Salafiyyuun Ndio Wenye Kuja Na Ukhaliyfah, Sio Khawaarij

Swali: Baadhi ya ndugu wanamaanisha kuwa mfumo wa Salaf ndio utarudisha ukhaliyfah uliomsafi, ambao ulielezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kutumia dalili ya Hadiyth ya Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu) kuhusiana na viongozi: "Utume utakuwa kati yenu kwa muda ambao Allaah Atataka. Kisha Allaah Ataunyanyua pale Atapotaka kufanya hivo. Halafu kutakuwa ukhalifah uliomsafi juu ya mfumo wa utume... " mpaka pale aliposema: "Kisha kutakuwa ukhalifah uliomsafi juu ya mfumo wa utume." Wanasema waliosimamisha ukhaliyfah wa kwanza baada ya utume ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na kwamba watakaourudisha tena kabla ya siku ya Qiyaamah ni wale wenye kushikamana na mfumo wa Maswahabah. Hii ina maana, wanavosema, ya kwamba mfumo wa Salaf ndio wenye kuandaliwa na Allaah kwa yale ambayo Waislamu wanatamani... al-Albaaniy: إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ "Hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka." (51:23) Swali: Je, utumiaji wa dalili kwa Hadiyth hii... al-Albaaniy: إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ "Hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka." (51:23) Hii ndio dhahiri. Swali: Wanasema kuwa yatayosimamisha ukhaliyfah huu ni kule kuhakikisha uabudu kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) katika ardhi. Wanatumia dalili kwa Hadiyth ya al-Bukhaariy na Muslim iliyopokelewa na Abu Hurayrah na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa mnasaba wa kuwapiga vita mayahudi ambapo mpaka mti na jiwe vitasema: "Ee Muislamu! Ee mja wa Allaah!" Uhakikishaji wa uabudu kwa Allaah ndio ambao utaoleta matokea ya nusura, kusimamisha... al-Albaaniy: Hili halina shaka yoyote. Pia ndio ambao unaleta matokeo ya miujiza. Hapa ndio unaona mfano wa upotevu wa Waislamu wakati wanapofikiria kuwa watashinda kama jinsi wanavoshindana makafiri wao kwa wao kwa msaada wa nguvu za kimali. Wanafikiria kuwa wanaweza kuwashinda makafiri kwa mfano huo huo wa nguvu za kimali. Hili tu linatosheleza kuona jinsi wanavojifananisha na makafiri. Kwao hakuna: إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ "Mkinusuru [Dini ya] Allaah, Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu." (47:07) Kwao hakuna kitu kama hichi. Makafiri hawana jengine zaidi ya nguvu na silaha. Kwa ajili hiyo utaona jinsi wanavovuka mipaka; wanaona kuwa wana silaha nyingi zaidi kuliko wengine. Kwa upande mwingine Muislamu hujiandaa, kama Alivyosema Allaah (Ta´ala): وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ "Na waandalieni nguvu [silaha] zozote mziwezazo." (08:60) Lakini mtu asifikirie kuwa nguvu hapa ndio msingi wa kila kitu. Kama jinsi vilevile haitakikani kufikiria kuwa kufanya kazi kwa sababu ya riziki ndio kila kitu: وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ "Na yeyote [yule] anayemcha Allaah, [basi Allaah] Atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo]. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii." (65:02-03) Mzungumzaji: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy Chanzo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930) Toleo la: 10-12-2012 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Swali: Baadhi ya ndugu wanamaanisha kuwa mfumo wa Salaf ndio utarudisha ukhaliyfah uliomsafi, ambao ulielezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kutumia dalili ya Hadiyth ya Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anhu) kuhusiana na viongozi:

“Utume utakuwa kati yenu kwa muda ambao Allaah Atataka. Kisha Allaah Ataunyanyua pale Atapotaka kufanya hivo. Halafu kutakuwa ukhalifah uliomsafi juu ya mfumo wa utume… ” mpaka pale aliposema: “Kisha kutakuwa ukhalifah uliomsafi juu ya mfumo wa utume.”

Wanasema waliosimamisha ukhaliyfah wa kwanza baada ya utume ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na kwamba watakaourudisha tena kabla ya siku ya Qiyaamah ni wale wenye kushikamana na mfumo wa Maswahabah. Hii ina maana, wanavosema, ya kwamba mfumo wa Salaf ndio wenye kuandaliwa na Allaah kwa yale ambayo Waislamu wanatamani…

al-Albaaniy:

إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
“Hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka.” (51:23)

Swali: Je, utumiaji wa dalili kwa Hadiyth hii…

al-Albaaniy:

إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
“Hakika hiyo ni Haki kama mnavyotamka.” (51:23)

Hii ndio dhahiri.

Swali: Wanasema kuwa yatayosimamisha ukhaliyfah huu ni kule kuhakikisha uabudu kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) katika ardhi. Wanatumia dalili kwa Hadiyth ya al-Bukhaariy na Muslim iliyopokelewa na Abu Hurayrah na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa mnasaba wa kuwapiga vita mayahudi ambapo mpaka mti na jiwe vitasema:

“Ee Muislamu! Ee mja wa Allaah!”

Uhakikishaji wa uabudu kwa Allaah ndio ambao utaoleta matokea ya nusura, kusimamisha…

al-Albaaniy: Hili halina shaka yoyote. Pia ndio ambao unaleta matokeo ya miujiza. Hapa ndio unaona mfano wa upotevu wa Waislamu wakati wanapofikiria kuwa watashinda kama jinsi wanavoshindana makafiri wao kwa wao kwa msaada wa nguvu za kimali. Wanafikiria kuwa wanaweza kuwashinda makafiri kwa mfano huo huo wa nguvu za kimali. Hili tu linatosheleza kuona jinsi wanavojifananisha na makafiri. Kwao hakuna:

إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ
“Mkinusuru [Dini ya] Allaah, Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu.” (47:07)

Kwao hakuna kitu kama hichi. Makafiri hawana jengine zaidi ya nguvu na silaha. Kwa ajili hiyo utaona jinsi wanavovuka mipaka; wanaona kuwa wana silaha nyingi zaidi kuliko wengine. Kwa upande mwingine Muislamu hujiandaa, kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):

وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ
“Na waandalieni nguvu [silaha] zozote mziwezazo.” (08:60)

Lakini mtu asifikirie kuwa nguvu hapa ndio msingi wa kila kitu. Kama jinsi vilevile haitakikani kufikiria kuwa kufanya kazi kwa sababu ya riziki ndio kila kitu:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ
“Na yeyote [yule] anayemcha Allaah, [basi Allaah] Atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo]. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Mzungumzaji: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Chanzo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
Toleo la: 10-12-2012
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Alama za Qiyaamah
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Wednesday 10th, December 2014