Salafiyyuun – Khawaarij Kwa Walinganiaji, Murji-ah Kwa Viongozi

Mtu huyu - ´Abdur-Razzaaq ash-Shaayjiy – anawaita – yaani Salafiyyuun – kuwa ni Khawaarij kwa kadhaa na Murji-ah kwa kadhaa na kadhalika. Je, hii ndio adabu ya Qur-aan isemayo: وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ “Na wala msiitane majina ya utani (mabaya).” (49:11) Mtu huyu ima akawa ni mjinga au mgonjwa, chuki na hasadi. Tunamuomba Allaah Amfunze ikiwa ni mjinga na Amponye ikiwa amesibiwa na kitu katika maradhi hayo. Kwa masikitiko makubwa yameanza kuonekana kwa vijana wengi ambao pengine wanaweza kuwa wanafahamu kitu katika Qur-aan na Sunnah wakati huo huo wamekosa mambo mengi. Na ikiwa wamejifunza sana, basi hawakulelewa malezi ya Kiislamu sahihi. Kwa ajili hiyo ni lazima kwetu kujua kwamba elimu kwa uwiano wa matendo ni kama njia kwa uwiano wa malengo. Yule mwenye kujua pasina kutenda ni kama mfano wa mwenye kutawadha pasina kuswali. Wudhuu wake huu hautomfidisha kitu na wala hautomkurubisha kwa Allaah.

Mtu huyu – ´Abdur-Razzaaq ash-Shaayjiy – anawaita – yaani Salafiyyuun – kuwa ni Khawaarij kwa kadhaa na Murji-ah kwa kadhaa na kadhalika. Je, hii ndio adabu ya Qur-aan isemayo:

وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ
“Na wala msiitane majina ya utani (mabaya).” (49:11)

Mtu huyu ima akawa ni mjinga au mgonjwa, chuki na hasadi. Tunamuomba Allaah Amfunze ikiwa ni mjinga na Amponye ikiwa amesibiwa na kitu katika maradhi hayo. Kwa masikitiko makubwa yameanza kuonekana kwa vijana wengi ambao pengine wanaweza kuwa wanafahamu kitu katika Qur-aan na Sunnah wakati huo huo wamekosa mambo mengi. Na ikiwa wamejifunza sana, basi hawakulelewa malezi ya Kiislamu sahihi. Kwa ajili hiyo ni lazima kwetu kujua kwamba elimu kwa uwiano wa matendo ni kama njia kwa uwiano wa malengo. Yule mwenye kujua pasina kutenda ni kama mfano wa mwenye kutawadha pasina kuswali. Wudhuu wake huu hautomfidisha kitu na wala hautomkurubisha kwa Allaah.