Shaykh al-´Abbaad Akifasiri Hadiyth Ya Makatazo Ya Mwanamke Kuyatembelea Makaburi

Baadhi ya watu wanasema: "Zawwaaraat maana yake ni wale wanawake wanaokithirisha kuyatembelea makaburi. Ama mwanamke akiyatembelea na wala hakithirishi, hili halina ubaya." Hili sio sahihi. Kwa kuwa mwanamke ni dhaifu na hawezi kujizuia na ana udhaifu. Hawezi kuimiliki nafsi yake wakati wa msiba wala wakati anapoiona kaburi na kulitembelea kaburi. Kutokana na udogo wa subira yake na udhaifu wake. Kwa ajili hii ndio maana ikakatazwa. Na kauli yake: "Allaah Anawalaani zawwaaraat wanawake wanaozuru makaburi." Zawwaaraat imenasibishwa na ziara, yaani asli ya ziara (kuyatembelea) na si kukithirisha. Na hili ni kama mfano wa Kauli Yake (Ta´ala): وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ”Na Mola wako si dhalimu (hata chembe) kwa waja (Wake).” (41:46) Allaah Kakataza asli ya dhulma. Allaah (´Azza wa Jalla) Hadhulumu, Hamdhulumu yeyote na wala makusudio yake si kwamba Hakithirishi (kuchupa mipaka). Maana yake ni kwamba sio Mwenye kudhulumu. Isitoshe, kauli ya kujuzisha (wanawake kuyatembelea makaburi) na kauli ya kukataza. Mwanamke akiacha kuyatembelea makaburi, kipi ambacho kitakuwa kimempita? Hakuna kitachokuwa kimempita isipokuwa jambo lililopendekezwa tu. Jambo lililopendekezwa ndio litakuwa limempita na si kwamba atakuwa ameacha jambo la wajibu mpaka achukuliwe (aadhibiwe). Atakuwa ameacha jambo lililopendekezwa. Ama lau atayatembelea, atakuwa amejiingiza katika laana. Kwa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Allaah Amewalaani wanawake wenye kuzuru makaburi." Kwa hivyo, kauli hii (ya wanachuoni wanaokataza) ndio ilio salama kuliko ile kauli nyingine. Kwa kuwa ndani yake kuna usalama wa kujisababishia laana na adhabu. Kwa hivyo, kuyatembelea makaburi, sawa ikiwa ni kaburi la Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ya mashahidi au makaburi yoyote duniani ni kwa wanaume peke yao na si kwa wanawake.

Baadhi ya watu wanasema: “Zawwaaraat maana yake ni wale wanawake wanaokithirisha kuyatembelea makaburi. Ama mwanamke akiyatembelea na wala hakithirishi, hili halina ubaya.”

Hili sio sahihi. Kwa kuwa mwanamke ni dhaifu na hawezi kujizuia na ana udhaifu. Hawezi kuimiliki nafsi yake wakati wa msiba wala wakati anapoiona kaburi na kulitembelea kaburi. Kutokana na udogo wa subira yake na udhaifu wake. Kwa ajili hii ndio maana ikakatazwa. Na kauli yake:

“Allaah Anawalaani zawwaaraat wanawake wanaozuru makaburi.”

Zawwaaraat imenasibishwa na ziara, yaani asli ya ziara (kuyatembelea) na si kukithirisha. Na hili ni kama mfano wa Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ
”Na Mola wako si dhalimu (hata chembe) kwa waja (Wake).” (41:46)

Allaah Kakataza asli ya dhulma. Allaah (´Azza wa Jalla) Hadhulumu, Hamdhulumu yeyote na wala makusudio yake si kwamba Hakithirishi (kuchupa mipaka). Maana yake ni kwamba sio Mwenye kudhulumu.

Isitoshe, kauli ya kujuzisha (wanawake kuyatembelea makaburi) na kauli ya kukataza. Mwanamke akiacha kuyatembelea makaburi, kipi ambacho kitakuwa kimempita? Hakuna kitachokuwa kimempita isipokuwa jambo lililopendekezwa tu. Jambo lililopendekezwa ndio litakuwa limempita na si kwamba atakuwa ameacha jambo la wajibu mpaka achukuliwe (aadhibiwe). Atakuwa ameacha jambo lililopendekezwa.

Ama lau atayatembelea, atakuwa amejiingiza katika laana. Kwa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Amewalaani wanawake wenye kuzuru makaburi.”

Kwa hivyo, kauli hii (ya wanachuoni wanaokataza) ndio ilio salama kuliko ile kauli nyingine. Kwa kuwa ndani yake kuna usalama wa kujisababishia laana na adhabu.

Kwa hivyo, kuyatembelea makaburi, sawa ikiwa ni kaburi la Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ya mashahidi au makaburi yoyote duniani ni kwa wanaume peke yao na si kwa wanawake.