Salafiyyah Ni Safina Ya Nuuh

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) anasema: "Hautofaulu mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale waliyofaulu kwayo wa mwanzo wao." Ni kipi kilichowafanya wakafaulu wa mwanzo wao ni kitu gani? Qur-aan na Sunnah na kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuifanyia kazi Qur-aan na Sunnah. Haya ndiyo yaliwafanya wakafaulu watu wa mwanzo wa Ummah huu. Mwisho wa Ummah huu hautofaulu vilevile isipokuwa kwa yale yaliyowafanya wakafaulu wa mwanzo wao. Yule ambaye anataka kuokoka ni juu yake kusoma Manhaj ya Salaf, kuifuata na kulingania kwayo. Hii ndio njia ya uokovu. Ni safina ya Nuuh (´alayhis-Salaam). Yule mwenye kupanda ndani yake anaokoka na yule asiyefanya hivo anaangamia na kuzama kwenye upotevu. Hatuna uokovu sisi isipokuwa kwa madhehebu ya Salaf. Na hatuwezi kujiufunza madhehebu ya Salaf isipokuwa kwa kuisoma, kuisomesha pamoja na kumuomba Allaah: اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ "Tuongoze katika njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha" (01:06-07) Tunamuomba Allaah Atuongoze kwayo na Atuthibitishe juu yake.

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) anasema:

“Hautofaulu mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa yale waliyofaulu kwayo wa mwanzo wao.”

Ni kipi kilichowafanya wakafaulu wa mwanzo wao ni kitu gani? Qur-aan na Sunnah na kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuifanyia kazi Qur-aan na Sunnah. Haya ndiyo yaliwafanya wakafaulu watu wa mwanzo wa Ummah huu. Mwisho wa Ummah huu hautofaulu vilevile isipokuwa kwa yale yaliyowafanya wakafaulu wa mwanzo wao. Yule ambaye anataka kuokoka ni juu yake kusoma Manhaj ya Salaf, kuifuata na kulingania kwayo. Hii ndio njia ya uokovu. Ni safina ya Nuuh (´alayhis-Salaam). Yule mwenye kupanda ndani yake anaokoka na yule asiyefanya hivo anaangamia na kuzama kwenye upotevu. Hatuna uokovu sisi isipokuwa kwa madhehebu ya Salaf.

Na hatuwezi kujiufunza madhehebu ya Salaf isipokuwa kwa kuisoma, kuisomesha pamoja na kumuomba Allaah:

اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ
“Tuongoze katika njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha” (01:06-07)

Tunamuomba Allaah Atuongoze kwayo na Atuthibitishe juu yake.