Sifa Nzuri Baada Ya Chakula

391 - Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu akila chakula, asifute mkono wake mpaka aurambe mkono wake au arambwe au kutoa sahani kabla ya kuliramba au likarambwa. Katika kile chakula cha mwisho kuna baraka." Ameipokea an-Nasaa'iy katika "as-Sunan al-Kubraa." (6736). Katika Hadiyth kuna tabia nzuri ya meza, nayo ni kuramba vidole na kukomboroza sahani kwavyo. Waislamu wengi leo hawatendei kazi hili. Wameathirika na makafiri wa Ulaya na maadili yao ambayo yamejengeka juu ya kufanyia israfu vitu na hawataki kumjua Muumba wao na kumshukuru kwa neema. Muislamu anatakiwa kuhakikisha hawafuati katika hili ili asije kuwa mmoja katika wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: "Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao." Hivyo usitumie leso katika kufuta mdomo na vidole wakati wa chakula. Sababu ya mimi kusema ya kwamba maadili haya ni wajibu, ni kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameamrisha na akakataza kuiacha. Kuwa muumini na ufuate maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na jitenge na makatazo yake. Usijali wale wanaodharau na kuzuia watu na njia ya Allaah sawa ikiwa wanajua hilo au hawajui.

391 – Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akila chakula, asifute mkono wake mpaka aurambe mkono wake au arambwe au kutoa sahani kabla ya kuliramba au likarambwa. Katika kile chakula cha mwisho kuna baraka.”

Ameipokea an-Nasaa’iy katika “as-Sunan al-Kubraa.” (6736).

Katika Hadiyth kuna tabia nzuri ya meza, nayo ni kuramba vidole na kukomboroza sahani kwavyo. Waislamu wengi leo hawatendei kazi hili. Wameathirika na makafiri wa Ulaya na maadili yao ambayo yamejengeka juu ya kufanyia israfu vitu na hawataki kumjua Muumba wao na kumshukuru kwa neema. Muislamu anatakiwa kuhakikisha hawafuati katika hili ili asije kuwa mmoja katika wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Hivyo usitumie leso katika kufuta mdomo na vidole wakati wa chakula.

Sababu ya mimi kusema ya kwamba maadili haya ni wajibu, ni kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ameamrisha na akakataza kuiacha. Kuwa muumini na ufuate maamrisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na jitenge na makatazo yake. Usijali wale wanaodharau na kuzuia watu na njia ya Allaah sawa ikiwa wanajua hilo au hawajui.


  • Author: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Silsilah al-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/746-747)
  • Kitengo: Uncategorized , Chakula
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Monday 20th, January 2014