Salafiyyah Inanufaisha Wote Na Haimdhuru Yeyote

´Allaamah al-Waadi´iy: Tunataraji wayemeni wakubali Salafiyyah. Ambayo ni Da´wah kutoka katika Kitabu cha Allaah na kwenda katika Kitabu cha Allaah na kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah kwenda katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Da´wah isiyokuwa na madhara kwa mtawala. Na wala haidhuru jamii. Da´wah inayomtengeneza mtawala na rai. Da´wah ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sisi hatuwaiti watu kutufuate. Mimi binafsi naona sio mtu wa kufuatwa. Na wala hatuwaiti watu pia watufuate kichwa mchunga. Kwa hakika kufuata kichwa mchunga ni haramu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala): اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03) Na Anasema (Subhaanahu wa Ta´ala): وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ”Na wala usiyafuate (kusema au kufanya) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo daima vitaulizwa (Siku ya Qiyaamah).” (17:36)

´Allaamah al-Waadi´iy:

Tunataraji wayemeni wakubali Salafiyyah. Ambayo ni Da´wah kutoka katika Kitabu cha Allaah na kwenda katika Kitabu cha Allaah na kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah kwenda katika Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni Da´wah isiyokuwa na madhara kwa mtawala. Na wala haidhuru jamii. Da´wah inayomtengeneza mtawala na rai. Da´wah ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sisi hatuwaiti watu kutufuate. Mimi binafsi naona sio mtu wa kufuatwa. Na wala hatuwaiti watu pia watufuate kichwa mchunga. Kwa hakika kufuata kichwa mchunga ni haramu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
”Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu (Qur-aan na Sunnah) na wala msifuate badala Yake (Allaah), awliyaa (marafiki wapenzi, walinzi wanaokuamrisheni kufru, shirki). Ni machache mnayoyakumbuka.” (07:03)

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا
”Na wala usiyafuate (kusema au kufanya) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo daima vitaulizwa (Siku ya Qiyaamah).” (17:36)