Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah Kuhusu Maulidi

Hali kadhalika na kwa yale waliozua baadhi ya watu ima ili kuiga manaswara au kwa ajili ya mapenzi na kumuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Huenda Allaah Akawalipa kwa mapenzi na shughuli hii, lakini si kwa Bid´ah hii ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Isitoshe, kuna tofauti kuhusiana na tarehe sahihi [ya kuzaliwa kwake]. Jambo hili halikufanywa na Salaf, ingawa walikuwa na uwezo juu ya hilo wakati vikwazo vyake kulikuwa hakuna. Lau jambo hili lingekuwa na kheri ndani yake, au lau lingekuwa na faida nyingi kuliko khasara, basi Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa na haki zaidi juu yake kuliko sisi. Walikuwa wakimpenda Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) zaidi kuliko sisi vile vile kama ambavyo walikuwa wakimuadhimisha (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) zaidi kuliko sisi. Walikuwa na hima ya kufanya matendo mema kuliko sisi. Lakini mapenzi kamilifu na uadhimisho unapatikana katika kumfuata na kumtii, kufuata amri zake, kuhuisha Sunnah zake sawa za ndani na za dhahiri, kueneza mafunzo yake na kupigana kwa hilo kwa moyo, mkono na ulimi. Hii ndio njia ya wale Makhalifah wa kwanza katika Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema. Watu wengi katika watu hawa ambao wako na bidii ya kujishughulisha na Bid´ah hii - angalau kwa nia njema na shughuli ambayo tunatarajia watapewa ujira kwa ajili yake - ni madhaifu katika kufuata amri za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Utawapata wao ni kama yule mwenye kuipamba Qur-aan bila ya kuisoma au anaisoma lakini bila ya kuifuata. Mtu kama huyo ni kama yule anaeupamba Msikiti bila ya kuswali au anafanya hivyo mara chache. Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah Iqtidhwaa´ as-Swiraat al-Mustaqiym (2/123-124) Daar-ul-'Asimah, 1419

Hali kadhalika na kwa yale waliozua baadhi ya watu ima ili kuiga manaswara au kwa ajili ya mapenzi na kumuadhimisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Huenda Allaah Akawalipa kwa mapenzi na shughuli hii, lakini si kwa Bid´ah hii ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Isitoshe, kuna tofauti kuhusiana na tarehe sahihi [ya kuzaliwa kwake].

Jambo hili halikufanywa na Salaf, ingawa walikuwa na uwezo juu ya hilo wakati vikwazo vyake kulikuwa hakuna. Lau jambo hili lingekuwa na kheri ndani yake, au lau lingekuwa na faida nyingi kuliko khasara, basi Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa na haki zaidi juu yake kuliko sisi. Walikuwa wakimpenda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) zaidi kuliko sisi vile vile kama ambavyo walikuwa wakimuadhimisha (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) zaidi kuliko sisi. Walikuwa na hima ya kufanya matendo mema kuliko sisi.
Lakini mapenzi kamilifu na uadhimisho unapatikana katika kumfuata na kumtii, kufuata amri zake, kuhuisha Sunnah zake sawa za ndani na za dhahiri, kueneza mafunzo yake na kupigana kwa hilo kwa moyo, mkono na ulimi. Hii ndio njia ya wale Makhalifah wa kwanza katika Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema.

Watu wengi katika watu hawa ambao wako na bidii ya kujishughulisha na Bid´ah hii – angalau kwa nia njema na shughuli ambayo tunatarajia watapewa ujira kwa ajili yake – ni madhaifu katika kufuata amri za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Utawapata wao ni kama yule mwenye kuipamba Qur-aan bila ya kuisoma au anaisoma lakini bila ya kuifuata. Mtu kama huyo ni kama yule anaeupamba Msikiti bila ya kuswali au anafanya hivyo mara chache.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
Iqtidhwaa´ as-Swiraat al-Mustaqiym (2/123-124)
Daar-ul-‘Asimah, 1419


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Thursday 24th, October 2013