Shubuha Zinazotumiwa Na Wale Wanaopinga Radd

Na kwa hili kuna uwajibu wa kumradi anayekwenda kinyume, kinyume na wanavyoseme baadhi ya watu acheni Ruduud, waacheni watu kila mmoja na abaki na maoni yake na heshima yake, uhuru wa maoni na maneno. Kwa haya Ummah utaangamia, kwa haya Ummah utaangamia. Salaf hawakuwanyamazia mfano wa watu kama hawa, bali waliwafedhehesha na kuwapiga Radd, kwa kujua kwao khatari yao kwa Ummah. Sisi hatuwezi kunyamaza kwa shari yao, ni lazima kwetu kubainisha yale Aliyoyateremsha Allaah. La sivyo tutakuwa wenye kuficha, wale ambao Allaah kasema kuwahusu: إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ "Hakika wale ambao wanaficha yale Tuliyoyateremsha katika Hoja zilizo wazi na Hidaaya baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani." (02:159) Jambo hili haliishii kwa Mubtadi´ah, bali linawapata pia watu wanaowanyamazia. Mwenye kuwanyamazia (watu wa Bid´ah) dhambi inampata na adhabu. Kwa kuwa ni wajibu kubainisha, kuwawekea watu wazi. Na hii ndio kazi ya Ruduud za kielimu. Ruduud za kielimu zilizoenea kwenye Maktabah za Waislamu, zote zinasafisha (upotofu) kwenda katika Njia iliyonyooka na zinatahadharisha dhidi ya watu hawa. Tusipandikizwe fikra hii; uhuru wa maoni, uhuru wa maneno, kuheshimia wengine na mengineyo. Sisi makusudio yetu sio kuwaingilia watu, makusudio yetu ni haki. Makusudio yetu sio kuwajeruhi watu na kutoa aibu za watu, makusudio yetu sisi ni kubainisha haki. Hii ni amaana Allaah Kawapa nayo wanachuoni. Haijuzu kunyamazia watu mfano wa hawa. Lakini kwa masikitiko makubwa, kunapotokea mtu akawapiga Radd mfano wa watu kama hawa, wanasema "Wewe una pupa, wewe una hili na lile, huyu hastahiki kupigwa Radd, ungemnyamazia jambo hili lisingejulikana." Na mfano wa maneno hayo ya kutia wasiwasi. Huyu hawezi kusitisha wanachuoni kubainisha kwa watu shari ya watu hawa Madu´aat wapotofu.

Na kwa hili kuna uwajibu wa kumradi anayekwenda kinyume, kinyume na wanavyoseme baadhi ya watu acheni Ruduud, waacheni watu kila mmoja na abaki na maoni yake na heshima yake, uhuru wa maoni na maneno. Kwa haya Ummah utaangamia, kwa haya Ummah utaangamia. Salaf hawakuwanyamazia mfano wa watu kama hawa, bali waliwafedhehesha na kuwapiga Radd, kwa kujua kwao khatari yao kwa Ummah.

Sisi hatuwezi kunyamaza kwa shari yao, ni lazima kwetu kubainisha yale Aliyoyateremsha Allaah. La sivyo tutakuwa wenye kuficha, wale ambao Allaah kasema kuwahusu:

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ
“Hakika wale ambao wanaficha yale Tuliyoyateremsha katika Hoja zilizo wazi na Hidaaya baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.” (02:159)

Jambo hili haliishii kwa Mubtadi´ah, bali linawapata pia watu wanaowanyamazia. Mwenye kuwanyamazia (watu wa Bid´ah) dhambi inampata na adhabu. Kwa kuwa ni wajibu kubainisha, kuwawekea watu wazi. Na hii ndio kazi ya Ruduud za kielimu. Ruduud za kielimu zilizoenea kwenye Maktabah za Waislamu, zote zinasafisha (upotofu) kwenda katika Njia iliyonyooka na zinatahadharisha dhidi ya watu hawa. Tusipandikizwe fikra hii; uhuru wa maoni, uhuru wa maneno, kuheshimia wengine na mengineyo.

Sisi makusudio yetu sio kuwaingilia watu, makusudio yetu ni haki. Makusudio yetu sio kuwajeruhi watu na kutoa aibu za watu, makusudio yetu sisi ni kubainisha haki. Hii ni amaana Allaah Kawapa nayo wanachuoni. Haijuzu kunyamazia watu mfano wa hawa.

Lakini kwa masikitiko makubwa, kunapotokea mtu akawapiga Radd mfano wa watu kama hawa, wanasema “Wewe una pupa, wewe una hili na lile, huyu hastahiki kupigwa Radd, ungemnyamazia jambo hili lisingejulikana.” Na mfano wa maneno hayo ya kutia wasiwasi. Huyu hawezi kusitisha wanachuoni kubainisha kwa watu shari ya watu hawa Madu´aat wapotofu.