Salafiyyah Isiokuwa Na Maana

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawasifia Salaf pale aliposema: "Watu bora ni wa karne yangu. Kisha wale watakaofuatia. Kisha wale watakaofuatia." Wao ni kiigizo cha Ummah huu. Manhaj yao inatakiwa kuwa njia inayopitwa juu yake katika ´Aqiydah yao, mu´amala wao, tabia yao na mambo yao mengine yote. Manhaj hii imechukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah kwa kule kueshi kwao karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uteremsho na kusoma kwao kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni karne bora. Manhaj yao ni Manhaj bora. Kwa ajili hii Waislamu wanatakiwa kuwa na pupa kutaka kujua Manhaj yao ili waifuate. Kwa kuwa haiwezekani kufuata Manhaj yao isipokuwa kwa elimu na kuisoma na kuifanyia kazi. Na kwa ajili hii Kasema Allaah (Jalla wa ´Alaa): وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ "Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan." (09:100) Bi maana kuwafuata kwa kuwaiga. Na mtu hawezi kuwafuata kwa wema isipokuwa mpaka mtu asome madhehebu yao na Manhaj yao. Ama kujinasibisha tu kwa Salaf na Salafiyyah bila ya kuwa na maarifa kwayo na Manhaj yake, hili halifidisha kitu bali ni jambo linaweza kudhuru. Ni lazima mtu kujua Manhaj ya Salaf-us-Swaalih. Na kwa ajili hii ndio maana Ummah huu ulikuwa unasoma Manhaj ya Salaf-us-Swaalih na wanaifuata kizazi baada ya kizazi. Ilikuwa inasomeshwa kwenye Misikiti, Madaaris na vyuo vikuu. Hii ndio Manhja ya Salaf-us-Swaalih na hii ndio njia ya kujifunza nayo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawasifia Salaf pale aliposema:

“Watu bora ni wa karne yangu. Kisha wale watakaofuatia. Kisha wale watakaofuatia.”

Wao ni kiigizo cha Ummah huu. Manhaj yao inatakiwa kuwa njia inayopitwa juu yake katika ´Aqiydah yao, mu´amala wao, tabia yao na mambo yao mengine yote. Manhaj hii imechukuliwa kutoka katika Qur-aan na Sunnah kwa kule kueshi kwao karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na uteremsho na kusoma kwao kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni karne bora. Manhaj yao ni Manhaj bora. Kwa ajili hii Waislamu wanatakiwa kuwa na pupa kutaka kujua Manhaj yao ili waifuate. Kwa kuwa haiwezekani kufuata Manhaj yao isipokuwa kwa elimu na kuisoma na kuifanyia kazi. Na kwa ajili hii Kasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiriyn (waliohajiri kutoka Makkah), na Answaar (wakaazi wa Madiynah waliowasaida na kuwanusuru Muhaajiriyn), na wale waliowafuata kwa ihsaan.” (09:100)

Bi maana kuwafuata kwa kuwaiga. Na mtu hawezi kuwafuata kwa wema isipokuwa mpaka mtu asome madhehebu yao na Manhaj yao. Ama kujinasibisha tu kwa Salaf na Salafiyyah bila ya kuwa na maarifa kwayo na Manhaj yake, hili halifidisha kitu bali ni jambo linaweza kudhuru. Ni lazima mtu kujua Manhaj ya Salaf-us-Swaalih. Na kwa ajili hii ndio maana Ummah huu ulikuwa unasoma Manhaj ya Salaf-us-Swaalih na wanaifuata kizazi baada ya kizazi. Ilikuwa inasomeshwa kwenye Misikiti, Madaaris na vyuo vikuu. Hii ndio Manhja ya Salaf-us-Swaalih na hii ndio njia ya kujifunza nayo.