Ruduud Hazifarikanishi Ummah – Bali Zinawafanya Watu Kuwa Na Umoja

Kosa halikubaliwa kwa yule mwenye kuja nalo. Haijalishi kitu ni nani. Sisi tunawapiga Radd watu wa Bid´ah hata Ahl-us-Sunnah. Mmoja katika Ahl-us-Sunnah akikosea tunampiga Radd hata kama atakuwa ni katika Ahl-us-Sunnah na hata kama atakuwa ni katika wanachuoni wakubwa. Kosa linaraddiwa. Hii haina maana ni kufarikanisha baina ya Ummah. Kinyume chake huku ni kuufanya Ummah kuwa na umoja. Kwa sababu Ummah hauwezi kuwa na umoja isipokuwa juu ya mfumo sahihi. Ama ikiwa watu wana mifumo iliyopinda na makosa, Ummah hauwezi kuwa na umoja. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema: كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ “Kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.” (23:53) Huku ni kwa njia ya kuwakemea. فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ “(Lakini) Wakalikatakata jambo lao (la Dini) baina yao mapande mbali mbali, kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.” (23:53) Huku ni kwa njia ya kuwakemea. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema: وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ “Na kwamba hakika huu Ummah wenu, ni Ummah mmoja Nami ni Mola wenu, basi Nicheni.” (23:52) Aayah nyingine inasema: إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ “Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, basi niabuduni.” (21:92) Ummah ni mmoja. Ummah hauwezi kufuata isipokuwa mfumo ulio salama uliosalimika na makosa, mambo ya uzushi na upindaji. Kuwafanya watu wawe na umoja sio kwa kuwakusanya tu, kama wanavyofikiria baadhi ya watu. Haiwi namna hii. Kuwanya watu wawe na umoja inakuwa kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. Hakuna kitu kitachowafanya watu kuwa na umoja isipokuwa kwa kufuata Qur-aan na Sunnah na mwenye kukosea arejee katika kosa lake. Ni lazima iwe namna hii. Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=7bAUKS4HdzA Toleo la: 07-09-2014 Imefasiriwa na: Wanachuoni.com

Kosa halikubaliwa kwa yule mwenye kuja nalo. Haijalishi kitu ni nani. Sisi tunawapiga Radd watu wa Bid´ah hata Ahl-us-Sunnah. Mmoja katika Ahl-us-Sunnah akikosea tunampiga Radd hata kama atakuwa ni katika Ahl-us-Sunnah na hata kama atakuwa ni katika wanachuoni wakubwa. Kosa linaraddiwa. Hii haina maana ni kufarikanisha baina ya Ummah. Kinyume chake huku ni kuufanya Ummah kuwa na umoja. Kwa sababu Ummah hauwezi kuwa na umoja isipokuwa juu ya mfumo sahihi. Ama ikiwa watu wana mifumo iliyopinda na makosa, Ummah hauwezi kuwa na umoja. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
“Kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.” (23:53)

Huku ni kwa njia ya kuwakemea.

فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
“(Lakini) Wakalikatakata jambo lao (la Dini) baina yao mapande mbali mbali, kila kundi kwa waliyokuwa nayo linafurahia.” (23:53)

Huku ni kwa njia ya kuwakemea. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ
“Na kwamba hakika huu Ummah wenu, ni Ummah mmoja Nami ni Mola wenu, basi Nicheni.” (23:52)

Aayah nyingine inasema:

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ
“Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Mola wenu, basi niabuduni.” (21:92)

Ummah ni mmoja. Ummah hauwezi kufuata isipokuwa mfumo ulio salama uliosalimika na makosa, mambo ya uzushi na upindaji.

Kuwafanya watu wawe na umoja sio kwa kuwakusanya tu, kama wanavyofikiria baadhi ya watu. Haiwi namna hii. Kuwanya watu wawe na umoja inakuwa kwa kufuata Qur-aan na Sunnah. Hakuna kitu kitachowafanya watu kuwa na umoja isipokuwa kwa kufuata Qur-aan na Sunnah na mwenye kukosea arejee katika kosa lake. Ni lazima iwe namna hii.

Mzungumzaji: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Chanzo: https://www.youtube.com/watch?v=7bAUKS4HdzA
Toleo la: 07-09-2014
Imefasiriwa na: Wanachuoni.com


  • Kitengo: Uncategorized , Manhaj
  • Mfasiri: https://wanachuoni.com
  • Imechapishwa: Sunday 7th, September 2014