Sifa Ya Kustawaa Na Kuwa Juu Kwa Allaah (´Azza wa Jalla)

Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ “Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah).” (20:05) Mna uthibitisho wa Sifa ya Kustawaa kwa Allaah (´Azza wa Jalla). al-Istiwaa inayolingana na Ukubwa na Utukufu Wake. al-Istiwaa ni Sifa ya kimatendo inayolingana na Ukubwa na Utukufu wa Allaah. Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla): أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ “Je, mnadhani mko (katika) amani na Aliyeko mbinguni (juu)... “ (67:16) Mna uthibitisho wa Sifa ya al-´Uluw, kuwa juu kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na Sifa ya Kustawaa vikiwa pamoja kwa kuwa Allaah (´Azza wa Jalla) Yuko juu ya mbingu Zake, yaani Yuko juu ya mbingu Zake juu ya ´Arshi Yake Kustawaa kustawaa ambako kunalingana na Ukubwa na Utukufu Wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mola Wetu ni Allaah Aliye juu ya mbingu, Limetakasika Jina Lako.” Kauli yake: “Mola Wetu ni Allaah Aliye juu ya mbingu” yaani al-´Uluw, juu. Neno “as-Samaa´” (mbingu) husemwa kwa kukusudia: 1- Kitu kuwa juu. 2- Mbingu zinazojulikana. Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=882&size=2h&ext=.rm

Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
“Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah).” (20:05)

Mna uthibitisho wa Sifa ya Kustawaa kwa Allaah (´Azza wa Jalla). al-Istiwaa inayolingana na Ukubwa na Utukufu Wake. al-Istiwaa ni Sifa ya kimatendo inayolingana na Ukubwa na Utukufu wa Allaah. Kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ
“Je, mnadhani mko (katika) amani na Aliyeko mbinguni (juu)… “ (67:16)

Mna uthibitisho wa Sifa ya al-´Uluw, kuwa juu kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na Sifa ya Kustawaa vikiwa pamoja kwa kuwa Allaah (´Azza wa Jalla) Yuko juu ya mbingu Zake, yaani Yuko juu ya mbingu Zake juu ya ´Arshi Yake Kustawaa kustawaa ambako kunalingana na Ukubwa na Utukufu Wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola Wetu ni Allaah Aliye juu ya mbingu, Limetakasika Jina Lako.”

Kauli yake:

“Mola Wetu ni Allaah Aliye juu ya mbingu”

yaani al-´Uluw, juu. Neno “as-Samaa´” (mbingu) husemwa kwa kukusudia:

1- Kitu kuwa juu.
2- Mbingu zinazojulikana.

Mwandishi: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn Ibn Qudaamah al-Maqdisiy
Chanzo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad
Mshereheshaji: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Marejeleo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=882&size=2h&ext=.rm


  • Kitengo: Uncategorized , Kulingana juu ya ´Arshi
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 2nd, April 2014