Shaykh Muhammad al-Madkhaliy Kuhusu Baadhi Ya Makosa Ya Ibn Jibriyn

Tulimradi Ibn Jibriyn (Rahimahu Allaah) wakati aliposema batili katika kuwasifu al-Ikhwaa al-Muslimuun na kuwasifu Jamaa´at-ut-Tabliygh na kuwatetea na kumsifu Usaamah bin Laadin na kumtetea. Hivi punde wamenieleza ndugu maneno ya ajabu sana. Lau ningelikuwa najua kuwa nitaongea leo ningeyaleta. Anamtetea al-´Alawiy al-Maalikiy. Makhurafi na waabudu makaburi anawatetea. Akasema kuwa ni mwanachuoni na kupendekeza visomwe vitabu vyake na kusema kuwa hakuna yeyote aliyetahadharisha dhidi yake pamoja na kwamba kuna miongoni mwa wanachuoni waliomfanyia Takfiyr. Fataawaa hizo zipo. Hali kadhalika al-Qaradhwaawiy. Anawatetea watu wote hawa na anasema visomwe vitabu vyake na watu wastafidi navyo. Wakati huo huo Ahmad an-Najmiy na Shaykh Rabiy´ anatahadharisha dhidi yao. Anasema Shaykh Rabiy´ sio mwanachuoni, sio katika watu wa al-Jarh wat-Ta´diyl na kwamba vitabu vyake vimejaa ujinga. Anamtetea Usaamah bin Laadin, al-´Alawiy al-Maalikiy, al-Qaraadhwaawiy, Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Sayyid Qutwub na kadhalika. Alimwambia Shaykh wetu Ahmad an-Najmiy (Rahimahu Allaah) usichapishe kitabu hichi "al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal". Hata hivyo akamradi Shaykh wetu kwa nguvu na ushujaa. Hakumuogopa na kutojali kuwa ni mwanachama wa baraza la Fatwaa. Alimradi kwa kitabu "Radd-ul-Jawaab ´alaa man talaba minniy ´Adam Tab´-il-Kitaab".

Tulimradi Ibn Jibriyn (Rahimahu Allaah) wakati aliposema batili katika kuwasifu al-Ikhwaa al-Muslimuun na kuwasifu Jamaa´at-ut-Tabliygh na kuwatetea na kumsifu Usaamah bin Laadin na kumtetea.

Hivi punde wamenieleza ndugu maneno ya ajabu sana. Lau ningelikuwa najua kuwa nitaongea leo ningeyaleta. Anamtetea al-´Alawiy al-Maalikiy. Makhurafi na waabudu makaburi anawatetea. Akasema kuwa ni mwanachuoni na kupendekeza visomwe vitabu vyake na kusema kuwa hakuna yeyote aliyetahadharisha dhidi yake pamoja na kwamba kuna miongoni mwa wanachuoni waliomfanyia Takfiyr. Fataawaa hizo zipo.

Hali kadhalika al-Qaradhwaawiy. Anawatetea watu wote hawa na anasema visomwe vitabu vyake na watu wastafidi navyo.

Wakati huo huo Ahmad an-Najmiy na Shaykh Rabiy´ anatahadharisha dhidi yao. Anasema Shaykh Rabiy´ sio mwanachuoni, sio katika watu wa al-Jarh wat-Ta´diyl na kwamba vitabu vyake vimejaa ujinga.

Anamtetea Usaamah bin Laadin, al-´Alawiy al-Maalikiy, al-Qaraadhwaawiy, Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun, Sayyid Qutwub na kadhalika.

Alimwambia Shaykh wetu Ahmad an-Najmiy (Rahimahu Allaah) usichapishe kitabu hichi “al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal”. Hata hivyo akamradi Shaykh wetu kwa nguvu na ushujaa. Hakumuogopa na kutojali kuwa ni mwanachama wa baraza la Fatwaa. Alimradi kwa kitabu “Radd-ul-Jawaab ´alaa man talaba minniy ´Adam Tab´-il-Kitaab”.