremki kwa mtu kusema kuwa hajui. Wale wanaomdharau mtu kama huyu ni baadhi ya watu wajinga. Kusema hivyo kunamnyanyua mtu na kuthibitisha manzilah yake kubwa, mtu wa Dini ya nguvu, mchaji Allaah, moyo msafi, elimu kamilifu na tabia nzuri. Tumepokea kutoka kwa baadhi ya Salaf juu ya maana yake.

Mtu ambaye anaona fakhari kutosema kuwa hajui ni mtu mwenye Dini dhaifu na kutokuwa na elimu. Anaogopa wasikilizaji wasipoteze heshima kwake. Hili linathibitisha ujinga wake na Dini yake nyembamba. Kuna khatari kosa lake likaenea kati ya watu na akatumbukia katika yale aliyotaka kuepuka na akawa maarufu kwa yale aliyokuwa anaogopa.


  • Author: Imaam Badr-ud-Diyn Muhammad bin Ibraahiym bin Jamaa´ah al-Hamawiy (d. 733). Tadhkirat-us-Saami´ wal-Mutakallim fiy Adab-il-´Aalim wal-Muta´allim, uk. 47-48
  • Kitengo: Uncategorized , Da´wah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 23rd, January 2014