Salafiy Hafanyi Hivo

Watu hawa wanaraddiwa kwa kuwaangalia wale walioshikamana na mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Wanaraddi propaganda hizi; wanajiita ´Salafiyyah wanaotoka katika Jihaad` [Salafiyyah al-Jihaadiyyah] au ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` [Salafiyyah ad-Da´wah wal-Qitaal]. Wanaowaraddi ni wanachuoni wa Da´wah ya Salafiyyah ya haki. al-Albaaniy aliwaraddi. Ibn Baaz aliwaraddi. Ibn ´Uthaymiyn aliwaraddi. Haya yanatajwa kwa mnasaba wa vita Algeria na baadaye Afghanistan. Mwanzoni kulikuwa Da´wah ya al-Ikhwaan na Da´wah ya Salafiyyah. Baada ya hapo wakaanza wao wenyewe kujiita ´Salafiyyah`. Mnajua ni kwa nini? Kwa sababu wanajua ´Salafiy` ni neno tukufu na linakubaliwa kwa Ahl-ut-Tawhiyd was-Sunnah. Lau wangelijiita ´al-Ikhwaan al-Muslimuun` hakuna yeyote angeliwaendea. Lau wangelijiita ´Khawaarij` hakuna yeyote angeliwaendea. Hivyo ndio wakawa wameanza kujiita ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` na ´Salafiyyah wanaotoka kwenda katika Jihaad`. Yote haya ili kuweka upotevu gizani. Je, katika Salafiyyah hakuna Jihaad mpaka hawa wawe na ulazima wa kutoka kwenda katika Jihaad? Ni katika uongo mkubwa na batili kubwa. Dalili ya hilo ni nchi hii. Imejengwa juu ya nini? Sio juu ya Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab? Ni nani aliyepigana kwa ajili yake? Je, sio Ahl-us-Sunnah? Walifanya hivo kwa ufalme wote tatu. Da´wah ilienea katika ufalme wa kwanza na Saudi Arabia ikawa imeanguka kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) Alitaka hivo. Kisha ikarudi katika msingi wake sahihi ambapo ilianguka tena. Kisha ikarudi katika msingi wake sahihi tena. Inawalingania watu katika kusahihisha Dini na kuwatoa katika Shirki, ukhurafi na ujinga. Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) aliwapa utawala. Viongozi na wanachuoni walikuwa sawa sawa. Ama kuhusiana na watu hawa, hawako na wanachuoni wala viongozi. Hawako na wanachuoni. Hawako na viongozi. Wanawakufurisha wanachuoni na watawala na wanawaponda wanachuoni. Hii ndio Salafiyyah? Ni Salafiyyah sampuli gani? Salafiyyah haiko kwa makundi na mapote. Salafiyyah ni kundi limoja kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaita hivo: “Na Ummah wangu utagawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wanaofuata yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.” Katika upokezi mwingine: “Jamaa´ah.” Ni kundi limoja tu na sio makundi mengi. Yule mwenye kwenda kinyume na wao sio katika wao. Ukiwapeleleza hawa wanaojiita ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` na ´Salafiyyah wanaotoka kwenda katika Jihaad` utaona kuwa ni al-Ikhwaan al-Muslimuun tawi la Qutbiyyah. Hawana lolote linalohusiana na Salafiyyah. Dalili ya hilo ukichunguza historia yao utaona jinsi al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na Ibn Baaz wanavyowanasihi na kuwakemea kwa uasi wao na ufisadi wao wakati wanapowapiga vita watawala, kumwaga damu, kuteka nyara wanawake na kuwaua watu wasiokuwa na hatia. Je, Salafiy anafanya hivo? Je, haya yanafanywa na Muislamu mwenye akili? Kamwe. Ni batili iliokuwa kubwa. Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=EcbgpflKWRs Toleo la: 13-09-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Watu hawa wanaraddiwa kwa kuwaangalia wale walioshikamana na mfumo wa Salaf-us-Swaalih. Wanaraddi propaganda hizi; wanajiita ´Salafiyyah wanaotoka katika Jihaad` [Salafiyyah al-Jihaadiyyah] au ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` [Salafiyyah ad-Da´wah wal-Qitaal]. Wanaowaraddi ni wanachuoni wa Da´wah ya Salafiyyah ya haki. al-Albaaniy aliwaraddi. Ibn Baaz aliwaraddi. Ibn ´Uthaymiyn aliwaraddi. Haya yanatajwa kwa mnasaba wa vita Algeria na baadaye Afghanistan. Mwanzoni kulikuwa Da´wah ya al-Ikhwaan na Da´wah ya Salafiyyah. Baada ya hapo wakaanza wao wenyewe kujiita ´Salafiyyah`. Mnajua ni kwa nini? Kwa sababu wanajua ´Salafiy` ni neno tukufu na linakubaliwa kwa Ahl-ut-Tawhiyd was-Sunnah. Lau wangelijiita ´al-Ikhwaan al-Muslimuun` hakuna yeyote angeliwaendea. Lau wangelijiita ´Khawaarij` hakuna yeyote angeliwaendea. Hivyo ndio wakawa wameanza kujiita ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` na ´Salafiyyah wanaotoka kwenda katika Jihaad`. Yote haya ili kuweka upotevu gizani. Je, katika Salafiyyah hakuna Jihaad mpaka hawa wawe na ulazima wa kutoka kwenda katika Jihaad? Ni katika uongo mkubwa na batili kubwa. Dalili ya hilo ni nchi hii. Imejengwa juu ya nini? Sio juu ya Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab? Ni nani aliyepigana kwa ajili yake? Je, sio Ahl-us-Sunnah? Walifanya hivo kwa ufalme wote tatu. Da´wah ilienea katika ufalme wa kwanza na Saudi Arabia ikawa imeanguka kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) Alitaka hivo. Kisha ikarudi katika msingi wake sahihi ambapo ilianguka tena. Kisha ikarudi katika msingi wake sahihi tena. Inawalingania watu katika kusahihisha Dini na kuwatoa katika Shirki, ukhurafi na ujinga. Kwa ajili hiyo ndio maana Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) aliwapa utawala. Viongozi na wanachuoni walikuwa sawa sawa.

Ama kuhusiana na watu hawa, hawako na wanachuoni wala viongozi. Hawako na wanachuoni. Hawako na viongozi. Wanawakufurisha wanachuoni na watawala na wanawaponda wanachuoni. Hii ndio Salafiyyah? Ni Salafiyyah sampuli gani?

Salafiyyah haiko kwa makundi na mapote. Salafiyyah ni kundi limoja kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaita hivo:

“Na Ummah wangu utagawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni wale wanaofuata yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.”

Katika upokezi mwingine:

“Jamaa´ah.”

Ni kundi limoja tu na sio makundi mengi. Yule mwenye kwenda kinyume na wao sio katika wao. Ukiwapeleleza hawa wanaojiita ´Salafiyyah wanaotoka kulingania na kupigana` na ´Salafiyyah wanaotoka kwenda katika Jihaad` utaona kuwa ni al-Ikhwaan al-Muslimuun tawi la Qutbiyyah. Hawana lolote linalohusiana na Salafiyyah. Dalili ya hilo ukichunguza historia yao utaona jinsi al-Albaaniy, Ibn ´Uthaymiyn na Ibn Baaz wanavyowanasihi na kuwakemea kwa uasi wao na ufisadi wao wakati wanapowapiga vita watawala, kumwaga damu, kuteka nyara wanawake na kuwaua watu wasiokuwa na hatia. Je, Salafiy anafanya hivo? Je, haya yanafanywa na Muislamu mwenye akili? Kamwe. Ni batili iliokuwa kubwa.

Mzungumzaji: Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=EcbgpflKWRs
Toleo la: 13-09-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Ikhwaan Muslimuun
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Saturday 13th, September 2014