Shaykh ar-Raajhiy Kuhusu Kupiga Kura Katiba Ya Misri

Muulizaji: Karibu wiki imepita nilikupigia simu na kukuuliza kuhusiana na hukumu ya kupiga kura katiba ya Misri. Ukaahidi utabainisha suala hili. Nilikuwa napenda kuuliza kama umeshafanya? ´Allaamah ar-Raajhiy: In Shaa Allaah karibu tutaweka bayana. Ndani ya bayana kuna uharamu wa kupiga kura katiba. Kupiga kura katiba haijuzu ni Haramu. Haijuzu. Yule aliyepiga kura ni juu yale kuleta Tawbah na kuikanusha katiba hiyo na watu wake walio nyuma yake. Huu ni mukhtasari. Ni katiba ya kufuru na Twaaghuut. Haijuzu kupiga kura. Muulizaji: Baadhi yao wanadai kuwa kuna maslahi ya kupiga kura. Vipi tutapiga Radd hili? ´Allaamah ar-Raajhiy: Maslahi yako wapi? Muulizaji: Wanasema kuwa kuna maslahi ya kupatikana utulivu katika mji. Muulizaji: Wanasema kuwa kuna maslahi ya kupatikana uimara wa nnchi... ´Allaamah ar-Raajhiy: Uimara wa nchi? Nchi huwa na uimara ikiwa imejengeka juu ya kufuru? Uimara wa nchi unapatikana kwa kuhukumu kwa Shari´ah. Kwa nini kuna mapinduzi sasa? Kunasimama mapinduzi dhidi ya uongozi wa kikafiri ili uongozi mwingine wa kikafiri utawale? Faida iko wapi? Uongozi wa kwanza si afadhali ubaki tu!

Muulizaji:
Karibu wiki imepita nilikupigia simu na kukuuliza kuhusiana na hukumu ya kupiga kura katiba ya Misri. Ukaahidi utabainisha suala hili. Nilikuwa napenda kuuliza kama umeshafanya?

´Allaamah ar-Raajhiy:
In Shaa Allaah karibu tutaweka bayana. Ndani ya bayana kuna uharamu wa kupiga kura katiba. Kupiga kura katiba haijuzu ni Haramu. Haijuzu. Yule aliyepiga kura ni juu yale kuleta Tawbah na kuikanusha katiba hiyo na watu wake walio nyuma yake. Huu ni mukhtasari. Ni katiba ya kufuru na Twaaghuut. Haijuzu kupiga kura.

Muulizaji:
Baadhi yao wanadai kuwa kuna maslahi ya kupiga kura. Vipi tutapiga Radd hili?

´Allaamah ar-Raajhiy:
Maslahi yako wapi?

Muulizaji:
Wanasema kuwa kuna maslahi ya kupatikana utulivu katika mji.

Muulizaji:
Wanasema kuwa kuna maslahi ya kupatikana uimara wa nnchi…

´Allaamah ar-Raajhiy:
Uimara wa nchi? Nchi huwa na uimara ikiwa imejengeka juu ya kufuru? Uimara wa nchi unapatikana kwa kuhukumu kwa Shari´ah. Kwa nini kuna mapinduzi sasa? Kunasimama mapinduzi dhidi ya uongozi wa kikafiri ili uongozi mwingine wa kikafiri utawale? Faida iko wapi? Uongozi wa kwanza si afadhali ubaki tu!