Sijda Ya Kusahau Kwenye Swalah (2)

Swali: Akiswali Imamu Rakaa mbili za ´Aswr, kisha akakumbushwa kama amesahau Rakaa mbili, akakhofia ikiwa atasujudu (Sijda ya kusahau) baada ya kutoa Salaam atawachanganya, akawaambia maamuma "Ntaswali Rakaa mbili, kisha nitoe Salaam, kisha nilete Sijda ya kusahau kisha nitoe Salaam (tena). Imaam Ibn Baaz: Hapana asiwaambie (haina haja), atatoa Salaam tu kwani ndo Sunnah. Atatoa Salaam kisha asujudu Sijda ya kusahau, kisha awafunze kuwa hii ndo Sunnah. Muulizaji: Vipi ikiwa atasujudu (Sijda ya kusahau) kabla ya kutoa Salaam? Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya anaweza kufanya hivyo. Muulizaji: Ikiwa kasahau kuleta Sijda ya kusahau baada ya muda, atarudi kuswali upya au... Imaam Ibn Baaz: Hapana, atasujudu Sijda ya kusahau atapokumbuka. Muulizaji: Hata kama muda mrefu umeshapita? Imaam Ibn Baaz: Hata kama muda mrefu umeshapita. Muulizaji: Vipi ikiwa ni baada ya siku mbili ? Imaam Ibn Baaz: Hata kama zimepita siku mbili. Baadhi yao huanza Swalah upya, lazima bora zaidi alete Sijda ya kusahau hata kama.

Swali:
Akiswali Imamu Rakaa mbili za ´Aswr, kisha akakumbushwa kama amesahau Rakaa mbili, akakhofia ikiwa atasujudu (Sijda ya kusahau) baada ya kutoa Salaam atawachanganya, akawaambia maamuma “Ntaswali Rakaa mbili, kisha nitoe Salaam, kisha nilete Sijda ya kusahau kisha nitoe Salaam (tena).

Imaam Ibn Baaz:
Hapana asiwaambie (haina haja), atatoa Salaam tu kwani ndo Sunnah. Atatoa Salaam kisha asujudu Sijda ya kusahau, kisha awafunze kuwa hii ndo Sunnah.

Muulizaji:
Vipi ikiwa atasujudu (Sijda ya kusahau) kabla ya kutoa Salaam?

Imaam Ibn Baaz:
Hakuna ubaya anaweza kufanya hivyo.

Muulizaji:
Ikiwa kasahau kuleta Sijda ya kusahau baada ya muda, atarudi kuswali upya au…

Imaam Ibn Baaz:
Hapana, atasujudu Sijda ya kusahau atapokumbuka.

Muulizaji:
Hata kama muda mrefu umeshapita?

Imaam Ibn Baaz:
Hata kama muda mrefu umeshapita.

Muulizaji:
Vipi ikiwa ni baada ya siku mbili ?

Imaam Ibn Baaz:
Hata kama zimepita siku mbili. Baadhi yao huanza Swalah upya, lazima bora zaidi alete Sijda ya kusahau hata kama.